Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Tarehe 23 Februari Waumini wote mnaalikwa kusali na kufunga kwa ajili ya amani

Baba Mtakatifu francisko aliomba kusali na kufunga kwa ajili ya amani duniani tarehe 23 Februari 2018 - RV

22/02/2018 16:23

Siku ya sala na kufunga kwa ajili ya amani tarehe 23 Februari 2018 ni dunia  nzima inaalikwa kusali kwa ajili ya amani ya Jamhuri ya Demokrasia  ya  Congo, Sudan ya Kusini na mahali popote penye ghasia vurugu na vita kwa mujibu wa mapendekezo ya Baba Mtakatifu Francisko.

Padre Padre Paul Samasumo wa Vatican News tarehe 20 Februari amehojiana na Askofu Edward Hiiboro Kussala wa Jimbo la Tombura Yambio nchini Sudan  Kusini  ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Sudan kueleza kwa ufupi juu ya mgogoro huo.

Katika mahojiano naye Askofu Kussala anachora picha halisi  ya hali halisi ya nchi hiyo ambapo mgogoro ni kati ya Rais Salva Kiir wa kusini Sudan ambaye alianza vita na Makamu wa Rais aliyeng’atuka Bwana Riek Machar tangu 2013.

Yeye binafsi anaamini katika nguvu ya sala, zinaweza kubadili mambo, wakati huo huo akitoa hata wito kwa jumuiya ya kimataifa ili kusaidia nchi ya Sudan ya kusini kufikia amani kamili  bila kusahau kutoa wito kwa  wote katika  kusaidia vifaa  na msaada mbalimbali kwa ajili wimbi kubwa la  wakimbizi waliorundikana ndani na nje ya nchi ya Sudan ya Kusini.

Mwisho amewakumbusha kwa namna ya pekee kuungana zaidi na wito wa Baba Mtakatifu Francisko tarehe 23 Februari kusali kwa pamoja duniani nzima ili Bwana aweza kutoa amani
Na vilevile katika kuungana na siku ya sala na kufunga kwa ajili ya amani , wafranciskani wa Konveti ya Mtakatifu Francisko  wa Asisi, pamoja na Meza ya amani, wanaawalika wazalendo wote, vyama na taasisi mbalimbali duniani kuungana kwa pamoja katika siku ya sala na kufunga kwa ajili hiyo.


Siku ya sala na kufunga kwa ajili ya amani kwa mujibu wa Baba Mtakatifu, ni fursa mpya na muhimu kwa ajili ya kuwasha dhamiri na kutafakari juu ya migogoro mingi ambayo inaendelea kusabisha majanga ya vifo vya maisha ya binadamu.

Wito kwa naana ya pekee wanasema, ni kwa ajili ya wote na zaidi kwa vyombo vya habari , kutangaza kwa wingi juu ya wito huo katika siku hiyo maalumu tarehe 23 Februari. Hadi sasa ni  nchi 36 ambazo zinahusika na matukio ya vita, migogoro ya silaha, ikiwa ni pamoja na nchi ya  Kidemokrasia ya Congo ,na sudan ya Kusini mahali ambapo  Papa Francisko amependa kusali kwa namna ya pekee.

Kujikita katika kutafakari hali halisi za watu wanaoishi, wanaoteseka na kufa katika nchi hizi ni jambo muhimu kwa kila mmoja kuwa na dhamiri wazi ya kufanya lolote kuanzia sala, kufunga na kutoa msaada wa dhati.

Aidha nia kuu ya sala ya tarehe 23 Februari ni kutaka kuwasha tafakari za amani juu ya vurugu na vita  na kuzima mianga ya matumizi mabaya yanayoendelea kuharibu mazingira nyumba yetu ya pamoja.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

22/02/2018 16:23