2018-02-20 14:38:00

Milioni 1,5 ya rosari zinatengenzwa Nchi Takatifu kwa ajili ya Vijana!


Mpango unaiitwa AveJmj ambao unatarajia kutoa milioni moja na nusu ya Rosari za miti ya mizeituni zinazotengeneza huko Betlehemu na familia hitaji, kwa ajili ya vijana ambao wataweza kushiriki Siku ya Vijana duniani huko Panama kuanzia tarehe 22-27 Januari 2019, lengo la kutaka kuwatia  moyo wasali kwa ajili ya amani.

Shughuli hii imeanzishwa kutokana na kujibu shauku ya Baba Mtakatifu Francisko,hasa ile ya  kusali kwa ajili ya  amani duniani kwa namna ya pekee katika nchi ya Yerusalem na nchi zote za mashariki, mahali ambapo Askofu mstaafu  Pierre Bürcher wa Reykjavik ndiye mwamasishaji mkuu wa mpango huo.

Katika mantandao wa nchi Takatifu Net, Askofu Mstaafu Pierre Bürcher, anaelezea kwanini kuchaguliwa jina la mpango wa AveJmj , mahali ambapo anafafanua kuwa “Ave” ni kuelezea sala ya Rosari ya Maria, wakati huo huo elufi tatu za mwanzo yaani “Jmj” zikiwa na maana ya Siku ya vijana lakini pia  ni elfu zinazo anza na  majina ya (Jesus Joseph and Mary) yaani Yesu, Yosefu na Maria!

Askofu  mstaafu Bürcher ni mjumbe wa Baraza la kipapa kwa ajili Makanisa ya Mashariki na kuandaa shughuli za nchi Takatifu tangu mwaka 2004. Anaelezea juu ya kuitikia kwa namna ya pekee  matashi ya Baba Mtakatifu anayewaalika vijana washiriki Siku ya Vijana Panama na kusali rosari kwa ajili ya Amani. Askofu huyo anasema mara baada ya kuwasiliana na Askofu Mkuu wa Panama, Monsinyo José Domingo Ulloa ameelezwa kuwa uwanja wa nakutano ya siku ya vojana kwa mwaka 2019 inakadiriwa kuwapokea watu laki 5. 

Kutokana na idadi hiyo Akofu Buch Bürcher amefikiria kwamba  kila kijana atakayeshiriki basi atapokea rosari 3: moja kwa ajili yake na mbili kumzawadia atakayejenga  urafiki hapo Panama na moja itakuwa ya kupeleka nchini kwake  mara baada ya maadhimisho hayo. Rosari hizo zitafungwa katika paketi moja ikiwa na picha ya Baba Mtakatifu Francisko. Aidha anasema, Rosari zitakazotengezwa kutoka nchi Takatifuzikuwa tayari mwezi Oktoba mwaka huu na kupelekwa katika Port ya Ashdod (Israel) tayari kusafirishwa nchini Panama.

Kwa sasa ni vituo 11 vya ujasiliamali kati ya Beit Sahour, Beit Jala na Betlemme ambavyo vinafanya kazi ili kuwezesha kukamilisha  kazi hii inayotengenezwa kwa miti ya mizeituni. Rosari hizi zinatengenezwa kwa aina ya mtindo unaopendwa na vijana, yaani za kuvaa mkono. 

Taarifa zaidi inasema kuwa, ili vijana vijana waweze kutambua zaidi na kujifunza kusali Rosari wameamua kutengeneza hata App  ambao vijana wengi wanatumia mitandao ya kijamii aweze kupta maelekezo na kujifunza zaidi. Msalaba wa rosari hiyo utakuwa na chapa ya maneno katika sehemu zote mbili “Betlehemu na JMJ 2019” !

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.