2018-02-19 12:36:00

Masaa 24 kwa ajili ya Bwana ,mwaka huu hata magerezani


Mwaka wa tano mfululizo kwa ajili ya kusali masaa 24 kwa ajili ya Bwana , mwaka huu hata katika magereza, kwa mujibu wa Kardinali Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha  Unjilishaji mpya, akielezea juu ya utaratibu huo,ulioanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kumaliza mwaka wa Jubilei ya huruma. Kardinali Fisichella anasema, Baba Mtakatifu atakutana hata na wamisionari wa huruma ambao kwa utashi wake wanaendelea kuwa muhimu katika Sakramenti ya kutubio na mapatano katika mabara matano, miaka miwili baada ya Jubilei ya huruma.

Tarehe za kufanya sala hiyo kwa ajili Bwana imepangawa 9 na 10 Machi, si tu katika makanisa yote katoliki ulimwenguni yatafunguliwa bila kufungwa kwa ajili ya masaa 24 kutoa huduma kwa waamini ambao wanatamani kuungamana na kuabudu Ekaristi Takatifu, bali shughuli hiyo pia itafanyakika katika magereza nchini Italia , mahali ambapo mapadre wa makanisa hayo watakuwapo kuwasaidia kuungama, kwa mujibu wa Kardinali Rino Fischela Mwenyekiti wa Braza la Kipapa kwa ajili ya kuhamsisha uinjilishaji mpya.

Aidha anafafanua kuwa kuabudu masaa 24 kwa Bwana, ni mawao ya moyo wa Papa ambaye katika ujumbe wake wa mwisho wa kwaresima mwaka huu ameelezea pia. Na hivyo Kardinali anasema toleo hilo ambao limefikia mwaka wa tano, tunaweza kusema limekuwa moyo wa Kanisa na kuwa kipindi mwafaka kwa ajili ya Kwaresima. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa mwama huu ameweka zaburi ya 130 , “kwako wewe kuna msamaha”, hivyo utashi ni ule wa kufungua mioyo ili maisha mapya ya Mungu yaweze kuingia ndani ya moyo  na kuubadili na kuwa wenye furaha.

Kama jibu la Kanisa mahalia , kuanzishwa kwa muhimili huu wenye ramani inayotazama majimbo yote duniani kwa ajili ya kutoa  Sakramenti ya Kitubio  na kuabudu, ni muhimu  kwa sababu habari zinazofika kwa njia ya maaskofu katika hija yao na Baba Mtakatifu wanaonesha bayana juu ya masaa 24 kwa ajili ya Bwana inaendelea vizuri.  Hiyo ni ishara muhimu kwa ajili ya wote ili kuweza kufanya uzoefu ambao unaruhusu kujikita kila mmoja katika jimbo binafsi. Kwa njia hiyo katika nchi ya Italia, wamepokea barua kutoka kwa Mkuu wa Magereza, ambaye anaomba huduma hiyo iweze kufunguliwa hata katika magereza zote nchini Italia, ni moja na huduma muhimu, ili kuishi njia ya mapatano na msamaha.

Katika Mwaka wa Jubilei , tumeonja kwa kina ni kwa jinsi gani watu wote wanahitaji huruma ya Mungu, anathibitisha Kardinali Fisichella . Ni safari inayoendelea na yenye ukuu kwa namna ya pekee, ambayo inazidi taratibu kuingia katika jumuiya mbalimbali. Uzoefu wa kusamehewa bila shaka ni uzoefu mzuri ambao kila mmoja anaweza kufanya uzoefu wa maisha, hasa kwa kuomba neema ya msamaha kutoka kwa Baba na kuacha asamehewe na yeye na ndipo  inawezekana kuwa na uwezo wa kupokea msamaha huo na kuwasamehe wengine!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.