Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maisha Ya Kanisa Afrika

TANZIA:Kifo cha Askofu Emmanuel Kanyama wa Jimbo la Dedza nchini Malawi!

Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Malawi anatangaza kifo cha Askofu Emmanuel Kanyama wa jimbo la Dedza kilichotkea tarehe 17 Februari 2018

17/02/2018 12:27

Padre  Henry Saindi, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Malawi anasikitika kutangaza kifo cha Askofu Emmanuel Kanyama wa Jimbo la Dedza, kilichotoke tarehe 17 Februari 2018 nyumbani kwake Kapiri.

Jimbo la Dedza ni jimbo Katoliki nchini Malawi  kikipakana na Jimbo Kuu la Lilongwe. Mwaka 2006 jimbo hilo lilikiwa na idadi ya wabatizwa 459.398 kati ya wakazi 1.173.000 wa jimbo hilo, wakiongozwa na hayati Askofu Emmanuel Kanyama.

Mpango  na taratibu zote za maadhimisho ya misa na kuaga  zitatolewa. Raha ya Milele umpe ee Bwana Askofu Emmanuel Kanyama apumzike kwa Amani. Amina.

Na Sr Angela Rwezaula 

Vatican News

 

17/02/2018 12:27