2018-02-17 16:36:00

Papa afanya uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Kipapa ya kulinda watoto!


Tarehe 17 Febbruari 2018, Baba Mtakatifu amewateua wajumbe  wapya wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya kulinda watoto, vijana na watu walioathirika na nyanyaso kijinisia , ambapo Kardinali O’Malley anaendelea kuwa mwenyekiti wa Tumehiyo. Wengine walioteuliwa ni kutoka katika mabara yote matano wakiwa ni: sista Jane Bertelsen, F.M.D.M. (Uingereza); Sista Arina Gonsalves, R.J.M. (India); Prof. Ernesto Caffo (Italia); Prof. Neville John Owen (Australia); Prof. Benyam Dawit Mezmur (Etiopia);Bw. Nelson Giovanelli Rosendo dos Santos (Brasil); Prof. Myriam Wijlens ( Ukutoka nchi za Ulaya ya kati); Bi Sinalelea Fe'ao (Tonga); Bi. Teresa Kettelkamp (Marekani).

Tume hiyo iliundwa tangu tarehe 22 Machi 2014 kwa Waraka  uliondikwa na Baba Mtakatifu Francisko wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya kulinda  wadogo  ambapo katika maelezo yake mwenyewe anasema, “shughuli maalumu ya mapendekezo ya Papa, ni fursa ya kuanzishwa kwa utetezi wa kulinda  wadogo na wakubwa walioathirika inapaswa kufanywa  haraka iwezekanovyo na kuhakikisha kuwa ualifu uliotendwa na kusababisha waathirika usirudiwe tena katika Kanisa.

Kwa hiyo, Tume ina kazi ya ushauri, ambayo iko chini ya huduma ya Baba Mtakatifu na inajumuisha watu kumi na wanane waliochaguliwa na yeye mwenyewe "kwa muda wa miaka mitatu, kulingana na uthibitisho wa waraka wake. Naye Kardinali O’Malley  Mwenyekiti wa Kamati ya Kipapa kwa ajili ya kulinda  watoto anasema uteuzi uliofanyika utasaidia kutazama kwa mapana duniani  katika ulinizi  wa wadogo na wakubwa walio athirika kwa manyanyaso ya kinjisia.

Amesema hayo kwa waandishi wa habari Vatican na kwamba Baba Mtakatifu Francisko amefikiria kwa undani, kwa kutafakari katika sala kabla ya kufanya  uteuzi wa wajumbe hao. Hata hivyo Baba Mtakatifu amewahikikishia kuendelea na kazi yao ya tume, ambayo wajibu wake pia ni kusaidia hata makanisa mahalia dunia ili kutekeleza juhudi za kutetea majeraha ya watoto wote, vijana na hata watu wazima walio athirika.

 Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.