2018-02-16 16:47:00

Tafakari ya Papa Francisko kwa Makleri wa Roma wakati wa mkutano wao!


Tarehe 15 Februari Baba Mtakatifu Francisko aliondoka asubuhi kutoka katika nyumba ya Mtakatifu Marta kuelekea katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterno Roma, ili kukutana na Mapadre na shemasi wa jimbo la Roma. Katika mkutano wao wa faragha, mapadre wametaka kuuliza maswali ambao walipewa ruhusa kuanzia swali la padre kijana, wa umri wa kati na mwisho padre mzee.

Huu ni mkutano wa utamaduni kila mwanzo wa Kwaresima, makleri wa Roma kukutana, pia ni fursa nzuri kwa Baba Mtakatifu Francisko kutoa  mawazo yake juu ya nini maana ya kuwa kuhani ,na jinsi gani ya kukabiliana na changamoto ambazo zinaikabili dunia ya sasa. Padre kijana ameuliza jinsi gani ya kuishi kikamilifu wito wake. Katika kujibu swali hili Baba Mtakatifu amesema ni swali lenye utata kwa maana vijana ni wengi wanauliza swali la kuishije wito wao kikamilifu mbele ya mambo mengi yanayo wazunguka ambayo hayawapatii nafasi.

Ni lazima kutafuta namna ya kwenda mbele ili kuweza kuishi kwa haki katika shughuli binafsi. Hakuna mtindo unaofafana , maana kila Padre anao mtindo binafsi wa kuishi wito wake, kila mtindo ni tofauti na mwingine, japokuwa ni vema kuhani kuiga ule mtindo wa Yesu Kristo. Ni lazima kutafuta mtindo wa kuishi, kijana asiangalie chnamoto nyini zinazomzungukahasa ambazo zinafunga  milango. Ni  kutafuta mtido wa kipekee. Kwa maana hiyo anawaalika makuhani wazungumze uso kwa uso na Bwana,na kufanya mang’amuzi ambayo yanajikita kutazama dhambi, vikwazo vinavyo wazunguka na hata vile vya utamaduni wa kisasa  wa ubinafsi  vyo hivyo ni lazima kuzungumza navyo. Msamamha daima upo pale pale anasema Baba Mtakatifu.

lakini ni lazima kuzungumza na kutafakari sababu zilizokufanya uangukie  katika dhambi ya kuvuna, wivu, masengenyo, sintojali yule. Njia ya kufanya mazungumzo na kutafakari vizingiti ulivyo navyo ndani na kung’amua ni muhimu katika safari ya kiroho kama kuhani. Mazungumzo hayo na vikwazo hivyo kama mwanakanisa lazima kuvieleza mbele ya shuhuda yaani  mtu ambaye anaweza kukusaidia kung’amua. Kuna umuhimu ya kukabiliana na hayo na mtu mwingine anayeweza kukusadia.

Lazima kumtafuta mtu mwenye hekima akuongoze, akusaidie kuzungumza na  akusaidie katika mang’amuzi. Kwa kuwa kuhani ni mtu ambaye hakuoa, lakini hawezi kuishi peke yake bila kuwa na mtu wa kumsindikiza na kumwongoza kiroho. Jambo hilo ni muhimu sana na linasaidia sana anathibitisha Baba Mtakatifu. Wapo makundi madogo ya mapadre ambao wanasindikiza ndugu makuhani kiroho. Hao wanakutana na kuongea kwa maana ni muhimu kwasababu upweke siyo jambo jema na halipendezi.

Jibu la pili la Baba Mtakatifu limetokana na swali na Padre mwenye umri kati ya miaka 40 na 50. Umri ambao kwa mawazo ya mengi ya kutume kwa kawaida tayari wanakuwa na uzoefu na hemia ya maisha wakati huo afya yao inaanza kuleta shida. Baba Mtakatifu anabaibnisha, kuwa hali hiyo inajitokeza hta kwa upande wa wanandoa.Hivyo maapadre hao waombe ushauri na maelekezo zaidi kwa manaa ni sehemu ya pili ya wito wa Bwana.

Ni kipindi cha vishawishi vingi na kipindi ambacho wengi wanataka na lazima kuwepo mabadiliko. Haiwezekani kuendelea bila ukomavu, ukitoa  nafasi ya kipeo hiki ambacho hakikiishi kamwe utaishia  kuishi maisha ya ndumila kuwili au kuacha kila kitu. Ni lazima kufanya mageuzi , kipindi hiki maana hakuna hata hisia kama zile za  mwanzo, na hayo yote yanatokea hata katika ndoa kwa maana hawana  upendo yaani kama upendo ule wa ujana.

Matatizo yatakuwapo daima mahali ambapo litaisha moja na , kuanza lingine, lakini la muhimu ni kujitafiti ndani na kushirikisha na kutembea kwa pamoja. Kuwa padre wa Jimbo ni lazima kutafuta msaada haraka kwasababu ni hatari kwenda mbele peke yako katika umri huo. Baba Mtakatifu amesema kuwa ni Sala na kuabudu katika kujitoa kwa Bwana na wengine ndiyo njia ya kuwafanya wakue pamoja wakati huo wakiendelea kuwa wadogo yaani unyenyekevu.
Aidha akifiiria juu ya umri na nguvu, amewashauri wajiandae mapema kustaafu kwasababu muda haufiki kwa ghafla lakini ni vizuri kujiandaa kwa kipindi hiki.

Katika maswali mengine kuhusu uzoefu wake akiwa padre, anasema kuwa ki ukweli ni yale ya ukosefu wa lugha ya kutumia katika dunia ya leo ya kitekolojia, lakini nahisi kwamba jambo msingi katika umri huo ni kufanya  kile ambacho inawezekana kwasababu watu wanahitaji uzoefu wao na daima wazee wanalo jambo la kutoa kwa wengine walio wadogo. Ametoa hata uzoefu wake , mara baada ya kumaliza muda wake wa kazi katika anasema alihisi uchungu kwakuwa alifikiri maisha yake yanaishia hapo, lakini alipata nguvu kutokana na kukaa mbele ya tabernakulo na kusali. Hivyo anawshauri umuhimu wa kusali na kusabudu mbele ya ekaristi takatifu wote na hasa wakati wa uzee.

Mwisho Baba Mtakatifu amezungumza juu ya uhusiano kati ya ukuhani, binadamu na jamii ya wakati huu. Kwa njia hiyo anasema ni lazima kutazama hali halisi kama ilivyo, kwasababu hali halisi inaficha jambo ambalo ni kubwa. Ni kutazama hali halisi bila kuwa na hofu na hali hiyo. Anatambua kuwa kuna mwendendo wa kimaadili ambao unakwenda kinyeme na walivyozoea kuona. Lakini pamoja na changamoto zilizopo kuna hata hali nzuri na roho mtakatifu anaweza kubadili hayo yote. Kwa maana ni kweli dunia kwa dhati ni yenye dhambi lakini ni muhimu kung’amua ishara za wakati vizuri!

Naye Askofu Mkuu wa Roma Angelo De Donatsi wakati liturujia ya kitubio kwa mapadre wa Jimbo kabla ya kuzungumza na Baba Mtakatifu amesema, Kama makuhani lazima kujiuzo kwa uwaza kwa namna ya kufanya paroko, mtindo ambao wanaupeleka mbele kwa miaka mengi, je  leo hii bado uko hai?
Ndilo swali nyeti la kujiuliza, akitoa mfano mmoja kuwa, padre mmoja alikuwa akisimulia kuwa alijikuta anafanya kazi uhasibu wa nyumba,wakati yeye alikuwa anataka kufanya kazi ambazo zinahusiana na padre.  Hivyo anasema, sadaka, sala na kufunga ndizo njia ya kwaresima, lakini ikiwa kila kitu kinafanyika kwa amani na kwa saburi bila mahaingiko au kujionesha, pia ni lazima kutafuta kila fursa ya kupatana na ndugu .

Kwaresima siyo kipindi cha changamoto  bali ni upendo, siyo uwanja wa kuchezea, mahali ambapo wanatafuta kupunguza uzito, bali ni duka la madawa, mahali ambapo yupo Daktari Mungu, mtaalamu wa udhaifu wetu ambaye anataka kuponya majeraha yetu na kutupatia uasili mwangavu wa ubatizo. Kwa namana hiyo inahitaji unyenyekevu zaidi ka nguvu ya Roho Mtakatifu na Dakatari uponyesha asiyedanganya kuwa ni mzima.

Askofu Mkuu De Donatis anakumbusha kuwa, Mungu anapenda kile ambacho hakitoi mwanga katika ulimwengu, yaani yatima wanahitaji daima kuendelea kutazamwa,lkuliko watoto walio nawazazi wao. Hata hivyo mitume wa Yesu walikuwa wakifunga chini ya mtazamo wa Baba na siyo katika viwanja. Anayetaka kusifiwa na watu, anabaki kipofu na kupoteza utambulisho wake wa ndani.

Hatuwezi kuishi na haki  isiyo ya kweli, na hivyo ili kuchota ukweli, tunapaswa kuacha kabisa tabia za kutafuta kujulikana.Tutambue na kukubali matashi ambayo yanastahili ili kuweza kuwa wakuhani wema wa  Kanisa la leo linaotambua kuishi utakatifu na mwanga usio zimika.

 Na Sr Angela Rwezaula

Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.