2018-02-16 16:57:00

Salam za Baba Mtakatifu Francisko kwa wanachama wa Pro Petri Sede!


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Februari 2018 amekutana na Kuzungumza na Chama cha Pro Petri Sede kinachojihusha na wajibu wa huduma ya maskini. Amewakaribisha kufika kwao katika hija kwenye kaburi la Mtakatifu Patro ili kuimarisha imani  kwa upendo na utume wao wa kusaidia wahitaji.
Hija yao imefikia katika kipindi cha  mwanzo wa Kwaresima, kipindi ambacho ni cha kujuta  kwa kina ndani ya mioyo kwa imani Katoliki na utume wa Kanisa, ambapo kila mbatizwa anapaswa kuwa mshiriki. Mbele ya kutazama dunia ambayo imejaa utofauti, vurugu, ubinafsi na tabia ya kuona mambo yote ni mabaya. Ni muhimu leo hii kujiuliza maswali ambayo yanasababisha ukosefu wa upendo, iwe katika mioyo  binafsi au mahusiano ya Mungu na watu.

Baba Mtakatifu Francisko anasema hayo ni maswali pia aliyo yaweka katika ujumbe wa Kwaresima 2018 ya kwaba, je upendo umezimika katika mioyo? Ni jambo jema kujitafiti ukweli ! na kutafuta namna ya kufanya  malipizi ambayo Mungu mwenyewe anatoa kwa Kanisa. Sala inatuweka katika njia ya kweli kwa upande wetu na Mungu mwenyewe; tendo la kufunga linatufanya kushirikisha hali halisi kwa watu wengi ambao wanakabiliana na matatizo mengi ya jamii na kuwa karibu na jirani; sadaka ni fursa iliyobarikiwa kwa ajili ya kushrikiana na zawadi ya Mungu na mema kwa ajili ya watoto wake.

Awaalika ktua sana kwa mtindo wa maisha na kutnza hali halisi kwa msaa wa wale ambao wanahitaji. Kazi yao inawayaka daima wawe makini na kujitoa zaidi ya msaada zana, hasa mahusiano ya karibu ya kwasikia wanakalibishwa kwa makiji, heshima na undugu kwa maana bila hili siyo rahisi kuwa na ujasiri wa kushinda na kuendelea mbele.

Baba Mtakatifu anawasifu na kuwashuru, kuwatia moyao kwa upya katika kazi yao ya utumea ambayo wanajikitia barabara kila siku katika sala binafsi na kwa jumuiya . Anawashukur mwa sadaka wanayoitoa kwa mfuasi wa Mtume Petro , kwa mchango wao wa utume wa kimisionari katika Kanisa , kwa maana hiyo wao wanajenga umoja wa kanisa mahali mabapo wote tunaye baba mmoja wa Mbinguni.

Baba Mtakatifu anasema wote kuomba Mungu Bwana katika mioyo yao ili iweze kuendelea kukua katika upendo wa dhati katika dunia, na ili mwishowe migogoro inayosabishwa na mabaya yasiyo na idadi yaweze kusitishwa. Aidha hija yao inaweza kuongeza ndani mwao upendo, kama vile shauku ya kikiri kila siku imani yao na kushuhudia mahali ambapo wanaishi. Anawaalika wote kusali kwa ajili ya vijana katika Sinodi ya Maaskofu ambayo ianjikita kuamsha kwa upya miito ya kikuhani na watawa katika nchi za ona dunia kwa ujumla.

Na anawakabidhi kila mmoja , familia zao na wajumbe wote wa chama kwa maombezi ya Bikira Maria, Mtakatifu Petro na watakatifu wote wa nchi zao  na mwisho kuwabariki kwa Baraka Takatifu.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.