Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa Francisko anawaalika waamini kufunga kwa kuwasaidia wengine!

Papa anawaalika waamini kufunga kwa dhati wakikimbuka wahitaji katika kipindi cha kwaresima

16/02/2018 16:41

Katika Misa ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Februari katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, amesisitiza juu ya kutazama hatari za udanganyifu wa kufunga hasa kudharau wengine, kwa maana kufunga  kwa dhati maana yake ni kuwasaidia wengine.

Kufunga ni jambo zuri lakini sio la kufanya wengine waone unachokifanya na kuwadharau na kwasababu wengine au kupinga kwa mujibu wa somo la siku kutoka kwa Nabii Isaya, ambaye anatafuta kuweka bayana juu ya nini maana ya kufunga akisema kufunga maana yake ni  kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kuvunje kila aina ya nira. (Is 58,1-9a).

Kufunga ni moja ya zoezi la kwaresima anathibitisha Baba Mtakatifu hata kama huwezi kufunga kabisa hadi kusikia njaa katika mfupa, unaweza kufunga kwa unyenyekevu na ukweli. Nabii Isaya anaweka mambo bayana fasdhila za kuweka katika matendo. Tabia ya kutazama mifukoni  na shughuli nyingine zipo lakini, kufunga maana yake ni kujivua wazi. Wapo maskini wengi ambao wanafunga na hawana chakula, wakati huo wewe unawadharau.Baba Mtakatifu anaongeza, fanya kitubio kwa amani. Pia huwezi kuongea wakati mwingine na Mungu na wakati mwingine na shetani.
 
Anaonya kutokana na neno la Mungu: msifunge kama mnavyofanya leo hii, mimi ni mkatoliki au mimi ni wa chama  hiki, la muhimu ni kifunga kwa dhati. Kufunga kwa tabasamu ili kutofanya wengine watambue unafanya nini kwa maana tendo kufunga jambo la unyenyekevu, kutafakari dhambi binafsi na kuomba msamaha wa dhambi kwa Bwana.

Ametoa mfano mmoja akifikiri watu ambao wanaangauka kufanya kazi ili waweze kupata mkate wa kupeleka nymbani kwa unyenyekevu na kudharauliwa. Anasema pia hatasahau kawe siku moja alikwenda kwa rafiki yake mmoja na kushuhudia mama mmoja  anampiga kofi mtoto wake, ni jinis gani unaweza kusaba makofu mtoto namna hiyo?

Baba Mtakatifu amewaomba warudipo nyumbani wafikirie jambo hilo la kufikiri jinsi gani wansishi na familia zao, wafanyakazi wao, haki ya mshahara wao, wanapewa likizo . Katika nyumba ,katika hali zote je mwendendo wangu ni upi?

Kama somo la kwanza linavyoeleza, kufunga maana yake ni kushirikiana mkate kwa wale ambao hawana,wale wasio kuwa na nyumba, kuwavalia walio uchi , bila hata kuwaacha ndugu.Leo hii wanajadiliana sana je tunawapatia nyumba wanaokuja kuomba au hapana.


Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

16/02/2018 16:41