2018-02-16 17:05:00

Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Maronite Roma!


Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na Jumuiya ya Tassisi ya Kipapa ya Wamaronite wakiwa katika maadhimisho ya Miaka 10 tangu kukubaliwa Taasisi hiyo. Baba Mtakatifu anasema ni fursa na zaidi ya kukutana ili kuweza kufanya kumbukumbu ya historia na kujikita ndani ya mizizi yake.  Kwa hakika, kipindi cha masomo yao Roma ni kipindi cha kuimarisha mizizi hiyo.

Anakumbuka mizizi iliyopo kwa jina lenyewe la Kanisa linalowaalika kutazama Mtakatifu  Marone, ambaye siku chache wamefanya kumbukumbu. Yeye kama mmonaki na mtindo wa maisha hakuridhika tu na imani za kisasa, bali alikuwa na utambuzi wa ulazima wa kwenda zidi  yaana wa kupenda kwa moyo wote.

Maisha yake ya kimaskin yalikuwa mbele ya macho ya dunia, lakini yenye thamani kwa Mungu na kwa wengine. Kwa kuchota katika kisima hicho alitafuta mwelekeo na kufuata kile anachokipenda; maana pale palipo  hazina yako, ndipo pia utakapokuwa na moyo wako (Mt 6,21) anasema Yesu.
 
Kufuatana na hayo wanachuo hao  kwa miaka hiyo katika msaada wa mafunzo ya tasauti ya kiroho na kutoka katika uzoefu wa jumuiya zao, wamepokea neema ambayo inawasidia kuishi vema mioyoni mwao kwasababu wanapata zaidi ile shauku ya mababa wakubwa na mama katika imani.

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa lakini kuna hatari leo hii ambayo inatokana na kuingilia utamaduni wa mpito na ule wa kutaka  kuonekana. Katika miaka hii ambayo wao wako masomoni ni fursa ya kuweza kwenda kinyume na mantiki za malimwengu na maisha yasiyofaa.

Ni miaka ya mazoezi katika uwanja wa Roma mahali ambapo Mungu anawasindikiza katika safari yao ili waweze kuimarika na kuwa na msingi wa kuwajibika kiroho hasa katika misingi miwili ya sala na kazi ya ndani. Sala za liturujia na binafsi ambazo hazitazami tu mazoea, lakini yanayojikita katika maisha mbele ya Bwana na Bwana ndani ya maisha. 

Kazi ya kiroho inahitaji sabir ina ufunguzi wazi wa moyo kwa kusaidiwa na masomo na kazi ya kung’amia vmea ili kuweza kuondoa viina macho na uongo ili kupta kuishi katika utumea ulio mkubwa wa uhuru bila ndumila kuwili na bila msimamo.

Aidha ameshirikishana nao juu ya utume wao wenye thamani kubwa Kwababu hasa ile amani kwa maana anasema kuwa, leo hii udungu na kushirikisha ni mambo yanayowakilisha changmoto ya dharura, ambayo hawezekani kusubiri, kwasababu nchini Lebanon wanalo jambo muhimu kwa namna ya pekee wito wa amani ya kutiza na katika ulimwengu. Baba Mtakatifu anasema katika nchi yao, wao wanaalikwa kutoa huduma kwa ndugu wote bila ubaguzi. Taaluma yao isaidie watu wa Lebanoni ili kujibu miito kwa watu wa kanda nzima na kuwa na ishara ya amani ambayo inatoka kwa Mungu (Yohane PAULO II, Esort. ap. postsin. Tumaini jipya kwa ajili ya Lebanoni, 125).

Pili Baba Mtakatifu ameshirikiana nao juu ya  kutazama vijana . Kama Kanisa linataka vijana wawe katika moyo wao, kwa ajili ya kuwasindikiza kwa matumaini na saburi kujitolea muda wao na kuwasikiliza. Vajana ndiyo ahadi ya wakati endelevu  hasa ambao ndiyo wa kuwekeza katika utume wao. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alipokutana nao alisema “Vijana wa Lebanon ni wakarimu na wazi kama Kristo anavyo waomba na kama baba wa nchii yao anavyo wafundisha (Mkutano na Vijana, 15 Septemba 2012)!

Kwa njia hiyo utume wao Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza ni kuwasadia ili kufungua mioyo kwa ajili ya wema ili nao waweze kufanya uzoefu wa furaha na kupokea Bwana katika maisha yao. Amewashukuru na kuwabariki!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.