Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa:Kipindi cha Kwaresima wamaamini lazima kusimama,kutazama na kurudi!

Simama kidogo juu ya tabia ya kukurupuka, ya kutaka kukagua kila kitu, kujua kila kitu, kutawala kila kitu,kuchunguza kila kitu mahali ambapo unaishia kuwa mtupu

15/02/2018 15:55

Kipindi cha Kwaresima ni kupindi mwafaka kwa ajili ya kusahihisha maisha yetu kikristo na kupokea kwa upya daima furaha na matumaini ya habari njema ya Pasaka ya Bwana. Kanisa kwa hekima ya umama, inapendekeza kuwa makini kwa kila chochote kile litetacho baridi na kuondoa hewa nzuri katika mioyo ya waamini. Ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo  wakati wa kuadhimisha misa ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa  la Mtakatifu Anselmi mjini Roma tarehe 14 Februari 2018, ikiwa mama Kanisa anaanza kipindi cha kwaresima.

Vishawishi ambayo vinajitokeza ni vingi mno, Baba Mtakatifu anaendelea; Kila mmoja anatambua matatizo ambayo anapaswa kukabiliana nayo. Ni huzuni kabisa kuona kwamba mbele ya majaribu ya kila siku, zipo sauti zinasikika hasa  za kudumbukia katika kisima cha ukosefu wa uhakika, wakati huo huo hawatambui hata kuona mbegu ya matumaini kwasababu wanakata tamaa. Iwapo tunda la imani ni upendo kama alivyokuwa anapendelea mama Teresa wa Kalkuta, basi tunda la kukata tamaa ni ukosefu wa uvumilivu na ubaridi. Kukata tamaa, ubaridi, na kutovumilia ni matunda ya shetani anayefanya mioyo ya waamini igandamane!

Kwaresima ni kipindi cha thamani ili kutoa viini macho vya mambo hayo na vishawishi vingine ili kuacha mioyo yetu irudi kudunda kwa mujibu wa mapigo ya moyo wa Yesu. Katika liturujia yote, inajikita katika fikira hizi na ambayo tunaweza kuifafanua katika maneno matatu ili kuweza kuwasha mioyo ya waamini  Baba Mtakatifu anasema. Maneno hayo ni simama, tazama na urudi!

Akianza kufafanua juu ya maneno hayo matatu amesema, Tazama, kidogo na hacha mambo ya kuangaika hapa na pale, ukikimbia bila kuwa na maana kwa kujaza  moyo uchungu na kuhisi hufiki sehemu yoyote kwamwe. Tazama na uache ulazima huo wa kuishi kwa  kukimbizana ambapo unapotea, unatengenisha na kuishi  kwa kupoteza muda kwa ajili ya familia, muda wa urafiki, muda kwa ajili ya watoto, muda kwa ajili ya babu na bibi, muda kwa ajili ya kutoa shukrani na mwisho muda wa Mungu!

Simama kidogo mbele ya mahitaji ya kutaka uonekane na kila mtu, wa kutaka kukaa kila wakati vioo ambayo vinakufanya usahau thamani ya kukaa kiundani na kusikiliza. Simama kidogo tabia ya kujitazama kuwa hu hali ya juu, mazungumzo ya kijuuu na madharau ambayo yanafanya usahau kuwa na ukarimu huruma na kuheshimu, kwa ajili ya kukutana na wengina hasa wale ambao wameathirika, wenye majeraha, hata ambao wamekumbwa na dhambi na makosa.

Simama kidogo tabia ya kukurupuka, ya kutaka kukagua kila kitu, kujua kila kitu, kutawala kila kitu,kuchunguza kila kitu, tabia inayotokana na kusahau kuwa na shukurani kwa ajili ya zawadi ya maisha na kwa ajili ya mema mengi uliyopokea. Simama kidogo tabia ya kupiga kelele zinazosababisha  hata kuziba maskio yetu na kufanya usahau nguvu yenye kuleta matunda na kuunda ukimya ndani mwako. Simama kidogo tabia za kuchocheza hisia tasa ambazo hazileti matunufaa, zitokanazo na kujifungia binafsi,kujitosheleza na kufanya usahau kwenda kukutana na wengine kwa ajili ya kushirikishana mizigo mizito na mateso. Simama na hacha tabia za utupu, ya mambo ya wakati yanayoisha, mambo yasiyo na kiini wala mizizi ya maisha,simama katika thamani katika mchakato wa hatua au kutambua daima safari. Simama  ili uweze kutazama na kutafakari!

Kuhusu neno la pili tazama, Baba Mtakatifu anasema, tazama ishara ambazo zinazuia na kuzima upendo, ambao unatunza moto hai wa imani na matumaini. Kuzim sura hai za ukarimu na wema wa Mungu anayetenda kwa njia yetu. Tazama sura za familia zetu ambazo pamoja na hayo yote yanayowatukia, bado wanaendelea kwa nguvu zote kwenda mbele katika maisha, na kati ya mambo mengi yanayokosa, lakini hawakosi kila siku kufanya nyumba zao ziwe shule ya upendo.

Tazama sura ambazo zinatualika, sura za watoto wetu na vijana walijaa wakati endelevu na matumaini, walijaa siku zijapo na uwezo mkubwa ambao unahitaji kuwajibika na kuwalinda. Ni vichupikiza hai vya upendo na maisha ambayo ndani yake yanazidi kuongezeka katika kuhesaba na ubinafsi.
Tazama sura za wazee wetu walioishi  wakisubiri muda wao upite: wao ni sura zinazobeba kumbukumbu hai ya watu wetu. Sura za matumaini katika matendo ya Mungu. Tazama sura za wagonjwa na watu wengi ambao wanawatunza; sura zao ambao wameathirika na katika huduma ambayo inawazunguka yenye thamani ya kila mtu ambayo haiwezi kamwe kuishia katika masuala ya kuhesabu au kutokufaa.

Tazama sura za walio tubu, wanajaribu kufanya malipizi ya makosa yao  , pamoja na udhaifu wao, lakini wanapambana ili kibadili hali na kwenda mbele. Tazama na kutafakari sura ya upendo wa msulibiwa ambao leo hii msalaba unaendelea kubebwa kwa matumaini. Mikono yake iko wazi akisubiri wote ambao wanahisi kusulibiwa; ambao wanafanya uzoefu katika maisha yao ya mizigo na kushindwa, wale ambao wamedanganya na kudanganyika.

Tazama na kutafakari sura halisi ya Kristo msulimbiwa, msulibiwa kwa ajili ya upendo bila ubaguzi wowote ni kwa wa ajili ya wote! Na kutazama sura yake ni mwaliko mkuu wa matumaini katika kipindi hiki cha kwaresima ili kuweza kushinda shetani wengi dhidi ya  matumaini, wa ubaridi na kutovumilia. Sura ambay inatualika kupaza sauti tukisema Ufalme wa Mungu unawezekana!

Simama, tazama na kurudi: kwa maana urudi katika nyumba ya Baba yako, Urudi bila kuogopa katika mikono inayotamaniwa kwa maana ni Mungu, mwingi wa huruma ambaye anakusubiri ( Ef 2,4)! Rudi bila hofu: Baba Mtakatifu anafafanua kuwa ni kipindi mwafaka cha kurudi katika nyumba ya Baba, na nyumba ya Baba yenu (Taz Yh 20,17). Hiki ni kipindi cha kuacha kuguswa moyo… Tendo la kubaki katika njia ya  ubaya ni kisima cha udanganyifu na huzuni! Maisha ya kweli ni jambo tofauti kabisa, hata mioyo yetu inatambua jambo hilo vema! Mungu hachoki na hatachoka  kamwe kusubiri kwa mikono yake (Taz Bolla Misericordiae Vultus, 19).

Rudi bila hofu  na kufanya uzoefu wa ukarimu wa uponyaji na kupatana na Mungu. Hacha Bwana aweze kukuponya majeraha ya dhambi na kutimiza unabii aliosema kwa baba zetu kwamba, Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama (Ez 36,26). Simama, tazama na rudi!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

15/02/2018 15:55