2018-02-15 15:40:00

Masikitiko ya Papa Francisko kwa tukio la vifo vya wanafunzi Parkland!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam zake za rambirambi kwa asikufu Thomas Gerard Wenski wa Jimbo Kuu la Miami Marekani kufuatia na janga la ufyatuaji wa risasi katika Shule moja ya   Marjory Stoneman Douglas huko Parkland. Ujumbe wake uliotiwa sahini na kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, baba Mtakatifu anawakikishia sala zake kiroho kwa Mungu ili marehemu wote wapumzike kwa amani na kuwaponya majeraha, utulivu kwa wote wanaumia kwa ajili ya wapendwa wao .Na akiwa na matumaini ya kuwa vitendo vya uhasama na vurugu za kikatili zinaweza kukomesha,  anawabariki kwa Baraka tele kutoka kwa Mungu zenye amani na kuwatia nguvu.

Kuhusiana na janga hilo hata Askofu Mkuu wa Miami Thomas Wenski nchini Marekani anashutumu vikali shambulio hilo lilitokea katika Sekondari ya Parkland, huko Florida tarehe 14 Februari 2018 saa 9 alasiri wakati wanafunzi wanatoka shuleni. Janga hilo limesababisha watu 17 kufariki na wengine wengi kujrehuiwa kwa mujibu wa taarifa kutoka jimbo hilo. 

Wanafunzi elfu 3 wanaosoma katika shule hiyo walipatwa wasiwasi na hofu kubwa. Kwani kijana aliyesababisha mauaji hayo ni  mwanafunzi aliye wahi kusomea katika shule hiyo kwa jina  Nikolas Cruz mwenye umri wa miaka 19 ambapo alichukua silaha na kuanza kuwashambulia watu mida ya saa 9 wakiwa wanatoa shuleni humo. 

Askofu Mkuu Menski hafichi kabisa huzuni yake kubwa mbele ya janga hili, wakati huo huo lakini anawaalika watu wote kusali mbele ya janga hili la kutisha kwa ajili ya marehemu, waliojeruhiwa, familia nyingi zilizopoteza wapendwa wao na hata watoa msaada. Hata hivyo askofu mkuu natambua hasira za raia walizo nazo wakati huu kwa ajili ya watoto wasio kuwa na hatia, lakini wanawomba waungane kwa pamoja kuwasaidia wengine katika kipindi hiki kigumu cha uchungu . na kwa msaada wa Mungu wanaweza kubaki kidete na kuvumilia mabaya yote ambayo yamesababishwa. Na mwisho Askofu anawaomba Mungu aweze kuponyesha mioyo iliyovunjika ili kuweza kukabiliana na mateso ya ndani ya roho. 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.