Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Ujumbe wa Papa kwa Kanisa la Brazil kuhusu Kampeni ya kindugu 2018!

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa Kanisa la Brazil katika maadhimisho ya Kampeni Kindugu 2018! - RV

14/02/2018 16:35

Ndugu kaka na dada wa Brazil, katika kipindi hiki cha kwaresima, ninaungana kwa furaha na kanisa la Brazil kuadhimisha Kampeni ya kindugu na kushinda nguvu za vurugu , kwa lengo la kujenga undugu na kuhamasha utamaduni wa amani, mapatano na haki, katika mwanga wa Mungu,ni kama safari kwa ajili ya kushinda kutumia nguvu.  Haya ni maneno ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francikso , kwa Kanisa la Brazil alio watumia, katika tukio hili la Kampeni ya mwaka juu ya udugu mwaka 2018. 

Baba Mtakatifu anaeleza kwamba, kwa namna hiyo Kampeni ya kindugu 2018, inawaalika kutambua nini maana ya vurugu wakiwa na  matumaini  ili kuweza kushinda, kwa njia ya upendo na kuwaonesha uso wa Yesu msulibiwa. Yesu alikufa na kutoa maisha timilifu (Yoh 10, 10). Katika kipimo cha ukuu wake  yeye yupo kati yetu, na maisha yanabadilika na kuwa uwanja wa kindugu, wa haki, wa amani na hadhi kwa kila mtu (Taz Injili ya Furaha 180. Katika kipindi hiki cha toba, mahali ambapo wote tuaalikwa kuishi kwa matendo ya dhati hasa kufunga, sala na upendo, inatufanya tutambue jinsi gani wote tulivyo ndugu. Kutokana na hilo, anawaalika kuacha upendo wa Mungu uonekane kati yao, kati ya familia na jumuiya nzima.

Hiki ni kipindi mwafaka na cha wokovu , ambacho kinatuplekakuwa na neema ya msamaha tulio upokea kutokana na  kutolewa sadaka. Msamaha wa dhambi zetu, kielelezo kwetu sisi cha upendo mkuu na huruma kwa wakristo wote na kipindi ambacho hatuwezi kukipoteza.  Baba Mtakatifu anasema, jinsi gani wakati mwingine inakuwa vigumu kusamehe, lakini wakati huo msamaha ni chombo cha kuweka mambo yetu madhaifu katika mikono yake, ili kuweza kupata utulivu wa kiroho na amani.

Anawaalika kuwacha visa na vikwazo, kwani kuacha hasira na kulipiza visasi ni hali ambayo inasaidia kuishi kama ndugu na kushinda vurugu. Wapokee wito huo na ushauri kutoka katika maneno ya Mtume Paulo kwa Waefeso asemaye “ jua lisizame ukiwa na hasira. (Ef 4, 26). Wao wako mstari wa mbele wa kushinda vurugu ili kuweza kuwa wajumbe na wajenzi wa amani. Amani ni tunda la maendeleo ya watu wote, amani inazaa uhusiano mwema kwa kila kiumbe. Amani ni lazima itande kila siku kwa saburi na uhuru katika umbu la familia na kwa namna hiyo katika jumuiya nzima, katika mahusiano ya kazini na katika kila kiumbe!

Anawashauri wafuate ishara ndogo na kuheshimu, kusikiliza , kuzungumza, kujadiliana , kukaa kimya, kuwa na upendo, ushikirikiano, ushirikishwaji katika ishara ya kindugu kwa mwaka huu. Katika Kristo wote ni familia moja, kwa maana wote tulizaliwa katika damu msalabani ambayo ni wokovu wetu. Jumuiya ya Kanisa nchini Brazil inatangaza na kila siku wokovu kwa ajili ya kuishi kindugu bila vurugu au kutumia  nguvu.

Anamalizia ujumbe wake akiwaombea kwa Mungu ili Kampeni ya kidungu mwaka huu iweze kuwatia moyo na kuanza safari ya kushinda vurugu na nguvu  ili  kushi daima kama ndugu kaka na dada katika Kristo!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

14/02/2018 16:35