2018-02-14 16:05:00

Katekesi ya Papa:Maana ya Nasadiki na Maombi ya waumini kwa ajili ya dunia!


Baba Mtakatifu Francisko, kabla ya kwenda katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Katekesi yake, amewasalima kwanza wagonjwa waliokuwa katika Ukumbi wa Mwenye heri Paulo wa VI na kuwashukuru uwepo wao. Amewabariki wote na kuwaleza kuwa anakwenda katika uwanja kwa ajili ya katekesi lakini mabap na wao watashiriki kusikiliza na kuonekana, maana ni jambo zuri. Mara baada ya maneno hayo wamesali salam Maria pamoja na mwisho amewabariki.

Katika mwendelezo wa Katekesi juu ya Misa Takatifu hasa katika kipengele za Liturujia ya Neno, Baba Mtakatatifu Francisko ameendelea kuelezea maana ya nasadiki na maombi ya sala kwa aumini kwa ajili ya ulimwengu. Lakini kabla ya tafakari hiyo, limesomwa Neno  la Mungu kutoka Injili ya Yohane( 15,7-8) mahali ambapo mwinjili anasema, “mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi ombeni chochote mnachotaka nanyi mtapewa kwa maana Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu”. Akianza Katekesi amesema “siku njema hata kama siku ni mbaya kidogo, lakini iwapo roho ina furaha daima ni siku njema, na hivyo siku njema ya”. 

Katekesi ya leo imegawanyika katika makundi mawili kwa maana kikundi kidogo cha wagonjwa wanasikiliza na kuona wakiwa katika ukumbi.
Kwa kuendelea na Katekesi juu ya misa ya Misa, kusikiliza masomo ya Biblia ambayo pia hufanyika mahubiri je  inaelezea nini?, anatoa jibu ya kuwa, inajibu haki: haki ya kiroho ya watu wa Mungu wanapokea kwa wingi tunu la Neno  la Mungu ( Utangulizi wa misale, 45).

Kila mmoja wetu anapokweda katika misa anayo haki  ya kupokea kwa wingi Neno la Mungu ambalo limesomwa vizuri, pia kuelezwa vizuri. Hiyo ni haki! Iwapo Neno la Mungu halisomwi vizuri au kuhubiriwa kwa shauku na shemasi, padri au askofu, ni kuwakosesha haki waamini. Kwa maana sisi wote tunayo haki ya kusikiliza neno la Mungu anathibitisha Baba Mtakatifu!.

Bwana anazungumza na wote, wachungaji na waamini. Yeye anabisha mlango wa moyo kwa wale wanaoshiriki misa, kwa kila hali ya maisha umri au hali. Bwana anatuliza, anaita  na kutoa vichipukiza vipya vya maisha na mapatano. Hiyo ni kwa njia ya Neno lake, na kwa neno hilo linabisha hodi katika moyo na kubadili mioyo!

Kwa maana hiyo mara baada ya mahubiri, upo muda wa kukaa kimya ili neno hili lipate mkao kutokana na mbegu iliyotolewa, na kwa kufanya hivyo ili mang’amuzi ya kufuata yaweze kuonekana kwa njia roho anayomjalia kila mmoja. Ukimya baada ya mahubiri ni msingi na lazima kwa kila mmoja , kufikiri kile ambacho umesikiliza!

Baada ya ukimya, misa iendeleaje: akijibu, Baba Mtakatifu anasema, mtu anayejikita katoa jibu la imani, anaingia moja kwa moja na  kuungama imani ya Kanisa, kwa maelezo ya Nasadiki. Wote kwa pamoja husali sala ya Nasadiki katika Ibada ya Misa. Kusali kwa pamoja ni ishara ya kuonesha umoja na jibu ambapo kwa pamoja limetokana na usikivu wa Neno la Mungu kama isemavyo katekesimu ya Kanisa katoliki (n.185-197).

Kuna muungano hai kati ya kusikiliza na imani. Imani haizaliwi kwa njia ya tamthiliya za akili za binadamu, bali kama anavyokumbusha Mtakatifu Paulo,  inakuja kwa njia ya kusikiliza neno la Kristo (Rm 10,17). Imani inaimalisha  usikivu na kukupeleka katika Sakramenti. Katika  kusali sala ya Nasadiki, waamini katika liturujia wanarudi kutafakari na kukiri  matendo makuu ya imani ambayo yanakuja kabla ya maadhimishio ya Ekaristi (Misale 67).
Ishara ya Nasadiki katika Ekaristi ya ubatizo tunayopokea katika jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, inatukumbusha kuwa Sakramenti ni msingi katika mwanga wa imani ya Kanisa.

Jibu la Neno la Mungu ambalo upokelewa kwa imani baadaye ni kujieleza katika sala ya pamoja ambayo inawakilisha sala ya ulimwengu mzima kwasababu inakumbatia mahitaji ya Kanisa na dunia nzima na ndiyo sala ya waamini! Mababa wa Mtakaguso walirudisha maombi hayo mara baada ya Injili na mahubiri kwa namna ya pekee katika siku ya Jumapili na katika sikukuu ili kwa ushiriki wa waamini , waweze kusali kwa ajili ya Kanisa , kwa ajili ya watawala , kwa ajili ya wale wenye kuhitaji, kwa ajili ya wote na  kwaajili ya wokovu wa dunia nzima. (Cost. Sacrosanctum Concilium, 53; Taz 1 Tm 2,1-2).  Kwa njia hiyo chini ya Padri ambaye anatoa utangulizi na kumalizia waamini wanasali wote kwa  ubatizo, wanamtolea Mungu sala zao kwa ajili ya wokovu wa wote. Na baadaye shemasi, au msomajo wa sala , waamini wote wanaungana wakijibu “twaomba usikilize”.

Kumbuka yale ambayo Bwana Yesu amesema, mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi ombeni chochote mnachotaka nanyi mtapewa” (Yh 15,7).  Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa, sisi hatuamni hili kwasababu imani yetu ni haba. Lakini kama tungekuwa na imani  kama asema Yesu kama mbegu ya aladali tungepokea kila kitu. Ombeni mtakacho nayi mtapewa”. Na ndiyo maana kipindi hicho cha sala ya ulimwengu mzima baada ya Nasadiki ni muda wa kuomba Bwana mambo nakuu katika Misa, mambo ambayo sisi tunahitaji  na tunataka, kwa maana tutapewa kwa namna moja au nyingine lakini tutapewa”.

Kila kitu cha wezekana kwa yule anaye amini Bwana alisema. Je mtu yule alijibu nini  mata baada ya bwana kumwambia maneno hayo? Alijibu “Ninaamini Bwana, lakini ningezee inamani yangu ni ndogo”. Hata sisi tunaweza kusema “ Bwana ninasadiki, lakini niongezee imani kwakuwa ya kwangu ni haba.
Na sala hiyo lazima kuifanya kwa roho ya imani. Bwana ninaamini, na niongezee imani. Mantiki za ulimwengu huu haziwezi kutoa katika mbingu, bali ni kubaki bila kusikilizwa , kama asemavyo Mtakatifu Yakobo  4,2-3,  “Mnatamani vitu kwa vile hamvipati mko tayari kuua;mwatamani kupaa vitu lakini hamvipati hivyo mnagombana na kupigana. Hampati kile mnachokiomba kwasababu hamkiombi kwa Mungu. Tena mnapoomba hampati kwasababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu”.

Baba Mtakatifu anamalizia na ufafanuzi kuwa, nia ya maombi ambayo anawalika waamini wote kusali, lazima iendane na sauti ya mahitaji ya kweli na dhati katika jumuiya ya Kanisa na ulimwngu mzima, kuepuka maombi ya alaiki na ambayo si ya kina. Maombi kwa ajili ya dunia nzima ambayo ni hitimisho la Litulurujia ya Neno , yanatualika kuwa na mtazamo wa Mungu ambaye anatutunza sisi wote kama watoto wake!

Sr Angela Rwezaula

Vativcan News !

 








All the contents on this site are copyrighted ©.