Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Sala ya Malaika wa Bwana

Yesu ni tabibu wa kweli na tuombe kwa maneno ya mkoma ukitaka nitakase!

Baba Mtakatifu anawaalika waamini kujitafiti mioyoni mwao ukoma binafsi wa dhambi - REUTERS

12/02/2018 15:48

Katika Domenika hizi, Injili kwa mujibu wa maelezo ya Mtakatifu Marko, anaonesha Yesu anayetibu wagonjwa wa kila aina. Kwa mantiki hiyo inakwenda sambamba na Siku ya Wagonjwa Duniani ikiwa leo hii ni kilele chake, mahalia ambapo kila tarehe 11 Februari ni siku ya kumbukumbu ya Bikira Mwenyeheri Maria wa Lourdes. Kwa mtazamo huo, mioyo yetu ielekee katika groto ya Masssabielle na kutafakari Yesu kama tabibu wa kweli anayetibu binadamu, ambaye amedumbukia katika  dhambi na matokeo yake!

Hayo ni maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko, katika mahubiri yake, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini wote waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, kusali naye, wakati Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya Bikira Maria wa Lourdes. Ni siku ya wagojwa duniani ambapo Mama Kanisa anachukua nafasi ya kuwakumbuka watu wote wanaoteseka kiroho na kimwili.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri yake anasema, Sura ya Injili kutoka Marko ( Mc 1,40-45) inaelezea juu ya uponyaji wa mtu mgojwa wa ukoma, ugonjwa ambao katika Kitabu cha Agano la kale ulikuwa unasadikika kuwa ni dhambi kubwa ambayo ilipelekea kutengwa katika jumuiya ya wanye ukoma tu, kwasababu ya kasumba ya wakati ule kwamba wao wajihisi kuwa ni wadhambi,  si mbele ya Mungu tu, bali hata kwa watu. Na ndiyo  maana mgonjwa wa ukoma katika Injili anamwomba  Yesu kwa maneno  “ukitaka unaweza kunitakasa”.

Kusikia maneno hayo Yesu akamwonea huruma. Ni muhimu sana kujikita kwa umakini zaidi maneno ya Yesu, hasa kama tulivyo fanya katika kipindi chote cha Jubilei ya Huruma, anasema Baba Mtakatifu. Na si rahisi kutambua kazi ya Kristo iwapo hujuhi Kristo mwenyewe; iwapo haingii ndani ya Moyo kwa upendo na huruma. Na ndiyo msukumo wake wa kunyosha mikono yake juu ya mtu huyo mwenye ukoma na kumgusa akisema “Nataka Takasika!”
Tendo la kustaajabisha ni lile ambalo Yeu anamgusa mkoma, kwasababu sheria  ya Musa ilikuwa inakataza kabisa.... Kugusa mkoma ilikuwa inasadikika kuwa  ni kuambukizwa hata ndani ya mwili na katika roho, kwa maana hiyo kuwa najisi. Baba Mtakatifu anafafanua kuwa katika kesi hiyo sasa haitazami mkoma kumwambukiza Yesu, bali huruma kutoka kwa Yesu, mkoma anaponywa na kutakasika!

Katika uponywaji huo, sisi tunashangaa haza zaidi ya upendo, ambao ni huruma, kustaajabu ni kwamba Yesu hajali kabisa kuambukizwa, au sheria ziliokuwapo, bali ni kuongozwa na utashi wa kutoa huru wa mtu huyo na balaa ambao lilikuwa limemzingira.
Baba Mtakatifu anaongeza kusema,hakuna ugonjwa unaosababishwa na uchafu, kwa maana  ugonjwa kwa hakika ni sehemu ya maisha maana  unakumba mtu lakini hauwezi kumkataza asiwe na uhusiano na Mungu. Badala yake mtu aliye mgonjwa anaweza kuwa zaidi na muungano na Mungu. Dhambi inayomfanya mtu awe mchafu ni ile ya ubinafsi, ukiburi, kuingia kwa rushwa katika dunia! haya ndiyo magonjwa ambayo moyo unahitaji kutakasikana  kurudia maneno kama ya mkoma " kama wataka nitakase!

Baba Mtakatifu kwa njia hiyo aliwataka waamini wote kuinamisha vichwa vyao na kukaa  kimya kidogo wakifikiri ndani ya moyo, ili kutazama mioyoni mwao ni wapi  uchafu wa dhambi binafsi upo. Na katika kimya kila mmoja aweze kurudia maneno ya yule mkoma, "kama wataka nitakase!

Kila mara, tukipokea sakramenti ya kitubio kwa moyo wa dhati, Bwana anarudia maneno hayo akisema, "ninataka takasika". Ni furaha gani hiyo! Baba Mtakatifu anaongeza!  Na ukoma wa dhambi unapotea na kubadilika  ili  kuishi kwa furaha na katika uhusiano na Mungu na kujumuika ndani ya jumuiya kikamilifu. Amemalizia mahuburi yake akisema, kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria Mama wa asiyekuwa na dhambi, tuombe Bwana aliyewaponyesha wagonjwa, ili atuponyeshe hata sisi majeraha ya ndani kwa njia ya huruma na kutupatia matumaini  na amani ya moyo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

12/02/2018 15:48