Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Tuombe Bwana fadhila ya kuwa na saburi hasa katika safari ya majaribu!

Papa Francisko anasema tuombee Bwana neema ya kuwa na saburi wakati wa kubeba mabegani mwetu matatizo

12/02/2018 15:05

Tuombe Bwana fadhila ya saburi hasa kwa yeyote aliyeko katika safari akibeba mabegani mwake matatizo na majaribu, kama walivyo ndugu wakristo wanaoteswa karika nchi za Mashariki. Ndiyo nia kuu ya maombi ya Baba Mtakatifu Francisko, iliyosikika katika Misa Takatifu, asubuhi tarehe 12 Februari 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Imani yenu ikijaribiwa inatoa saburi. Ni maneno anayo andika Mtakatifu Yakobo mtume katika somo la kwanza la siku, ambayo Baba Mtakatifu amefafanua zaidi akisema, saburi  haina maana ya kujiachia au kushindwa, je nini maana ya kuwa na saburi katika maisha na mbele ya majaribu?

Sio rahisi kutambua hilo kwa haraka, hasa namna ya kuchanganua kati ya saburi ya kikristo ya kujikabidhi au kushindwa, kwa kuonesha zaidi fadhila ambayo ni safari na si kwa yule anayesimama na kujifungia binafsi.  Unaposafiri, hujitokeza mambo mengi ambayo wakati mwingine siyo mazuri anabainisha baba Mtakatifu. Mara nyingi kuhusiana na suala la saburi ni kama fadhila katika safari, na huo ni mtindo hasa wa wazazi walio wengi wanapokuwa na mtoto walemavu au mgonjwa, saburi hujitokeza! Japokuwa saburi hiyo ni kwa njia ya neema ya Mungu anayeishi. Na kwa neema ya sabauri hiyo wanaotunza mtoto huyo kilema humtunza kwa upendo hadi mwisho japokuwa siyo rahisi   kuchukua mzigo wa ulemavu na ugonjwa kwa miaka mingi Baba Mtakatifu anasisitiza…

Lakini furaha ya kuwa na mtoto inawapa nguvu wa kuendelea mbele na ndiyo uvumilivu na siyo tu kujiachia, yaani ni fadhila inayokuja wakati uko safarini, kwa maana saburi ya kikristo si kwenda katika njia ya kushindwa!
Saburi hukataa na  kudharau vizingiti binafsi; Baba Mtakatifu akifafanua tena maana ya neno saburi  anasema, hiyo ni kutambua kuchukua majaribu binanfsi; ina maana ya uwajibika kwasababu saburi inakufanya utambue kwa kina, si kuacha mateso, bali kuyachukua yakawa furaha ya kweli na furaha timilifu kama asemavyo mtume Yakobo.

Saburi maana yake ni kubeba mabegani matatizo,si kukabidhi mtu mwingine achukue matatizo hayo: unayachukua binafsi kwa maana hayo ni matatizo yako. Ndiyo yananifanya niteseka kwa hakika, lakini ninayabeba! Pamoja na hayo saburi ni hekima ya kutambua kuzungumza na vizingiti. Kuna vizingiti vingi katika maisha lakini zaburi haitaki vizingiti hivyo, lakini inavidharau kwasababu inatambua kuzungumza na vizingiti hivyo! Kuna utundu wa hali ya juu au uvivu hatujuhi, lakini saburi haitambui lolote juu yake anasisitiza Baba Mtakatifu! 

Saburi ya Mungu inasindikiza na kusubiri: Lakini saburi inayozungumzwa na Mtakatifu Yakobo, siyo ushauri kwa ajili ya wakristo, Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, iwapo tukitazama historia ya wokovu, tunaweza kuona saburi ya Mungu Baba yetu, ambayo alikuwa nayo  na kupeleka watu wake wenye vichwa vigumu kila mara walipogeuka na kutengeneza miungu, au kwenda katika njia zao. Saburi hiyo ni kama ya Mungu Baba aliyo nayo kwa kila mmoja wetu , akitusindikiza na kusubiri wakati wetu. Mungu ambaye alimtuma Mwanae wa pekee ili aingie kwa saburi, achukue utume wake na kuteseka hadi kufikia mauti.

Baba Mtakatifu anasema kwa njia hiyo mawazo yanawaendea watu waoteseka kwamba, unaweza kufikiria ndugu wanaoendelea kuteswa wa nchi za Mashariki , waliofukuzwa kutokana  kwamba ni wakristo. Lakini wao wanatambua kuwa ni wakristo wa mahali pale  na wameingia taratibu kwa saburi kama Bwana alivyoingia kwa saburi. Katika mawazo hayo anasisitiza, tunaweza leo hii kusali kwa ajili ya watu wetu: Mungu awape  watu wake saburi ili waweze kuchukua majaribu. Na hata kusali kwa ajili yetu. Kwa maana mara nyingi tukikosa saburi, hasa wakati kitu kidogo kikokosa ni kupiga kele, lakini wakati huo simama na kufikiria saburi ya Mungu Baba, na ingia kwa saburi kama Yesu . Hiyo ndiyo fadhila nzuri ya saburi ambayo tumwombe Bwana.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

12/02/2018 15:05