Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Sala ya Malaika wa Bwana

Kuzindua kujiandikisha kwa njia ya Intaneti katika Siku ya Vijana duniani!

Tazama na mimi ninajiandikisha kwa njia ya Intaneti kuudhuria Siku ya Vijana duniani huko Panama 2019 - REUTERS

12/02/2018 16:07

Leo hii unazinduliwa mchakato wa kujiandikisha kwa Siku ya Vijana Duniani ambayo inatafanyika Panama mwezi Januari 2019. Hata mimi kwa uwepo wa vijana wawili, ninajiandikisha kwa njia ya Interneti,(Tablet). Tazama nimejiandikia sasa kama mhujaji wa Siku ya Vijana Duniani. Tunapaswa kujiandaa! Ninawaalika vijana wote duniani kuishi kwa imani na shauku ya tukio la neema na kindugu iwe katika kuelekea Panama au kuudhuria siku hiyo katika jumuiya mahalia.

Haya ni maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya kumaliza sala ya Malaika wa Bwana, katika viwanja vya Mtakatifu Petro akiwaalika vijana kuanza kujiandikisha kwa njia ya mtandao ya kijamii wote ambao wanatarajia  kudhuria siku ya Vijana duniani huko Panama 2019.
Baba Mtakatifu akiendelea amesema kuwa tarehe 15 Februari nchi za  Mashariki na katika nchi nyingine duniani, mamilioni ya watu wanataadhimisha Mwaka mpya. Kwa njia hiyo anawatumia salam nyingi  za matashi mema familia ili wapate  kuishi daima katika mshikamano, undugu na shauku ya wema kwa kutoa mchango wa kuunda jamii ambayo kila mtu anakaribishwa, analindwa , anahamasisha na kushirikishwa. Aidha amewaomba wasali kwa ajili ya zawadi ya amani, tunu msingi ya kufuata kwa upendo, bila kukwepa  na kwa ujasiri. Kwa wote anawasindikiza na kuwabariki

Amewasalimiwa mahujaji wote familia, parokia , vyama na wote waliofikia kutoka Italia na duniani kote kwa namna ya pekee wahujaji kutoka Murcia (Uispania), na watoto kutoka Guimarães (Ureno) .Pia amewasalimia jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma wakiwa katika sala ya kuombea amani ya nchi yao ya Jamhuri ya Kidemokrasai ya Congo; kwa namna ya pekee amewakumbusha nia ya Siku ya Sala na kufunga kwa ajili hiyo tarehe 23 Februari!

Halikadhalika mawazo yake yamewaendea wagonjwa wote mahali popote duniani, kwamba zaidi ya ugonjwa kimwili bado wapo wengi wanoteseka na upweke na kutupwa pembezoni mwa jamii. Mama Maria msaada wa wagonjwa asadie kila mmoja kupata nguvu ya kimwili na kutoa neema kwa njia  ya kupata matibabu na upendo wa kindugu na mshikamano wa dhati.


Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

12/02/2018 16:07