Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Hotuba ya Papa Francisko kwa wajumbe wa Sinodi ya Kigiriki-Melkiti!

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Sinodi ya Kigiriki-Melkiti mjini Vatican

12/02/2018 15:23

Ninawashukuru kufika kwenu. Furaha ya tukio hili inajikita katika maadhimisho ya umma ya umoja wa Kanisa ambayo itafanyika kesho asubuhi wakati wa maadhimisho ya Ekaristi, ambapo nilipata kuafikiana na Kiongozi wenu katika barua ya tarehe 22 Juni mwaka jana, mara baada ya uchaguzi wa Patriaki Pater et Caput kwa upande wa Sinodi ya maaskofu. Ni maneno hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko wakati akihutubia kwa wajumbe wa Sinodi ya Wagiriki- Wamelkiti aliokutana nao tarehe 12 Februari 2018 mjini Vatican.

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake amesema, leo hii kama daima anapenda kuwaakikishia uwepo wake karibu kwa sala, ili Bwana Mfufuka aweze kuwa karibu na kumsindikiza kiongozi mpya  katika utume aliomkabidhi. Ni sala ambayo haiwezi kwenda tofauti na ile ya kuombea nchi ya Siria na kwa nchi zote za Mashariki, kanda ambazo Kanisa lao kwa namna ya pekee imechimba mizizi ndani yake na kutoa huduma nyeti kwa ajili ya watu wa Mungu!

Uwepo wake na wao wote ambao hawatazami tu nchi za mashariki bali uwepo wao  kwa miaka mingi katika nchi ambayo waamini wa kigiriki - Melkiti walihamia wakitafuta maisha bora, kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema  hata waamini wa diaspora na wachungaji wake wote anawaombea. Katika kipindi hiki kigumu cha kihistoria  jumuiya nyingi za kikristo huko Mashariki zinaalikwa kuishi kwa imani katika Bwana Yesu katikati ya majaribu mengi. Baba Mtakatifu anawatakia  wao, wawe na ushuhuda wa maisha hasa Maaskofu, mapadre wa kigiriki-Melkini ili waweze kuwatia moyo waamini wabaki katika nchi mahali ambapo neema ya Mungu ilizaliwa.

Akikumbuka barua aliyoandika mwezi Juni mwaka jana anasema, hakuna kipindi kama hiki ambacho wachungaji wanaalikwa zaidi kuonesha mbele ya watu wa Mungu wanaoteseka umoja, muungano na ukaribu, mshikamano , uwazi na ushuhuda. Kwa njia hiyo anazidi  anawaalika kindugu kuendelea katika njia hiyo. Na amewakumbusha kama wajuavyo tarehe 23 mwezi huu ni siku ya sala na kufunga kwa ajili ya amani. Katika fursa hiyo anasema, hatasahau kukumbuka kwa namna ya pekee nchi ya Siria ambayo kwa miaka hii imekabiliwa na mateso makubwa.

Wamefika  kama mahujaji mjini Roma katika kaburi la Mtume Petro wakati wa kumaliza sinodi yao ambayo imefanyika nchini Lebanoni siku za mwanzo wa mwezi. Baba Mtakatifu anasititzia kuwa, hicho ni kipindi msingi wa safari ya pamoja, ambayo Patriaki na Maaskofu wamealikwa kuchukua maamuzi mang’amuzi muhimu kwa ajili ya wema wa waamini, hata kwa njia ya uchaguzi wa maaskofu wapya, wachungaji ambao wawe mashuhuda wa Ufufuko. Mchungaji kama alivyofanya Bwana na mitume wake wawe karibu na roho za waumini, kwa kuwatuliza na kushuka kwa wale wenye kuhitaji; wakati huo huo wachungaji wawasindikize waamini kupania mambo yaliyo ya juu, kule Kristo aliko, wawe na shauku ya mambo ya juu na si mambo ya hapa duniani (taz. Kol 3,1-2).

Kutokan na hilo anafafanua zaidi kuwa, Kanisa lina mahitaji wa kuwa na Wachungaji wanaokumbatia maisha kwa moyo mkuu wa Mungu, bila kupendelea kushibishwa na mambo ya kidunia, bila kuridhika na kile ambacho tayari kipo, bali kuzingatia daima kwenda mbeza zaidi ya; wawe Wachungaji wa wanaotazama juu, na walio huru dhidi ya vishawishi vya kujitunza wenyewe binafsi, ambavyo ni vizingiti vya maisha ya uvuguvugu na mazoea; wawe wachungaji maskini, ambao hawashikilii fedha na mali; wawe wachungaji ambao wako katikati ya maskini wanao teseka; wanaotangaza kwa dhati matumaini ya Pasaka na safari ya pamoja na ndugu kaka na dada. Wakati huo  anakubaliana na uteuzi wa mkuu wao kwa maaskofu ambao wamemchagua na anataka kuunga mkono kwa ukubwa wa mtazamo wa mambo hayo aliyoyataja.

Kwa namna ya pekee amerudia kwa moyo wa dhati kwa kiongozi wao mkuu aliyechaguliwa kumshukuru  kwa hija hiyo. Na kwamba watakaporudi katika makao yao na kukutana na mapadre, watawa wote kike na kiume waamini, wawaeleze kuwa, yeye yupo pamoja nao katika sala. Na kwa maombezi ya mama Maria Mtakatifu mama wa Mungu na Mama wa amani, anawabariki na kuwalinda.

Amemalizia akiwashukuru!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

12/02/2018 15:23