Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Habari \ Habari kutoka Barani Afrika

Bara la Afrika linaendelea kujizatiti kuwekeza katika elimu bora

Bara la Afrika linaendelea kujizatiti zaidi katika maboresho ya sera na mifumo ya elimu ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kupambana vyema na mazingira yao! - REUTERS

07/02/2018 08:00

Huko Dakar, nchini Senegal hivi karibuni kumefanyika Mkutano wa wadau wa elimu ulimwenguni, wenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuendeleza takribani watoto millioni 870 walioko katika nchi maskini zaidi Afrika. Katika Mkutano huo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, akitoa hotuba yake amesema kuna kazi kubwa ya kufanya na anategemea sana ushirikiano wa kila mmoja. Katika kutimiza malengo haya, taifa la Ufaransa tayari limeanza kuongeza misaada yake kwa upande wa elimu kwenye nchi maskini zaidi Afrika.

Zinahitajika takribani Dolla Billioni 3.1 kwa muda wa miaka mitatu, 2018 – 2020, kwa ajili ya kusaidia watoto kwa elimu ya msingi na sekondari walioko kwenye nchi 67, ambazo aidha ni maskini zaidi au zimo katika kinzani mbalimbali. Kati ya nchi zinazotarajiwa kufaidika na mpango huo wa kuboresha elimu ni pamoja na Afghanstan, Jamhuri ya Watu wa Congo, Senegal na Tanzania. Baadhi ya wataalamu wamesema kwamba kazi ya kufanya ni kubwa mno katika sekta hiyo, hata hivyo dalili njema zimeishaanza kuonekana. Mfano mzuri ni nchi ya Senegal yenyewe ambayo imeongeza uwekezaji wake kwenye sekta ya elimu, nayo nchi ya Tanzania imeendelea kufafanua fursa ya elimu bure au kwa gharama nafuu zaidi, ili watoto wengi zaidi wapata fursa ya kupata elimu. Tukio hilo Jijini Dakar limehudhuriwa na wakuu wa mataifa na serikali kutoka nchi zilizoendelea, wawakilishi zaidi ya 50 wa nchi zinazoendelea na wafadhili 15. wameshiriki pia mashirika ya kimataifa, wawekezaji binafsi na mifuko kadhaa wenye kutoa kipaumbele kwa elimu.

Na Padre Celestine Nyanda

Vatican News!

07/02/2018 08:00