Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Mitandao miwili ya Internet iliyoanzishwa na maskofu Marekani kwa jamii!

Baraza Maaskofu wamefungua mitandao miwili ya kijamii kwa lengo la kuhafamisha, kujifunza zaidi ili kupambana na umaskini - AFP

03/02/2018 16:12

Mitandao miwili imeundwa kwa ajili ya kuleta ufahamu, kujifunza na kutenda kwa matedno halisi ili hatimaye kuweza kukabiliana na umaskini nchini Marekani. Huo ni mpango  ulioanzishwa hivi karibuni na Baraza la Maaskofu  wa Marekani , wakiwa na lengo la kutaka kuchangia mafunzo zaidi ya kina kwa waamini katoliki  kuhusiana na hali halsi ngumu ambayo inawalazimu walio wengi kuiishi.

Taarifa za hakika zinaeleza kwamba watu zaidi ya milioni 40,6 wanaishi katika hali ya umaskini na  (hiyo ni kwamba raia 1 kati ya 6 na mtoto 1 kati ya watano). Mwaka 2015, zaidi ya milioni mbili na nusu ya watoto wameonja uzoefu  wa kukosa mahali pa kuishi , kwa kuishi wanalanda landa tu mitaani na njiani, mwaka tu 2016 mpango wa shule wa kuhakikisha chakula cha watoto kinapatika kwa ajili ya kuishi, umesaidia kuwahudumia zaidi ya milioni 30.
Mitandao miwili ya kijamii inayoitwa Povertyusa.org na  Pobrezausa.org kwa lugha ya kingereza na kihispania inatoa nyenzo  na vileez zaidi vya ufahamu ili kuweza kuwasaidia wakatoliki kueleza imani yao kwa njia ya matendo halisi , hasa kufanya kazi kwa ajili ya kukabiliana  na umaskini unaozidi kutanda mizizi yake.

Mitandao hiyo miwili ya kijamii, inaonesha ramani pana ya takwimu juu ya umaskini kwa ngazi ya kitaifa,na wilaya, shughuli za kujikita katika matukio mbalimbali, zana za kuandaa  sala na na mawasiliano zaidi. Zaidi kuna maelezo kamili kuhusu matumaini, ambayo jumuiya ya watu wa marekani wanaendelea kuionesha na  kujikita katika shughuli hiyo ya kukabiliana na umaskini kwa mantiki mahalia. hata ramani kamili za kuonesha jinsi gani ya kutafuta hata mashirika mengine ya kibinadamu ya kuweza kuwafadhili na kusaidia njia ya kampeni ya maendeleo ya kibinadamu iliyo anzishwa na Maaskofu wa Marekani.

Askofu David Prescott Talley, wa Jimbo la Alexandria na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za ndani na mwandeleo ya binadamu ya Baraza la Maaskofu Marekani anasema, lengo lao ni kutaka kutafsiri hasa imani katika matendo halisi, kwa maana hiyo wao wanaalikwa kukutana na watu wote wa jumuiya zao wanaoishi katika hali ngumu.Umaskini Marekani ni hali halisi ambayo lazima kufanya kazi kwa pamoja na umoja, ili kutafisiri kwa dhati imani hiyo katika matendo na kutoa suluhisho la tatizo hilo.

Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu, umakini wa kukithiri katika familia ya Amerika, imezidi kutanda  hadi kifikia dola 24,000 kwa mwaka, ikiwa na maada ya kuishi karibia na dola 1,900 kwa mwezi. Kwa upande wa nchi nyingine wanaweza kuona kuwa ni kiasi kikubwa, lakini kumbe ni kinyume  kwa kufikiria gharama ya maisha na manunuzi ya matumizi zaidi kwa upande wa afya na shule, mamilioni ya watu wanaishi katika uzi mfinyo wa kukatika.

Mpango wa Baraza la Maaskofu wa kuzuia umaskini, ni mpango nyeti na maalumu kwa ajili ya watu walio pembezoni ambao kila siku wanakabiliana na changamoto za nchi hiyo,na wakati huo huo ni kwenda kukutana na mwili wa Kristo anayeteseka. Askofu Talley kwa niaba ya Maaskofu anasema , shughuli ya Baraza la Maaskofu kwa hakika ni ishara ya dhati ya mshikamano wa Kanisa na wajibu wa kupeleka matumaini na furaha ya Injili kwa ndugu wahitaji.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

 

03/02/2018 16:12