Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Ni watawa 31,000 nchini Poland wanao mtumikia Mungu na jirani!

Tarehe 2 Februari ni siku ya watawa duniani, siku iliyo anzishwa na Mt. Yohane Paulo II miaka 22 iliyopita - OSS_ROM

02/02/2018 15:04

Watawa katika dunia ni gurudumu la kuhamasisha upendo wa Mungu kati ya watu. Na umuhimu wa maisha ya kitawa ni kuonesha bayana ule  upendo wa Mungu kwa watu na ndiyo maana watawa katika ulimwengu wa leo  wanaalikwa kuhamasisha upendo huo na kuwa wajenzi wa utamaduni wa umoja.Watawa wanaonesha hali halisi ya Mungu na jirani lei hii katika dunia ambayo inahitaji.

Haya ni maneno ya hotuba ya Askofu Jacek Kiciński CMF, na mwenyekiti wa Tume kwa ajili ya Taasisi, mashirika na vyama vya kitume wa Baraza la Maaskofu wa Poland, wakati wa mkutano wake tarehe 31 Januari na waandishi wa habari kuhusiana na Siku ya watawa duniani, iliyo anzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II sanjari na Sikukuu ya Kutolewa Bwana Ekaluni kila tarehe 2 Februari ya kila mwaka.

Mkutano wa waandishi wa habari mwaka huu umejikita zaidi katika mada kuhusu ushirikiano na wote walio wekwa  wakfu na vijiana kwa mtazamo wa mantiki ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana ambayo inatarajiwa kufanyaika Oktoba mwaka huu.

Katika Kanisa la Polond wapo watawa wa kike 18,000 na karibu wamonaki wa wakiume 12,000, na wamonaki wa kike 1281, ukiongeza wasekulari wenye nadhiri pia wajane wa kike na kiume 1,000. Katika Taasisi 56 wapo mapadre 9302 na mafrateli 1313.Wapo watawa 18,000 wa mashirika 105 yanayofanya kazi. Katika monasteri  83 wanaishi mamonaki wa ndani 1281. Kati vyama vya kitume katoliki ni  100 ,wapo wasekulari wenye nadhiri 267 na 305 wajane na 2 wa kiume.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 

02/02/2018 15:04