2018-02-01 09:10:00

Pakistan:wakristo wameungana mpakani India kusali kwa ajili ya amani!


Tumesali na tumeshikana mikono kwa pamoja ,tumewasha mishumaa, ikiwa ishara ya kuomba Mungu msaada, hata kwa shughuli binafsi. Ni maombi kwa Mungu katika ukimya na  nyimbo za pamoja kwa ajili ya kuomba amani , heshima ya pamoja, kuhamasisha umoja na maendeleo kati ya nchi ya Pakistan na India.

Ni maneno ya Padre Francis Nadeem, Katibu wa Kamati kwa ajili ya majadiliano ya kidini na kiekumene wa Baraza la Maaskofu wa Pakistan, wakati wa kuhitimisha siku ya maombi ya umoja wa wakristo hivi karibuni mpakani wa India na nchi hiyo. Taarifa izinasema kuwa pamoja kwamba wameadhisha hivi karibuni siku ya uhuru dhidi ya waingereza, walioondoka 15 Agosti 1947, nchi hizi mbili bado zinaona maongezo ya cheche za hisia za utaifa ambazo zinaashiria mantiki za kidini, kwa namna ya pekee katika mahusiano ya waislam na wahindu. 

Katikati ya mwaka 80 hadi leo hii, majihadi wa kipakistan na mivutano ndani ya nchi ya India, imesababisha zaidi ya watu 40,000 sasa uwepo wa majanga ya sera za kisiasa katika nchi zote mbili, inazidi kuogezeka na kuhatarisha kati ya nguvu za kunyuklia. Juhudi kwa upande wa wakaristo zinahitajika, hasa za kukuza mahusiano wakati wa mkutano wa majadiliano kati ya watu na dini.

Na ndiyo fursa ambayo imewezekana wakati wa kuhitimisha Juma la maombi kwa ajili ya wakristo, mkutano uliofanyika katika Kanisa Katoliki la Kasur mpakani wa Pakistan na India,katika Jumuiya ya wamisionari wa Waoblati  wa Maria Imakulata, na kuudhuriwa na wachungaji wa madhehebu mengine ya kianglikani na wakuu wa majeshi mahalia pia.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.