Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Kuna ongezeko la wimbi la watu kuikimbia nchi ya DRC kutokana na ghasia!

Wimbi kubwa la watu kutoka DRC kuelekea Rwanda,Burundi,Uganda na Tanzania wakikimbia ghasia! - AFP

01/02/2018 09:36

Shirika la Wakimbizi UNHCR la Umoja wa Mataifa (UN) linaonesha wasiwasi mkubwa kutokana na ongezeko la vurugu kwa upande wa mashariki ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) ambapo imesababisha idadi kubwa ya watu kukimbia makazi yao kuelekea mashariki katika mipaka ya Burundi, Rwanda,Tanzania na Uganda. Maelfu na maelfu ya watu wameacha nyumba zao katikati ya operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya wenye silaha wa Mai Mai katika jimbo la Kaskazini ya Kivu. Tangu wiki iliyopita karibia watu 7,000 wamekatisha  mipaka ya Burundi na wengine 1,200 kuekelea Tanzania. Na inasemekana kuwa watu walio wengi wanaishi katika hali ngumu sana Kaskazini ya Kivu, na hata kukosa mahali pa kukimbilia na ukosefu wa chakula na maji ya kunywa!

Katika mahojiano ya wakimbizi na vyombo vya habari wanasema, wamekimbia kwa kulazimishwa na ghasia za moja kwa moja pia nyanyaso kwa upande wa makundi ya mgambo yenye silaha. Na wengine wamekimbia kutokana na operesheni ya wanajeshi kwasababu wanaogopa. Kwa maana hiyo upo umuhimu wa kuhakikisha kuwa watu hawa wanapata msaada wa usalama wakati wanakimbia hizo vurugu na kuwasaidia hata watu walio rundikana nchini DRC kuotkana na ghasia hizo.

Sehemu kubwa ya watu wanaokimbia nchini mwao ili kufika Burundi wanakatisha ziwa Tanganyika na mitumbwi midogo ya uvuvi. Kituo cha makaribisho kilichopo ziwa Nyanza na Rumonge ni kidogo hakuna nafasi ya kutosha kuwapokea watu wote, hata kituo cha afya, maji na chakula. Shirika la Wakimbizi na vyama vingine wakishirikiana na utawala wa nchi wanamokimbilia wakimbizi, wanajaribu kuwahamisha wakimbizi katika vituo vya mpito ambavyo lakini vimejaa huko mashariki ya nchi ya Burundi!

Taarifa pia inaeleza kuwa, wakongo wanaopitia pia katika ziwa Tanganyika wanafika Tanzania kupitia kaskazini ya kivu ili wafike mji wa Kigoma na maeneo yanayozunguka mji huo. Wimbi la watu hao wamekuwa hata vichaa na wengine ni wagonjwa. Hata hivyo, imeelezwa kwamba, wimbi hili la wakimbizi, linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa malazi, maji na hata huduma za choo, huku wengine wakiwa hawana jinsi zaidi ya kulala katika sehemu zilizo wazi. UNHCR imesema, hivi sasa inatafuta msaada wa chakula, maji na dawa katika maeneo ya kupokea wakimbizi, zaidi hata kuhamisha watu wapya kuwapeleka katika kambi za Nyarugusu kaskazini mwa Kigoma Tanzania.

Vile vile hata katika mipaka ya Uganda mwezi Desemba 2017, wanaonesha kuwa  wamefika wakimbiz zaidi ya 15,000 wakikatisha ziwa Albert kwa mitumbwi midogo na baadaye kutembea kwa miguu. Januari mwaka huu wamefika karibia watu 330 kila siku na idadi inazidi kuongezeka mara tatu ya mwezi Desemba.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

01/02/2018 09:36