2018-01-31 16:00:00

Ni lazima kutazama kwa upya halisi ya umaskini na madeni duniani!


Madeni duniani ni kutokana na matumizi mabaya ya fedha yanayosababisha hali ya ukosefu wa haki sawa , umaskini na ugumu wa hali nyingi za wahamiaji. Hali ya usimamizi mbaya wa fedha na madeni umegeuka kuwa kubwa kwa ngazi  ya nchi ya Italia  na kwa ulimwengu  mzima.  Hayo ni maelezo ya Askofu Mkuu katoliki wa Jimbo Kuu la Pescara- Penne Italia Italia,  wakati wa kutoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano, tarehe 27 Januari 2017, mkutano ulikuwa unaongozwa na mada ya “usimamizi wa fedha katika ulimwengu wa madeni ya umma nchini Italia”.

Askofu Mkuu Valentinetti, anasisitiza ya kuwa, madeni hayo yanayumbisha na kuleta umaskini zidi katika nchi zilizo maskini, hata katika nchi zinazotambulika kuwa na  maendeleo. Kwa hakikia anaongeza, madeni ni kitovu cha matatizo makubwa ya nyakati  hizi, na hivyo ni kipeo cha dharura ambacho wote lazima kutafakari kwa kina na kutafuta ufumbuzi. Akiendelea na hotuba yake amesema, miaka miwili iliyopita huko Genova nchini Italia walianzisha tafakari kuhusu ushirikiano na mshikamano kati ya ulimwengu Katoliki na watu waliotopea katika ulimwengu kwa mada kama hizi, hasa mara baada ya  miaka 15 ya kuafanya kwa Mkutano wa Wakuu wa nchi 8 Tajiri ( G8) za wakati hule huko Geneva,  pia  kutazama kwa upya mantiki zilizomo katika Waraka wake wa kitume wa Baba Mtakatifu Francisko, juu ya utunzaji bora wa mazingira “Laudato si”, mahali ambapo Baba Mtakatifu, anapendelea kukazia umuhimu wa maendeleo endelevu ambayo yanajikita katika kanuni ya maadili na utu wema, lakini pia mwanadamu apewe kipaumbele cha kwanza kwa kutafuta mafao, ustawi na maendeleo kamili ya mwanadamu huyo.

Pamoja na hayo Askofu Mkuu amekumbusha jinsi gani tukio la Jubilei ya mwaka 2000 walivyo anzisha  Kampeni hata Baraza la Maaskofu wa Italia, ili madeni ambayo yalikuwa mazito na kukithiri  katika baadhi ya nchi maskini yaweza kupunguzwa au kusamehewa kabisa! : Anaongeza, haya yalikuwa ni madeni mabaya na mengi, yasiyo halali, kwa sababu hayakuwa na malengo ya usawa, ni madeni ambayo yalikuwa ni  kichocheo cha  kuongezeka kwa uhamiaji. Hata hivyo Askofu Mkuu amewaalika kutazama kwa upya  hali halisi ya umaskini si katika kutafuta namna ya kutoa msaaada wa haraka tu,  bali hata usimamizi kama suala muhimu, ambalo linapaswa kujikita katika mzizi yake wa matatizo, kwa lengo la kuondoa kabisa sababu za umaskini. 

Na katika kuchunguza nyakati miaka ya mwisho inaonesha ripoti kuwa asilimia 1% ya watu diniani  wanaishi  na utajiri kati ya asilimia 80% ya utajiri wa dunia hii. Vilevile amewaleza  juu ya mkutano wake na Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 27 kabla ya kuanza mkutano huo, akiwa amewasindikiza wanafamilia wa waathirika wa Rigopiano. Hawa ni ndugu wa waathirika waliokufa katika nyumba moja ya kulala wageni iliyoangushwa na barafu kali mwaka jana na kusababisha vio vya makumi kadhaa. Askofu Mkuu anasema kuwa, alipompatia ratiba ya mkutano huo, Papa amesema “hiyo ndiyo njia ya kufuata” kwa maana hiyo amemalizia kwa kuthibitisha kuwa, kazi hiyo ya mkutano na jitihada zao tayari  zimebarikiwa na  Baba Mtakatifu!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.