2018-01-30 12:16:00

Askofu Alick Banda ateuliwa kuwa Askofu mkuu Jimbo kuu la Lusaka!


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Telesphore George Mpundu wa Jimbo Kuu la Lusaka, Zambia la kung’atuka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Alick Banda kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lusaka, Zambia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Alick Banda alikuwa ni Askofu wa Jimbo kuu la Ndola. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Alick Banda alizaliwa tarehe 15 Novemba 1963 huko Mufulira, Zambia.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 7 Agosti 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre! Tarehe 30 Mei 2007 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Solwezi na kuwekwa wakfu tarehe 29 Julai 2009. Tarehe 13 Novemba 2009, akateuliwa tena na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo Katoliki Ndola na kusimikwa rasmi tarehe 16 Januari 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.