2018-01-29 10:46:00

Mafungo ya Kiroho kwa Papa na Sekretarieti ya Vatican tarehe 18-23 Februari!


Kuanzia tarehe 18-23 Februari 2018, Baba Mtakatifu atakuwa katika mafungo ya kiroho na Sekretarieti nzima ya Vatican. Atakayeongoza tafakari ya mafungo ya kiroho mwaka 2018, ni Padre wa Kireno  José Tolentino de Mendonça. Mafungo ya kiroho yataongozwa na kauli mbiu: “Sifa ya kiu” ambayo Mkuu msaidizi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Lisbon na mshauri wa Baraza la Kipapa la Utamaduni, amechagua kuwakilisha kwa Baba Mtakatifu na Sekretarieti ya Vatican kuanzia tarehe 18 hadi 23 Februari huko Ariccia, Roma.

Padre José Tolentino de Mendonça alizaliwa nchini Ureno mnamo mwaka 1965, na kupewa daraja Takatifu la Upadre mwaka 1990. Ni mtaalimungu na mtunzi wa mashairi , ambaye ni mmoja ya sauti maarufu inayosikika katika ulimwengu wa utamaduni kwa nchi yake, ambaye alipata kuwakilisha usanii huo rasmi mnamo mwaka 2014, katika Siku ya Mashairi duniani!

Ratiba ya mafungo ambayo kama kawaida hufanyika katika nyumba ya Mafungo iitwayo "Divin Maestro", yaani Mungu Mwalimu inaonesha kuanza siku ya Jumapili saa 12 jioni masaa ya Ulaya, kwa utangulizi, kuabudu na masifu ya jioni. Siku sitakazofuata , kila siku wataanza na Ibada ya Misa Takatifu saa 1.30 ya kila asubuhi, ikifuatia tafakari ya kwanza saa 3:30.

Kwa njia hiyo kuanzia saa 10.00 jioni itakuwa ni sehemu ya pili ya tafakari , ambayo itakuwa ikifuatiwa na masifu na kuabudu Ekaristi Takatifu. Na siku ya mwisho ya mafungo ambayo ni tarehe 23 Januari 2018, ratiba inaonesha kwamba kutakuwa na  tafakari moja tu.

Aidha “Wanafunzi wa mshangao itakuwa ni mada ya tafakari ya Jumapili tarehe 18 Februari, ambayo itafungua tafakari ya kipindi cha mafungo. Kwa siku zitakazofuata, mada za kutafakari zitakuwa: sayansi ya kiu; nimegutuka kuwa nina kiu; hiki ni kiu cha bure; kiu ya Yesu; machozi yanasimulia kiu; kunywa kutoka katika kiu yako; aina za shauku; kusikiliza kiu za pembezoni; na heri za kiu!

Aidha taarifa zinaonesha kwamba mada ya tafakari ya siku ya kuanza mafungo Jumapili tarehe 18 Januari, itakayongoza utangulizi wa mafungo itakuwa ni “wanafunzi wa mshangao”. Kama kawaida ya kipindi cha mafungo,  mikutano binafsi na maalumu, ikiwemo hata katekesi ya kila Jumatano havitakuwapo!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.