2018-01-29 15:48:00

Kardinali Parolin amekabidhi Tuzo Padre Jacques Hamel huko Lourdes!


Baada ya Misa iliyoongozwa na Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican wakati wa kuhitimisha Siku ya 22 ya  Mtakatifu Francisko wa  Sales, Msimamizi wa waandishi wa Habari, iliyoongozwa na mada ya Vyombo vya habri na Ukweli, Kardinali Parolin alipata kukabidhi “Tuzo Padre Jacques Hamel”, iliyotolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya Padre huyo, aliyekuwa na umri wa miaka 84,aliuwawa mikononi mwa magaidi wawili wa kijihadi mnamo asubuhi ya tarehe 26 Julai 2016 akiwa anaadhimisha ibada ya misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Etienne du Rouvrey huko Rouen nchini Ufaransa. Maadhimisho siku ya 22 ya Mtakatifu Francisko wa Sales na utoaji wa tuzo hiyo yamefanyikia huko Lourdes. Maadimisho hayo alikuwapo hata dada yake marehemu Padre Jacques, ambapo  Roseline Hamel,amemshukuru Mwenyekiti wa Shirikisho la Habari Katoliki Jean-Marie Montel.

Wakati huo huo kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, Kardinali Pietro Parolin alitoa hotuba yake, akiwasifu wahudumu wote katika sekta ya mawasiliano, katika kuandaa tukio hili la kumbukumbu ya Padre Hamel, na kwamba wameonesha kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko aliandika katika ujumbe wake, mwaka jana: “wale ambao wanajiachilia kuongozwa kwa imani na Roho Mtakatifu, wanakuwa na uwezo wa kung’amua na kutambua tendo la Mungu katika kila tukio ambalo linaendelea kutanda katika historia ya wokovu”.

Na katika mahubiri ya Kardinali Pietro Parolin,amesisitiza juu ya kazi ya kuwa waandishi, wakati huo huo akibainsha kuwa ni msingi katika jamii iliyo huru iliyo jaa utamaduni kama anavyosistiza hata Baba Mtakatifu kwamba: “kuwa na taaluma ndogo huathiri jamiii kama ile ya uandishi wa habari”. Kwa maana hiyo anasisitiza juu ya umuhimu wa nafasi ya uandishi wa habari na ukuu wake kwamba inahitaji uwajibikaji.

Pamoja na hayo, akitafakari somo la siku, mahali ambapo somo liliongozwa na barua ya Mtakatifu Paulo kwa Timoteo kwa kuonesha utume wake, kama huduma ya Mungu na ili aweze kufanya watu watambue ukweli ambao unawapelekea kuwa na huruma na pia huru wa kutumikia. Kardinali anabainisha kwamba huruma kwa upande wa wakristo ina maana ya kuiga Kristo na  kuishi kwa upendo ambao uanjionesha katika sura ya Baba.  

Nini Maana ya ukweli? Kardinali akitafakari zaidi, amefikiria neno la kiyahudi lisemalo “emet”, yaani mzizi wake una maana ya amani katika liturujia yetu,na kwa maana hiyo ni ukweli; kwa njia hiyo anathibitisha kuwa ukweli maana yake ni mwenendo wa uaminifu. Aidha anasisitiza ukweli huo hata Mtakatifu Yohane kwamba, iwapo mienendo  yetu si ya uaminifu, sisi ni waongo na matukoe yake ni kutoa habari za fake news! Kwa maana hiyo ukweli kwa wakristo maana yake ni mtu, na Yesu mwenyewe anathibitisha kuwa “Mimi ni Njia, ni Ukweli na Uzima”. Kutokana na maana hiyo hata sisi wenyewe tunaweza kuingia katika ukweli huo kwa kufuata unyenyekevu, kuishi umoja na Yeye hata ndugu zetu!

Kardinali anasema kuwa mawasiliano ni muhimu ili kuweza kuunda mtazamo wetu hata katika kutoa sifa za utume wa Kanisa na Ulimwenguni, na ili kuimarisha na kukuza roho  za kibinadamu. Amekumbusha maneno ya wito wa Askofu Dominque Lebrun, Askofu wa Rouen  alio utowa kwa vijana wakati wa Siku ya Vijana huko Poland na kabla ya Padre Humel kurudi nchini mwake Ufaransa:“Hebu tusikate tamaa  mbele ya uso wa vurugu na tuwe mitume wa ustaarabu wa upendo”.

Akifafanua zaidi juu ya utoaji wa habari ,Kardinali, anasema, katika majanga ya sasa yanayojionesha ya habari, waandishi wa habari wanayo nafsi na jukumu muhimu na hasa la kupinga chuki na vurugu na majadiliano yanayoleta uchochezi; Kwa hiyo anapendekeza miongozo mitatu muhimu ambayo inaweza kuwa kivutio cha kazi ya waandishi wa habari ili kuhimiza kuishi pamoja na umoja: wajibu wa utambulisho, ujasiri wa wengine na uaminifu wa nia.
Kwa kuhitimisha ametumia maneno ya Roseline, dada yake Padre Jacques: “Mungu wa Upendo na huruma, amekuchagua uwe katika huduma ya wengine ili kukuza upendo, kushirikiana na kuvumiliana miongoni mwa watu wa imani zote. Tujifunze kuishi pamoja kwa maana sisi ni mafundi wa amani, kila mmoja kwa njia yake mwenyewe, kwa sababu ulimwengu unahitaji tumaini!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.