2018-01-29 15:14:00

Ireland:Wito wa Maaskofu kuhusu kupinga kura ya maoni ya utoaji mimba!


 “Ikiwa jamii inakubali kuwa mwanadamu anayo haki ya kumaliza maisha ya mwingine, basi haiwezekani kudai haki ya maisha kama haki ya msingi ya binadamu kwa mtu yeyote”. Haya ni maelezo ya Askofu wa Ireland  Kevin Doran (Elphin) Mwenyekiti wa kikosi cha masomo juu ya elimu ya viumbe wa Tume ya Baraza la Maaskofu katika ujumbe wa kichungaji uliotangazwa tarehe 28 Januari 2018, akirudi katika mada ya utoaji mimba , kwa kusubiri matokeo ya mkutano wa serikali ya nchi ambao, tarehe 29 Januari 2018 unatarajia kutoa ruhusa ya kwenda mbele katika kupanga tarehe ya kupiga kura ya maoni juu ya suala la utoaji mimba.

Maaskofu wanaandika katika ujumbe wao kuwa, ikiwa tunatoa sababu yoyote ya utoaji mimba, hoja hiyo itakuwa sawa inatumika kuhalalisha mwisho wa maisha ya wazee, wadhaifu au ulemavu mkubwa. Na ikiwa tutavuka mpaka huu, haitakuwa rahisi kurudi nyuma. Halikadhalia,Maaskofu wanaelezea  matokeo yanayoweza kutokea iwapo wanaondoa  kipengele cha katiba hiyo  ya 40.3.3, ya nchi  kwamba, marekebisho kuhusu maisha, yatakuwa mabaya sana, kwa sababu wanaweza kuondoa katika Katiba, ule mwongozo wa haki ya maisha ya mama na mtoto bila kuchukua nafasi yake ya bure: na itakuwa kama vile, hundi tupu  mikononi mwa serikali, huru katika siku zijazo kuanzisha  taratibu wa utashi wa hovyo wa  utoaji mimba.

Kwa njia hiyo Askofu kwa niaba ya maaskofu wote  anahimiza waamini wote na wenye mapenzi mema katika ujumbe huo ya kwamba wawe na huruma, ukweli, maombi, msaada kwa wanawake, pia kuwaweleza kwamba, chochote kinachoweza kutokea kuhusu  Katiba hiyo, wao, tayari wako wanatafuta kusoma mbinu na  njia  za kuzingatia ili kuwa na uwezo wa kutoa msaada, zaidi kwa wanawake ili waweze kuchagua maisha, si tu kwa mtoto peke yake lakini pia kwa ajili yao wenyewe!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.