2018-01-29 14:22:00

Bangladesh miito inaongezeka na jimbo la Sylhet seminari mpya kuzinduliwa!


Miito ya kitawa inazidi kuongezeka katika maeneo ya makabila huko Bangladesh,na kwa siku zilizo pita imezinduliwa seminari moja ya Jimbo la Sylhet huko Kaskazini ya nchi. Hiyo ni seminari ndogo ya Mtakatifu Yohane iliyofadhiliwa na Jimbo Katoliki la Suwon nchini Korea, ambayo itawakaribisha waseminari 60. Kwa mujibu wa habari zinasema kuwa kwa sasa wito vijana 22 ambao wanataka kutangaza ujumbe wa kikristo katika nchi na Ulimwengu. Ufadhili wa kujenga seminari hiyo umetolewa  katika Jimbo la Suwon nchini  Korea ya kusini , katika makao makuuu ya Ubalozi wa Vatican na baadhi ya wafadhili mahalia wa jimbo. Taarifa pia inasema kuwa katika Jimbo la Sylhet, wanatoa huduma mapadre 16 na watawa 30. Wakatoliki wa kwanza walifika katika jimbo hilo karibia miaka 60 na ambao walikuwa ni wamisionari wa Oblati wa Maria mkingiwa wa dhambi ya asili (Omi) na kwa sasa wakatoliki ni zaidi ya 19,000.

Naye Askofu Bijoy Nicephorus D’Cruze wa Jimbo la Sylhet anabainisha kuwa katika maeneo hayo, sehemu kubwa ya wakazi ni wa makabila mengi, kwa maana hiyo waseminari watakuwa na fursa kubwa ya kutangaza Injili katika maeneo hayo. Pia Askofu  D’Cruze anasisitiza kuwa, karibia asilimia  98% ni wakatoliki. Kwa upande wa makabila hayo ni vigumu kuishi katika mji wa Dacca kwasababu wanatumia  lugha na utamaduni tofauti na wa mji huo. Zaidi katika Jimbo la Sylhet kuna mbali na mji Mkuu na wazazi wengi ni maskini hawana uwezo wa kuwatuma watoto wao kwenda kusoma masomo yao nje .Lakini kwa sasa anaongeza Askofu , kwa upande wa vijana itakuwa rahisi kwenda seminari, na mara moja kwa kila mwezi wazazi wao wanaweza kuwatembelea.

Kwa kufanya hivyo, vijana hao watabaki na mawasiliano na familia zao, na ndiyo matarajio yake Askofu ya  kuwa seminari hiyo inaweza kuwa chachu ya jumuiya nzima, ambayo kila mwaka kwa shauku kubwa wamekuwa wakishiriki kutoa mchango wao kifedha kuwasaidia waseminari na shule zenye mafunzo katoliki. Ili kuweza kuwafanya vijana waweze kung’amua vema maisha ya kitawa na kikuhani, Kanisa la Bangladesh kwa miaka ya hivi karibuni wamejikita kwa kina katika kuhamasisha kwa njia nyingi, na kazi ya njia hiyo imejionesha katika miito ya sasa. Ni tukio linalotazama majimbo yote ya nchi. Lengo kubwa ni lile la kuhakikisha wanaandaa vijana jinsi gani ya kuendesha maisha ya kitawa na kikuhani kwa mantiki hasa ya nini maana ya kujitoa kuhudumia na kuwa mtumishi au mchungaji. Mapadre na maaskofu wanawatia moyo wote vijana kujikita katika mchakato, hata mingine inayofafana na hiyo katika mang’amuzi ambayo hadi sasa imeleta manufaa, kuona waseminari wengi kati ya watu wa makabila ambao wanazidi kuongezeka.

Gazeti la Asianews linenaendelea kueleza juu ya maadhimisho ya usinduzi wa seminari ndogo ya Mtakatifu Yohane, kuwa yaliendeshwa na Askofu Mkuu George Kocherry, ambaye ni Balozi wa Vatican nchini Bangladesh, Akisaidiana na Askofu D’Cruze na kuudhuriwa na waamini wengi wakatoliki , mapadre 22 na zaidi ya watawa wa kike 30. Katika eneo ambali seheku kubwa ni waislam kwa maana hiyo ufunguzi wa seminari hiyo katika eneo hilo unawakilisha tatukio la kipekee.Tukio hilo kwa dhati linaonesha kuwa nchi ya Bangladesh, miito ya kumfuasa Kristo inazidi kuongezeka tofauti na tabia inayozidi kutawala katika ulimwengu wa nchi za Ulaya.

Naye Padre Lawrence Toppo Gombera wa Seminari hiyo ndogo ya Mtakatifu Yohane anasema, vijawa wao kwanza walikuwa wanakwenda katika Seminari ndogo ya  Bandhura mjini (Dacca), karibia umbali wa 300 km kutoka mahali walipo. Na walikuwa na uwezo wa kutuma vijana watano tu, sasa wataweza kupokea vijana 13 kila mwaka. Na wakati endelevu watakuwa na fursa ya kuwa na makuhani wengi ambao wataweza kutangaza ujumbe wa Mungu!

Sr Angela Rwezaula
 Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.