Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa Francisko anawaomba waamini umakini wa Neno la Yesu lenye nguvu na uwezo!

Papa Francisko anawaomba waamini umakini wa Neno la Yesu lenye nguvu na uwezo wakati wa mahubiri yake katika sala ya Malaika wa Bwana - AFP

28/01/2018 14:29

Injili ya Jumapili kutoka Mtakatifu (Marko 1,21-28) ni sehemu kubwa ya maelezo marefu ya siku yake huko Kafaranaumu. Kiini cha maelezo ya leo yapo katika matukio ya kuponyesha mahali ambapo Yesu anajionesha kama nabii wa nguvu katika meneno na matendo. Ni Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyo anza nayo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Jumapili tarehe 28 Januari 2018 katika viwanja vya Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu anasimuli  kuwa, Yesu aliingia katika Sinagogi ya Kafaranaumu siku ya Jumamosi akassnza kufafundisha; watu walibaki na mshangao wa maneno yake maalumu, ambayo hayakufanana na yale waliyokuwa wamezoe saikia kawaida kusika. Waandishi kwa dhati, walikuwa wanafundisha bila kuwa na madaraka yoyote, kwa mana maneno yao yalisimamia juu ya utamaduni wa kuridhisha kile walichosema watangulizi wao, Musa na manabii. Lakini Yesu anafundisha akiwa na madaraka  na kuonesha kuwa ametumwa na Mungu na si mtu wa kawaida wa kufundiah juu ya tamaduni zilizotanguliwa. Yesu kwa hakika  anayo madaraka kamili. Mafundisho yake ni mapya  kama isemavyo Injili.

Wakati huo huo anaonesha kuwa na uwezo. Ndipo katika  Sinagogi anatokea mtu aliye na pepo wabaya na kusema,” una nini ee Yesu wa Nazareth ? umekuja kutuhari? Ninajua wewe ni nani: Mtakatifu wa Mungu”(..24). Roho  chafu inatambua nguvu ya Mungu na kutangaza utakatifu. Lakini Yesu ananyamazisha; na ni kwa kutumia maneno machache tu, yanatosha kuleta ushindi dhidi ya shetani, maana pepo wabaya hao wanamtoka mtu huyo akipiga kelele kwa nguvu zaidi(….24)
Tendo hilo linawashangaza watu waliokuwapo; wote walikuwa na hofu na kujiuliza je huyo ni nani(…) anahamuru pepo wabaya na wanatii! (…)Nguvu ya Yesu inathibitisha madaraka ya mafundisho yake. Yeye hatoi maneno tu bali hata matendo. Kwa maana hiyo anaonesha mpango wa Mungu kwa maneno na katika nguvu ya matendo yake. Katika Injili kwa dhati tunaona kuwa Yesu, wakati wa utume wake ,alionesha upendo wa Mungu kwa njia ya kuhubiri na hata ishara nyingi makini, kama vile za kusaidia wagonjwa,wenye matatizo, watoto na wenye dhambi.

Injili ya leo hii, Baba Mtakatifu anathibitisha, ina mwonesha Yesu kuwani mwalimu wetu, mwenye nguvu ya maneno na matendo. Yesu anawasiliana nasi katika mwanga wake wote ambao unaangaza njia zetu, wakati mwingine zilizo jaa giza la maisha; yeye anatangaza hata nguvu muhimu kwa ajili ya kukabiliana na matatizo, majaribu na vishawishi. Fikirieni neema hiyo kubwa kwa ajili yetu tuliyo nayo ya kutambua Mungu aliye na nguvu hivyo na mwema! Mwalimu na rafiki anatuonesha njia na anatusindikiza kwa namna ya pekee sisi wahitaji.

Na Bikira  Maria ,mama msikivu atusaidie kufanya ukimya ndani na nje yetu ,ili kusikiliza kwa makini ujumbe wa neno lenye  nguvu   la mwanae Yesu Kristo, analitangaza kwa maana ya maisha yetu na kutuokoa kila aina ya utumwa hasa wa ubaya pamoja na kelele kubwa za ulimwengu huu.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

28/01/2018 14:29