2018-01-28 15:13:00

Papa Francisko anasema tumkimbilie Bikira Maria usalama hakika wa maisha!


Kama watu wa Mungu katika safari, tupo hapa kukaa katika ekalu la Mama. Uwepo wa Mama unafanya ekelu hili kuwa kama nyumba ya familia yetu sisi watoto wake. Kwa pamoja, kizazi hadi kizazi cha Waroma , tunatambua nyumba ya mama kuwa ni nyumba yetu, nyumba ambayo tunapata tunu na faraja, ulinzi na kimbilio. Wakristo wanajua tangu mwanzo katika matatizo na majaribu, ni lazima kukimbilia kwa Mama kama unavyoeleza wimbo wa zamani wa Maria usemao, ”tunakimbilia ulinzi wako, mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukioomba katika shida zetu, utuokoe siku zote kila tuiingiapo hatarini, ewe bikira Mtukufu,mwenye baraka amina”.  Ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya Jumapili tarehe 28 Januari 2018, katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu, kuadhimisha Sikukuu ya Tafsiri ya Maria afya ya watu wa Roma, “Salus Popoli Romani”.

Akifafanua maana ya sala hiyo anasema:Tunakimbilia ulinzi wako: Mababa zetu katika imani walifundisha kuwa katika kipindi kigumu ni lazima kukimbilia chini ya kivuli cha Mama Mtakatifu wa Mungu. Katika tamaduni hizo walikuwa na tabi ya kwamba katika kipindi cha vurugu na mahitaji walikuwa wakitafuta kimbilio kwa wanawake waliokuwa wa hali ya juu, walikuwa wakitandaza vazi lao kama ishara ya kukaribisha na ulinzi. Na kwa njia hiyo, hata sisi sote  tuko mbele ya mtazamo wa Mama Maria, mwanamke wa hali ya juu anayezaa binadamu.  Joho lake daima ni wazi linalopokea  na kukusanya. Hata hivyo Baba Mtakatifu  anaeleza kuwa , Joho la ulinzi linatukumbushwa wakristo wa mashariki ambao wanaibada ya kuandishimisha Ulinzi wa Mama wa Mungu kwa picha nzuri inayoonesha joho  kubwa lililowazi na kuwakaribisha  watoto na kufunika dunia nzima.

Hata Mamonaki wa zamani walikuwa wanashauri wakati wa majaribu kukimbilia chini ya joho la Mama Mtakatifu wa Mungu, wakimuomba Mama Mtakatifu, aliye kuwa tayari anahakikisha ulinzi na msaada katika sala kwa kutumia  maneno machache  tu ya kwamba:  Mtakatifu Mama wa Mungu, Mtakatifu Mama wa Mungu! Hekima hiyo inayotoka mbali  inatusaidia kuelewa kuwa Mama anatunza imani, analinda mahusiano, anaokoa katika majanga na kuokoa katika ubaya. Mahali ambapo kuna nyumba ya Mama Maria, shetani haingii. Nyumba ambayo Mama Maria yupo, ibilisi haingii. Mahali ambapo yupo Maria, hakuna wasiwasi , woga na huzuni.

Je ni nani hasiyehitaji , je ni nani hasiye kuwa na wasiwasi na mahangaiko. Mara ngapi mioyo yetu imegubikwa na bahari yenye mawimbi makali , na  matatizo yanapuliza! Mama Maria ni mashua ya hakika katikakti ya gharika. Si mawazo au teknolojia ya kuweza kutoa nguvu na matumaini , bali ni uso mpole wa Mama na mikono yake itakayo tubembeleza katka maihisha, joho lake lenye kivuli linatukinga; na hivyo tujifunze  mahali pa kukimbilia kila siku na  kwenda kwa mama Maria.

Baba Mtakatifu akitafakakari; juu ya husitunyime tukiomba; tunapokuwa tunaomba naye Mama Maria anaomba kwa ajili yetu. Kuna neno la kigiriki lisemalo Grigorusa,maana yake, ambaye yuko tayari. Utayari huo ni tendo ambalo Mtakatifu  Luka anatumia katika Injili ili kuonesha kuwa Mama Maria alikuwa tayari na alikwenda kwa haraka haraka kwa Elisabeth! Na namna hiyo yeye daima yu tayari, anomba kwa haraka ! Hata katika Injili ya Yohane, Maria anaonesha utayari na kumwambia Yesu kwa haraka kuwa,  hawana divai (Yoh 2,3).

Kwa njia hiyo tunapokosa matumani , kukata tamaa, kukosa furaha , nguvu zinapoisha ,tunapokosa nyota mbele yetu za maisha, Mama Maria ni msaada. Yeye hawezi kamwe kudharau maombi yetu hawezi kuacha hata sala moja iende bure. Mama Maria haoni aibu kwa ajili yetu, kinyume chake anasubiri ili aweze kusaidia wanae. Baba Mtakatifu ametoa historia ya mwammke mmoja aliyekuwa hospitalini akimuuguza mwanae aliyekuwa amepatwa hajali mbaya na kwamba historia hiyo inaweza kufanya tuelewa zaidi; Mama huyo alikuwa pale usiku na mchana : Siku moja akalalamika kwa Padre akisema, Je Bwana hakutoa ahadi kwetu sisi mama? Je kitu gani, Padre akauliza.  Kuchukua mateso ya watoto” akajibu mwanamke. Tazama moyo wa mama Baba Mtakatifu anaongeza: haoni aibu ya majeraha na udhaifu wa watoto bali anataka kuyachukua mwenyewe. Na Mama wa Mungu na pia mama yetu anataka kuchukua mateso na uchungu, kutuliza , kusimamia na kuponya.

Utuokoe siku zote hatarini:  Bwana mwenyewe anatambua kuwa tunahitaji kimbilo  na ulinzi katikati ya hatari. Na kwa njia hiyo katika kipindi kigumu akiwa juu ya msalaba, alimwambia mwanafunzi wake mpendwa " tazama huyo ni Mama yako (Yh 19,27) . Mama siyo jambo la kusachugua yeye ni urithi wa Kristo. Na sisi tunahitaji msaada wake tulio katika safari, na  kama mtoto anayetaka kuwekwa mikononi.Ni hatari kubwa katika imani kuishi bila mama, bila ulinzi na kuacha ukavutwa na maisha kama  upepo unavyopeperusha majani ya mti.  Bila ulizni wa Mama hatuwezi kuwa wana, kwa maana hawali ya yote sisi ni wana waoendwa ambao wana Baba Mungu na Mama Maria kama Mama.

Katika mtaguso wa Pili wa Vatican unatufundisha:Maria ni ishara ya hakika ya matumaini na faraja kwa ajili ya safari ya  watu wa Mungu (Cost. Lumen gentium, VIII, V). Ni ishara ambayo Mungu aliiweka kwa ajili yetu na tusipoifuata tutakwenda nje ya njia. Hiyo ndiyo ishara ya maisha ya kiroho inayopaswa kutafakariwa kwa  kina. Je tunasubiri nini kutoifuata katika safari yetu kama mtume chini ya msalaba aliyempokea Mama Maria kati ya mambo mengi?(Yh 19,29) Hata sisi katika nyumba ya mama tumkaribishe  Maria katika nyuma zatu, yaani mioyoni mwetu na katika maisha yetu.

Si rahisi  kuondokana na Mama , maana matokeo yake ni kupoteza utambulisho wa kuwa watoto na utambulisho wetu kama watu na si ukristo unaotengenezwa na mawazo na mipango bila kuamini, bila huruma na bila moyo. Lakini bila moyo hakuna upendo na imani hiyo inakuwa hatari ya kugeuka kuwa tamthiliya ya vipindi vingine. Badala yake Mama anawatunza na kuwafunika watoto wake. Anawapenda na kuwalinda kwasababu wapate kupenda na kulinda ulimwengu.

Baba Mtakatifu anasema tumkaribishe Mama Maria awe kimbilio letu la kila siku na  awe usalama hakika katika nyumba zetu. Tumwamini kila siku; tumwombe kila wakati tunapokuwa na shida yoyote na tusisahau kurudi kwake kushukuru. Na kama yule mama baada ya kutoka hospitali, tumtazame kwa aliye na macho ya huruma na kumsalimia kama walivyo kuwa wakisalimu wakristo wa Efeso mara tatu “Mama Mtakatifu wa Mungu, Mama Mtaktifu wa Mungu, Mama Mtakatifu wa Mungu”.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News
 








All the contents on this site are copyrighted ©.