Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Papa amepokea na kukubali kuwatangaza wenyeheri wapya wa Kanisa!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kardinali Angelo Amato Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa mchakato wa kutangaza watakatifu

27/01/2018 15:59

Tarehe 26 Januari 2018 Baba Mtakatifu amekutana na Kardinali Angelo Amato S.D.B, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mchakato wa kuwatangaza wenye heri na Watakatifu. Katika mkutano wao, Baba Mtakatifu ametambua na kukubali kuwatangazwa wenye heri: Mtumishi wa Mungu Nazaia Ignazia wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Mwanzilishi wa Shirika wa Wamisionari wa Kanisa. Alizaliwa huko Madrid Huispania, tarehe 10 Januari 1889 na kifo chake huko Buenos Aires (Argentina) tareh  6 Julai 1943;

Mtumishi wa Mungu  Alfonsa Maria Eppinger, Mwanzilishi wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Mwokozi; alizaliwa huko Niederbronn (Ufaransa), tarehe  9 Septemba 1814 na kifo chake tarehe 31 Julai 1867; Mtumishi wa Mungu Clelia Merloni, Mwanzilishi wa Shirika la Mitume wa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Alizaliwa tarehe 10 machi  1861 huko Forlì (Italia) na kifo chake tarehe 21 Novemba 1930 Roma;

Mtumishi wa Mungu Maria Crocefissa dell'Amore Divino (zamani: aliitwa Maria Gargani), Mwanzilishi wa Shirika la Mitume wa Moyo Mtakatifu ; alizaliwa tarehe  23 Desemba 1892 huko Morra De Sanctis (Italia) na kifo chake tarehe  23 Mei  1973  Napoli (Italia); Utambuzi wa kifodini cha Mtumishi wa Mungu, Pietro Claverie, wa Shirika la Fratelii Wahubiri na Askofu wa  Oran, na wenzake  18 wakiume na kike walio uwawa wakitetea imani yao nchini Algeria kati ya Mwaka 1994 - 1996; Kifodini cha Mtumishi wa Mungu Veronica Antal,  Mlei,  wa Shirika la wasekulari wa Mtakatifu Francisko wa Asizi; alizaliwa tarehe  7 Desemba  1935  huko Nisiporeşti (Romania)  na kuwawa kwa ajili ya kutetea imani yake tarehe 24 agosto 1958 huko Hălăuceşti (Romania);

Fadhila za Mtumishi wa Mungu Ambrosio Grittani, Padre wa Kijimbo na Mwanzilishi wa Waoblate wa Mtakatifu  Benedikto  Giuseppe Labre; alizaliwa huko Ceglie del Campo (Italia), tarehe 11 Oktoba 1907 na kifo chake tarehe  30 Aprili 1951 huko Molfetta (Italia); Fadhila za Mtumishi wa Mungu Anna-Maria Maddalena Delbrêl, Mlei; alizaliwa huko Mussidan (Ufaransa) tarehe  24 Oktoba 1904  na kifo chake  huko  Ivry-sur-Seine (Francia) tarehe  13 Oktoba 1964.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

27/01/2018 15:59