2018-01-27 11:04:00

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kufanya mkutano wa mwaka!


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Anawashukuru wote kwa niaba ya Mwenyekiti wake Askofu mkuu Luis Francisco Ladaria Ferrer, S.J., katika maneno ya utangulizi wa mkutano wao, akisisitiza juu ya umuhimu wa shughuli ya mkutano wa kuhusu miaka miwili ya mwisho.

Anawapongeza kwa huduma yao nyeti ambayo inajaribu kujibu kwa namna ya pekee mahusiano ya Baraza la Kipapa na Mfuasi wa Kharifa wa Mtume Petro ambaye anaitwa kuimarisha ndugu wote  katika imani na umoja wa Kanisa. Anawashuru kwa kazi yao ya  ila siku kusaidia Baraza la Maaskofu na kuhakikisha kuwa sahihi mchakato wa imani na utakatifu wa sakramenti, hata katika masuala tofauti ambayo leo hii yanahitaji mang’amuzi ya kichungaji na muhimu kama vile utatifi wa kesi zinazohusiana na delicta graviora utaratibu wa kuendesha kesi za makosa makubwa ya uhalifu:imani au maadili: makosa yanayohusu sakramenti, kitubio na amri ya sita.

Kazi zote hizi Baba Mtakatifu anasema,bado zinahitaji juhudi kubwa ya kukabiliana kwa upeo wa dhati, kwani matokeo daima yanazidi kuendelea, yenye tabia ya utambuzi wa binadamu,  ambayo yanajikita hasa katika uchuguzi wa maadili. Binadamu wa leo hajijuhi yeye binafsi ni nani, hivyo inakuwa vigumu kutambua jinsi gani ya kutenda yaliyo mema. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anasema, ni wazi kuona kuwa kuna shughuli  ya Baraza lao kuhimiza na kutoa  wito utokao kwa Mungu na kwenda  kwa binadamu  ili aweze  kutafuta kuunganisha maoni yake ya kweli ukweli na wema ambao unajikita imani katika Kristo Yesu. Hakuna kisichoshindwa, iwapo sababu hizo zinaweza kujifunza katika mwanga wa Mungu, inamsaidia mtu kujifungua yeye mwenyewe na kuwa ishara ya Mungu katika ulimwengu.

Baba Mtakatifu anakumbusha juu ya tafiti wanazoendelea nazo iili hatimaye kuweza kuonesha maadili yanayostahili ya mafundisho ya binadamu hata katika sekta ya uchumi na fedha. Ni kwa njia ya upeo tu wa binadamu unaweza kuwa msingi kwenye mahusiano na kuupanua kwa dhati ,wenye uwezo wa kutanda jambo msingi la maadili ya binadamu. Hata Hivyo: mafundisho ya  Kanisa daima yaneonesha wazi juu ya mtazamo wa shughuli za kiuchumi ambazo ni lazima kwenda na sheria na mtindo wake wa kiuchumi lakini katika mantiki ya maadili (Conc. Ecum. Vat. II, Cost. past. Gaudium et spes, 64).

Katika utume wao, unachukua nafasi kubwa ya kutazama kwa mapama shughuli za kichungaji. Wachungaji wa kweli ni wale ambao hawatupi binadamu peke yake, hata kumwacha mikononi mwa mawindo ya upotofu na makosa, bali wanakuwa wahudumu wa kumkomboa , wanaweza kumrudisha ili aweze kujijua kutambua  uso wake katika wema. Kila mchangaji wa kweli ni mwenye mikono ili wazi na inayosubiri, hasa akiona wale ambao wanapotea, kwa maana ya ukosefu wa hadhi yake  na kuwarudisha wawe na matumaini, wagundue kweli uso wa baba  Mungu mwenye upendo. Wanaweza kujenga njia yao na kuujenga ulimwengu ulio bora. Hiyo ni kazi kubwa, Baba Mtakatifu anabainisha ambayo inasubiriwa  Baraza la kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kila aina ya taasisi ya kichungaji katika Kanisa.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.