Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Unaweza kuwa Baba,iwapo unamfanya mtu awe na imani na ujasiri wa kusema ukweli!

Ni huzuni kuona watoto wadogo hawajuhi hata kufanya hata ishara ya msalaba, badala yake wanawafundishwa kuchora vizuri picha ya msalaba - RV

26/01/2018 17:15

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta , Baba Mtakatifu amesistiza maneno matatu yanayo elekezwa na Mtume Paulo, hasa namna ya kutangaza Kristo kuwa ni mwana, kushuhudia na umama wa Kanisa. Unaweza kuwa baba iwapo utafanya mtu awe na imani na ujasiri wa kusema ukweli; kuwa mama wa kudumu muda mrefu katika umama wa Kanisa kwa maana hakuna maisha katika maneno matupu.Ni tafakari ya kina ambayo Baba Mtakatifu amejikita tarehe 26 Januari 2018,wakati Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya Mtakatifu Timoteo na Tito.

Ni mada ya imani ambayo imejikita katika mahubiri ya Baba Mtakatifu akitafakari  Barua ya Pili ya Mtakatifu Paulo kwa Tito Paulo  anawaalika wafuasi wake wawe na imani ya thabiti. Katika barua hiyo, Baba Mtakatifu anaonesha maneno matatu ambayo Paulo ameyatumia kuhimiza Timometeo kuyatazama kwa kina yaani kutambua mama, bibi na mwisho ushuhuda. Paulo alimpata mtoto Timoteo katika kiroho  kutokana   na kuhubiri kwake na kwa njia hiyo yeye anakuwa baba. Katika barua inaeleza hata machozi ya Paulo, si kwamba Paulo aliweza kusita kusema nusu ukweli, hapana yeye anatangaza kwa ujasiri. Na ujasiri huo unamfanya Paulo awe baba wa kiroho wa Timoteo, hiyo ni kwasababu ya mahubiri hayawezi kuwa baridi. 

Kuhubiri wakati mwingine ni kama kupiga kofi, lakini kofi ambalo linakusukuma kuondoka  mahali ulipo ili kwenda mbele. Mtakatifu Paulo alitajwa kuwa  yeye ni mwehu ,lakini wehu wake wa kuhubiri ulikuwa wa kusema, Mungu alijifanya mtu , akasulibiwa, lakini baadaye akafufuka. Je Watu  wa Atene walisemaje? tutakusikiliza siku nyingne(…) : Baba Mtakatifu anabainsha kuwa daima katika mahubiri ipo chembe ya wehu ,japokuwa bado kuna vishawisho ambavyo vyaweza  kutokeza uongo,sikweli,  kutania na wakati mwingine mahubiri kuwa ya baridi.

Akifafanua juu ya neno la pil kutoa ushuhuda: Baba Mtakatifu anathibitisha: ushuhuda lazima utolewe na ambao unatokana na nguvu ya Neno. Zamani wakristo walialikwa kujulikana kwa matendo yao na hasa ya kupendana kati yao.Katika ushuhudia ndipo Baba Mtakatifu anaonya kuhusu maneno matupu dhidi ya wengine: Leo hii kuna baadhi ya parokia, badala kunena pamoja na kupendana, wanaunda mitafaruko ya hapa na pale, kutokana na ulimi unaokata mwingine. Swali, utawezaje kuonesha  imani yako wakati umejaa masengenyeo na maneno.  Ushuhuda lazima utokane na kujuliza swali, je ni kwa nini kuwana  imani au ni kwanini nkufuata nyayo za Yesu kwa maana bila kujiuliza, ubaya unazuia kutoa ushuhuda na kudhoofisha imani za watu.

Katika suala la tatu,Kanisa kama mama: Imani inaoneshwa katika umbu,yaani umbu la Kanisa sababu  Kanisa ni Mama, Kanisa ni mwanamke. Umama wa Kanisa unadumu muda mrefu katika  umama  na kama bibi. Swali la kujiulza je mama   na bibi wanafanya kama kama watu wawili analiotajwa na  Mtakatifu Paulo?  ”hata bibi Loida na mama yako Eunice” ambao wameonesha imani inayolegea, lakini watajifunza zaidi wakienda katika katekisimu.

Baba Mtakatifu anaongeza, ni huzuni kuona watoto wadogo hawajuhi hata kufanya  ishara ya msalaba, badala yake wanawafundishwa kuchora vizuri picha ya msalaba. Hiyo ni kutokana na ukosefu wa mafundisho kutoka kwa mama na bibi wa watoto hao. Mara ngapi, Baba Mtakatifu ameongeza, anafikiria kuona mama wengi wanandaa watoto katika matayarisho ya kufunga ndoa, lakini je,  wanawafundisha  kuonesha imani?
Baba Mtakatifu amehitimisha akiomba kufundisha kushuhudia, kama wahubiri, hata wanawake kama mama na bibi kurithisha imani!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News


 

26/01/2018 17:15