2018-01-25 16:05:00

Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa Kanisa la Kiluteri la Finland!


Katika tukio la kuadhimisha kumbukumbu ya Mtakatifu Henrik. Kanisa la Kiinjili la Kiluteri nchini Finland, wamefanya hija mjini Roma, ambapo katika fursa hiyo wawakilishi wakiluteri wameweza kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 25 Januari 2018. Wakati wa kukutana nao, Baba Mtakatifu Francisko ametoa hotuba yake akimshukuru Askofu wa Espoo, kwa maneno ya hotuba yake na kwamba wanapohitimisha Juma la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, anapenda  kurudia kukumbuka kwa furaha Maadhimisho ya kumbukumbu ya mageuzi ya miaka 500 mwaka jana, ambayo yamezidisha juhudi  na kutafakari kwa kina katika Bwana wetu Yesu kristo juu ya umoja kati ya waluteri, wakatoliki na makanisa yote ya kiekuemene katika ulimwengu.

Akifafanua juu ya maaadhimisho hayo nasema, kumbukumbu hiyo ya pamoja inabaki kuwa yenye fursa kwa ajili ya mchakato wa kiekuemen kwasababu si katika hatua ya kufika mwisho, bali ni fursa ya nafasi ya kuanza hatua ya safari ili kutafuta uekumene wa umoja kamili unaoonekana kati  yetu chini ishara ya za aina tatu yaani kushukuru,kutubu na kuwa na matumaini. Ishara hizi tatu ni msingi iwapo tunataka kweli kuponya majeraha yetu ya kumbukumbu, anatuhibitisha Papa.Si kwa bahati mbaya Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, jitihada zetu zinaelekea katika upeo wa kutafiti masuala ya kiekumene katika lengo la kutazama upeo wa wakati ujao kwa namna ya pekee masuala ya asili ya Kanisa.

Umuhimu wa kumbukumbu ya pamoja ya mageuzi katika ulimwengu wote, Baba Mtakatifu anafafanua , ulikuwa ni mkubwa na wa maana  wa kiekumene katika maombi na katika mikutano ambapo hapakuonekana hata kidogo ugomv wa aina yoyote na migogoro ya wakati uliopita. Kumbukumbu hiyo iliadhimishwa katika roho nzuri na kuwa na utambuzi wa matukio ya mageuzi kama vile wito wa kukabiliana kwa pamoja kile ambacho kimepoteza uaminifu wa ukristo,pia ulikuwa ni kutoa wito kwa upya ili kuongeza juhudi za pamoja wakati wa kikiri umoja wa Mungu katika utatu. Mwaka ambao umamalizika hivi karibuni, umekumbusha kipindi ambacho umoja kati ya wakristo kuwa bado haujatenguka. Na ndiyo maana waluteri na wakatoliki wameweza kuadhaimisha pamoja kumbukumbu hiyo 2017 na hasa katika umoja wa kiekumene.

Baba Mtakatifu anaongeza kusema: kwa furaha anaionesha kupokea mikononi mwake  hati ambayo imetolewa hivi karibuni ya Kamati ya mazungumzo ya kiluteri na katoliki wa Finland yenye mada ya “Umoja unaokua: Ni Hati  inayohusu Kanisa , Ekaristi na utume”. Katika hati hiyo Baba Mtakatifu anasema zipo mada muhimu ambazo mazungumzo yanaweza kuendelezwa mbele. Hiyo kwasababu baada ya makubaliano kati ya waluteri na wakatoliki juu ya misingi inayohusiana na mafundisho ya haki , uendelezwaji wa Kanisa na makubaliano yanapaswa kuwa sehemu ya lazima katika hatua za kila siku kwenye mazungumzo ya kiekumene. 

Juma la Maombi ya umoja wa wakristo yafanyikayo kila mwaka yanakwenda samabamaba na hija yao, mahali ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema  “Mkono wako wa kuume ee Bwana una nguvu (Kut 15,6) na unatukumbusha hali ngumu wanayo ishi watu wengi katika dunia hii ambapo sisi wote tunalazimika kutelemka katika kambi, tukiwa tumeungana pamoja katika wajibu wa kiekumene anasema baba Mtakatifu.

Kwa unyenyekevu mwingi Baba Mtakatifu anasema tusali kwa Bwana wetu Yesu Kristo ili kwa neema yake , wakristo wote ulimwenguni waweze kuwa chombo cha amani yake. Na asaidie daima kwa watu waliogawanyika kati yao na kufanya kuwa mashuhuda, wahuduma ya upendo wake, ambapo wanaponyesha na kupatanisha , kutakatifuza na kusifu jina lake. Tuombe bila kuchoka msaada wa neema ya Mungu na mwanga wa Roho Mtakatifu anatakayetupeleka katika ukweli kamili. 

Sr Angela Rwezaula

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.