2018-01-22 14:26:00

Jimbo Kuu la Québec linaunganisha parokia kutoka 216 hadi 37 kufikia 2020


Ili kusaidia uinjilishaji, ramani ya mpango wa maparokia katika majimbo ya Québec nchini Canada inafanya uzoefu wa kina katika mabadiliko ya ukarabati mpya ya kuunganisha maparokia. Tangu tarehe Mosi Januari 2018 wameanza hatua ya pili ambayo imeweza kuona matokeo tayari kutoka parokia 130 hadi kufikia parokia 64. Na mnamo mwaka 2020 wanatarajia ukarabati huo uwe umekamilishwa, mahali ambapo wanatazamia kuwa na parokia 37. Mnamo mwaka 2011, walianza mchakato huo wa upunguzaji wa parokia  mahali ambapo zilikuwa parokia 216 kwa ujumla katika Jimbo Kuu la Québec.

Katika mtandao wa kijamii wa Jimbo Kuu la Quebec unaandika kuwa, ni muhimu uwepo wa mkusanyiko wa maparokia hizo katika  historia ya Kanisa Katoliki la Quebec.  Umuhimu wake msingi wa kuunganisha maparokia unatokana  kutengeneza nguvu zaidi za kuchugaji katika parokia hili ziweze kuwa hai na kusaidia mchakato mzima wa uinjilishaji. Aidha kikundi cha kichungaji kinakachoundwa kwa sasa  kinalazimika kufanya kazi kwa pamoja, kama alivyothibitisha Askofu Mkuu wa Quebec Kardinali, Gérald Cyprien Lacroix, kwa kuita kuwa ni “umoja wa jumuiya”. Umoja huo unaalikwa kujikita kwa namna  moja na mpya katika kushirikiana na kufanya utume  kwa pamoja ifikapo mwaka 2020. Na Jimbo Kuu limeweza kuweka kila aina ya zana  ya msaada na uwezekano wa kusaidia mchakato huo.

Aidha taarifa inasema kuwa Mashirika ya uendeshaji  (fabrique d’églises,) yaani kiwanda cha Kanisa, ambacho ni kitengo kinachohusika na usimamizi wa mali za parokia kama vile (majengo,makaburi na rasilimali za kiuchumi) ni nyeti sana, lakini  kitajihusisha  kuwainua mapadre na kutoa rasilimali zao kwa ajili ya utume wao wa kimisionari. Naye Kardinali Cyprien Lacroix anaandika tarehe 17 Januari 2018 kuwa, tendo la  kuunganisha makundi haya kichungaji, utasaidia katika kutoa  mapendekezo au kupyaisha mikutano binafsi na ile ya  jumuiya pamoja na Kristo katika kuunda jumuiya ya mitume wa kimisionari.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.