2018-01-19 09:02:00

Ujumbe wa Pamoja wa CCEE na CEC kwa tukio la Maombi ya Umoja wa Wakristo!


Ndugu wote katika Kristo ni kushuhudia matumaini ya kikristo katika jamii iliyomezwa na ulimwengu kwa “Mkono wako ee Bwana ni wa nguvu na utukufu " (Kut 15,6a) ambayo ni kauli mbiu  iliyochanguliwa kuongoza mwaka huu 2018 Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo. Kaulimbiu hiyo inakumbusha kuwa Bwana bado anashikilia ulimwengu na historia yake ambapo kuna ishara(Ef 1, 3-10) ya matumaini kwa ajili ya binadamu. Ulaya leo hii inahitaji matumaini  kwa maana ya kutaka kuondoa  kilio chake  katika  sura nyingi za wazalendo wa nchi zake. Hiyo ni kutokana na  utupu ambao unajionesha kutokana na ukosefu wa uwepo wa Mungu ndani ya maisha ya watu wengi. Ustawi wa kiuchumi peke yake hauna uwezo wa kukinaisha moyo wa binadamu. Mpango wa Ulaya ambao umelimbikiza utajiri wa kutoweza kujikimu na kujisaidia, wakati huohuo inaunda  umaskini mpya. Lakini anayejifunulia Injili anagundua mwingine katika mateso yake kama vile kwa wazee, kwa wale wasiokuwa na ajira; na  uhisi kuwa na mshikamano na mdhaifu ili aweze kumpatia matumaini.

Huu ni ujumbe wa pamoja kutoka Umoja wa  Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CEE), kwa njia ya Mwenyekiti wake, Kardinali Angelo Bagnasco na Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa Ulaya (KEK)  mchungaji wa Kianglikani Christopher Hill, uliotangazwa kwa waamini wote, kufuatia tukio la Juma la kuombea Umoja wa Wakristo, tukio ambalo limeanza tarehe 18-25 Januari 2018. Maaskofu wanasisitiza katika ujumbe wao kuwa, kama wakristo wanataka kuwa mashuhuda hai kwa wote na kuonesha  matumaini yao, yatokayo katika  mzizi wa maisha na Kristo. Kwa maana wanao uhakika kuwa katika Kristo upo uwezekano wa kuishi kwa utulivu leo hii katika historia kwa ajili ya kujenga wakati ujao ulo bora kwa upeo wa umilele!

Maskofu hao wakihamasisha matendo ya dhati hasa kwa kila binadamu na ulimwengu mzima, wanaonesha kuwa, yapo mambo mengi yanayoashiria hatari na aina nyingi za utumwa mamboleo hasa kuzidi kukandamiza  hadhi ya maisha ya binadamu aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Hawali ya yote wanafikiria wimbi la watu wanaolazimika kuhama kutokana na vita mabaya na umaskini kwa kuacha familia zao au nyumba zao.  Wanabainisha kuwa, wakati endelevu na ulio bora unawezakana, lakini ni kwa kufuata Mungu na uongofu wa mioyo kwa kupitia matendo ya huruma na kutafuta haki binafsi na kama jumuiya.

Makanisa ya kikristo barani Ulaya wanataka kushuhudia upendo wa Kikirsto kwa kila binadamu aliyeumbwa na mfano wa sura ya Mungu; kutokana na kwamba inawezekana kupatikana katika makanisa yote leo hii hasa  kujikita katika upendo wa dhati  na kuonesha umoja huo kwa njia ya mshikamano na ndugu wakristo wanaoishi katika hali mbaya ya maisha, ya upekwe na pembezoni; mshikamano na ndugu wakristo wanaoteseka kwasababu ya imani yao kwa namna ya pekee katika nchi za mashariki,Afrika na Asia;mshikamano kwa ndugu wa karibu wanaofika kubisha milango Barani Ulaya; uhamasishaji wa Ulaya ili waweze kuchukua jukumu la kusaidia watu wenye shida kiroho na kimwili hasa wazalendo wake; mwisho kuwa na uvumilivu wa mchakato wa kiekuemene. Mambo hayo yaliyotajwa na viongozi wa Makanisa,ndizo dharura na umuhimu wa umoja wa wakristo. Kwa njia hiyo, viongozi  wanawaalika waamini wote kuwa na uvumulivu katika matumaini na kushuhudia Injili kwa matendo ya huruma na dhati. Na ndiyo inayosisitiza na kusaidia wengine waweze kuwa na  utambuzi wa pamoja na mwisho kutunza  umoja  wa Roho kwa njia ya kiunganishi cha amani!

Sr Angela Rwezaula   
Vatican News!

 

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.