Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maisha Ya Kanisa Afrika

TOGO:Ujasiri katika kujenga amani unatokana na neema ya imani!

Migogoro nchini Togo zimeyumbisha uchumi wa nchi, hivyo ujasiri katika kujenga amani unatokana na neema ya imani - AFP

16/01/2018 14:31

Mwaka ambao umemalizika umekuwa ni kipindi kigumu cha mivutano iliyotokana na kipeo cha sera za kisiasa jamii, ambapo hadi sasa bado hali hiyo inaendelea katika nchi yote na kwa namna ya pekee katika ya kati nchini Togo. Si rahisi mbele ya ghasia za kila aina na migogoro ambayo haisemeki kuwa kweli mjenzi wa amani, lakini pamoja na hayo yote na udogo wao wamejaribu kupanda mbegu ndogo kila siku katika shughuli zao. Haya ni maelezo ya Sista Antonietta Profumo wa Jumuiya moja ya Shrika la Mama Yetu wa Mitume ambaye ni muhusika wa kituo cha Afya huko Koloware nchini Togo, akihojiana na shirika la habari katoliki la Fides.

Sista Antoneietta anasema kuwa, katika Kituo chao cha Afya ka kipindi cha mwaka uliopita wameweza kuwapokea idadi kubwa ya wagonjwa, wadogo kwa wakubwa kutoka kila sehemu ya nchi . Shukrani kwa wafadhili wao walio wawezesha kuwatibu watu wengi wa asili na kuwapa mambo muhimu kwa ajili ya afya bora. Watoto wengi wenye utapia malo wameweza kupona na kurudia hali yao ya kawada hadi kurudia kwa furaha. Huo ndiyo mchango wao mdogo wa kuhamasisha maendeleo, amani na ustawi wa watu katika jamii.

Sista anabainisha pia shughuli za walizotenda kipindi chote cha mwaka kuwa hata vijana wao 53 wenye ugonjwa wa ukimwi wameweza kushiriki baadhi ya mipango ya kichungaji kwa ajili yao. Ilikuwa ni fursa nzuri na utajiri mkubwa kuwahusisha viongozi wa kichungaji kwa vijana na watu kuwashirikisha. Vijana hao wamewasaidia watoto wa vijijini katika masomo yao, kutazama picha, michezo, ngoma hata uchunguzi wa afya zao.

Hata hivyo kuna mpango wa kuweza kuwasaidia kutibu watu wenye matatizo ya mtoto wa macho kwa mwaka mzima. Na kwa kipindi cha mwaka 2017 wamefanya operesheni 149 na wengine wako katika orodha ili waweze kupata huduma hiyo. Mwakilishi wa watawa hao amesema wao wataendelea kuota dunia iliyo bora, ya kindugu , mahali ambapo kila mtu anayo nafasi ma hadi ya kuheshimiwa na kupendwa, upendo unaoneshwa kwakatika Injili na Makat wa maisha!


Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

16/01/2018 14:31