Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Tafakari \ Makala

Askofu Kardijn ni mwanzilishi wa chama cha vijana wafanyakazi Katoliki

Kila mahali katika dunia utakutana na vijana wa chama katoliki cha vijana, kinachoongozwa na misingi mikuu ya uinjilishaji, mshikamano na upendo

13/01/2018 14:25

Wapendwa wasomaji wa Vatican news, ninawakaribisheni katika makala ambayo ninapendelea tutazame kwanza mada ya kuhusu maandalizi ya sinodi ya Maaskofu  mwaka huu inayohusu Vijana  yenye kauli mbiu Vijana imani na mang’amuzi ya miito, kwa kutaka kuhamasisha dunia ya watu wazima,jamii na Kanisa kwa ujumla waelewe moyo wa vijana na ili vijana waweze kugutuka kuwa wako machoni pa wote, Kanisa na jamii linawajali pia kuwa na shauku ya kuwakaribia, ili watembee kwa pamoja, kama sehemu ya mchakato wa hatua adilifu ya maisha yao.  Sehemu ya pili ambayo ni ndefu, nitawaletea historia ya  mmoja kati ya  mashujaa wa kiroho na upendo mkuu kwa vijana, ambaye alijitoa au aliitwa tangu mwanzo wa maisha yake kutembea  karibu na maisha ya vijana. Huyo ni  kiongozi wa Kanisa ambaye kwa miaka mingi aliweza kutetea maisha ya vijana wakristo na wasio kuwa wakristo kwa hali zote, hadi kuacha mbegu bora ambayo hadi leo shukrani kwa juhudi zake mbegu hiyo bado inaendelea katika ulimwengu mzima hasa wa vijana ni Padre Joseph Kardijn mwanzilishi wa Chama cha vijana wafanyakazi katoliki (ICYCW).

Ndugu wapendwa wasilizaji wa Vatican news, nikirudi katika mada ya vijana, changamoto haziishi katika mzunguko wa dunia hii, hasa ule unaotazama makuzi na malezi ya vijana, ndiyo maana mama Kanisa kwa njia ya Kiongozi wake mkuu na Khalifa wa mtume Petro anaendelea kusisitiza na kuwatazama kwa karibu, si yeye tu, kama nilivyokwisha dokezea, bali hata Mababa wote wa nyakazi zote za Kanisa hata sasa kila mahali walipo wanaungana kwa sauti moja  ya wito ili wajikite kwa namna ya pekee kuwa karibu na vijana.

Je ni kwa njia gani?:  Hawali ya yote upendeleo Baba Mtakatifu Francisko wa kuitisha Sinodi ya maaskofu,  ili wakutane kwa ajili ya mada ya vijana ni jambo msingi na la kupewa sifa na mtazamo mwema wa kutaka kuwa karibu na vijana katika moyo wa Kanisa; na pia wao watambue kweli nia kuu ya utashi wa Kanisa. Pamoja na kwamba zimetangulia Sinodi nyingine, bila kuzitaja zote,… lakini labda ile ya karibu na muhimu ambayo ni  Sinodi ya familia iliyoadhimishwa  mjini Vatican kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015. Kwa kuwakumbusha kidogo  ilikuwa na kauli mbiu  “Wito na utume wa Familia ndani ya Kanisa na Ulimwengu mamboleo”. Hata  sinodi hiyo ilikuwa muhimu hasa na inaendelea kuwapo  kwa kipindi hiki cha  changomoto kwa ujumla ndani ya Kanisa na jamii katika ujumla wake.

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana yanayotarajiwa kufanyika kuanzia 3-28 Oktoba 2018 yataongozwa na kauli mbiu “Vijana, Imani na mang’amuzi ya Miito”. Maandalizi  tangu  yafunguliwe rasmi mwaka jana, Sekretarieti kuu ya Sinodi za Maaskofu ilitoa  “Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya XV ya Maaskofu kwa ajili ya vijana”.  Hati hii ni imekuwa ni mwaliko mkuu na chachu hasa ikiwa inaonesha wito wa Yohane akifuasa Yesu, na mwanafunzi anayejulikana na wengi kwa ajili ya kupendwa zaidi na Yesu. Na kwa maana hiyo hati hiyo imeonesha hali halisi ambayo vijana wa nyakati zote wanawezaje kutembea katika hatua kama zile za mwanafunzi mpendwa wa Yesu, yaani Yohane! 

Tangu kutangazwa kwa hati hiyo, kwa ujumla majimbo mengi duniani, yamejikita kwa namna ya pekee kufanya maandalizi kuanzia katika maparokia,vyama vya vijana, kimajimbo, mikoa hata kitaifa.  Zaidi ya hayo Sekretarieti ya Sinodi imejaribu kufungua hata akaunti za mitandao ya kijamii, kwa kujali hata sehemu za kisasa ambazo vijana wengi wanapendelea, ili  kuwezesha hata nafasi ya  vijana wote wanao tumia mitandao hiyo waweze kujibu maswali yalitungwa kwa ajili yao  na hata wao waweze  kutoa hoja zao.  Majibu na hoja zao ziweze kuwasaidia maaskofu watakao kuwa katika sinodi hiyo kuweza kuingia moja ka moja kuzungumza katika moyo wa vijana.

Kwa namna moja au nyingine ndugu wasomaji wa Vatican News, shughuli kubwa kutoka ngazi ya juu ya  Kanisa inajitahidi, kinachobaki ni makanisa mahalia ulimwenguni, kwa ushirikianoa na maaskofu wa majimbo na hasa wahusika kichungaji kuanzia nzi ya jumuiya ndogondogo, parokia, jimbo wanafanya jitihada zipi? Ni cheche za moto zipi zinawasadia vijana kuanzaia ngazi za chini wanashirikishwa kikamilifu kuandaa sinodi ya maaskofu inayowahusu?

Aidha pamoja na sinodi hiyo kwa matashi ya Baba Mtakatifu, itatanguliwa lakini mkutano kabla ya sinodo , Mkutano utakao waona washiriki 300 kutoka dunia nzima, ambao ni vijana waamini wakristo na wasio wakristo. Mkutano huo unatajiwa kuanzaia tarehe 22-24 na 25 Machi 2018 Vijana hao watashiriki Siku ya  XXXIV ya vijana  kijimbo katika Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Mjini Vatican, mahali ambapo Baba Mtakatifu ataongoza Ibada ya Misa Takatifu. Kwa njia hiyo tunaweza kuthibitisha kuwa ni jambo msingi katika maisha ya Vijana ndani ya Kanisa la  ulimwenguni; ni kuonesha  bayana muungano wa vijana  kutoka pande zote za dunia kwa njia ya wawakilishi wake. Kwa ujumla, Sinodi ya Maaskofu ni nafasi nzuri kwa Mababa wa Kanisa, baada ya maandalizi yote hayo kuwasikiliza vijana mbashala sauti zao kupitia maoni yao na majibu ya maswali waliyowatumia kupitia mitandao. Itakuwa ni maadhimisho ya aina yake, maana ni sauti ya vijana watakaosikika katika sinodi hiyo. Na kwa maana hiyo Kanisa kupitia vyombo vyake vyote, linawaaalika wote vijana kuwahamasika, si tu vijana lakini pia watu wazima kwa  kuwahimiza vijana ushiriki wa kila tukio  hasa kila mahali penye fursa ya mikutano ya vijana.

Ndugu wasomaji wa Vatican News, kama nilivyotangulia mwanzo kusema kuwa baada ya kuona sehemu ya kwanza juu ya maandalizi ya Sinodi ya vijana, sehemu ya pili inataka kutazama tuite mabingwa wa uzoefu wa vijana ambao walitumiminia muda wao na maisha yao yote kwa kujikita barabara katika maisha ya vijana, na hasa kumtazama sura ya Askofu Joseph Cardijn mwanzilishi wa Chama cha Vijana wafanyakazi Katoliki. (YMCA)
Je alikuwa ni nani? 
Cardijn alizaliwa huko Schaerbeek tarehe 15 Novemba 1882  nchini Ubergiji. Ni padre ambaye maisha yake yote alijikita zaidi katika kukaribia hali halisi ya vijana wafanyakazi na wote ambao walianza kwenda mbali na Kanisa na kuwakaribia kwa kuwatangazia neno la kweli la uongofu, na akaweza kuaminika kuingia katika mawazo na mioyo ya vijana.  Alikulia,katika familia ya kawaida ya wafanyakazi. Babayake alikuwa mtunza bustani,mama yake alikuwa akifanya kazi katika nyumba ya tajiri mmoja katika mji Mkuu. Baada ya miaka 4 walihamia huko Hall Kaskazini ya Bruxelles, mahali ambapo walikuwa wanatokea ili kufungua duka moja la kuuza mkaa kwa ajili ya kusaidia familia.

Akiwa kijana alikuwa akimsaidia baba yake wakati wa kazi, pamoja na hayo haifanya asiendelee vizuri katika masomo yake shuleni, na aliweza kusoma kila kitu kilichokuwa anakiona machoni pake. Enzi zile watu walikuwa wanaanza kazi kwakudamka mapema sana.Watu hao walikuwa wakipitia karibu na nyumba yao, ambapo sauti za viatu vya wapita njia zilianza kusikikia kuanzia saa 10 na 11 moja alfajiri. Hakika maisha kwa hakika yalikuwa magumu sana enzi zile. Joseph alibahatika  kuanza masomo yake katika Chuo cha Notre Dame , pamoja na kwamba enzi zile rika lake ndilo sasa ilikuwa aanze kutafuta  kazi kwa ajili ya kuishi. Na hiyo ilitokana na hekima yake aliyokuwa nayo, kwani siku moja kabla ya kulala alianza mazungumzo na baba yake kama ilivyokuwa kawaida yake, lakini siku hiyo ilikuwa maalum kwani alimwambia Baba yake shauku ya kutaka kuendelea kusoma sana. Nia  ya kutaka kusoma sana ilikuwa ili aweze kuwa  kuhani.  Kwa maana hiyo alimwomba  baba yake ili asiende kufanya kazi bali aendelee na masomo.  Jibu la baba yake,utafikiri alikuwa amesha liandaa tayari, na kwa maana hiyo alimjibu kwamba, wao wamesha fanya kazi sana na kama wao ni maskini na wanaweza kuwa na zawadi kama hiyo ya kumtoa mtoto wao kwa Mungu , basi watanya kufanya kazi kwa juhudi  zaidi kwa ajili ya mtoto na maisha yao.

Ni jambo zuri kusikia utayari wa wazazi kutoka sadaka binafsi na hasa ya mtoto wao bila malalamiko. Kumbe katika mfano huo tunatambua wazi kwamba, wapo wazazi wengi ambao wanakuwa na upendeleo mkubwa zaidi wa kusikiliza sauti kutoka kwa vijana wenyewe, bila kulazimishwa, na ambao wanajibu ndiyo  iliyo kubwa ya kutaka kumfuasa Kristo. Hiyo inaturudisha hata sehemu ya kwanza ya mada ya vijana ambayo, Mama Kanisa linataka kutoa nafasi ya kusikiliza vijana, maana tendo la kutoa nafasi hiyo ni muhimu, maana inatoa uhuru wa kujieleza.

Hivyo basi tukiendelea na kijana wetu Joseph, hatua nyingine iliyofuata ilikuwa,  ni mwaka 1897 Joseph Cardijn aliondoka nyumbani kwao  na kujiunga na Seminari ya Malines. Na wakati wa masomo pia kilifuata hata kipindi likizo mahali amabapo Joseph alipata kukutana na vijana wenzake aliosma nao shule ya msingi, lakini wao wakaendelea njia ya kazi, lakini kwa bahati mbaya alikuwa wamegeuka kabisa ndani ya jamii,hata kuwa mbali na  imani kwa Mungu na Kanisa. Hali hii ilimtia wasiwasi lakini pia kuchota nguvu zaidi ya kuendelea katika wito kwa ili aweze  kuwasaidia; na ndiyo mwaka 1903 alipewa daraja takatifu la upadre  akiwa kweli na nia ya kusaidia uongofu wa wimbi za roho ya vijana wafanyakazi. Ndugu wasomaji wa Vatican News, tutaendelea na makala yetu kipindi kijacho, kwa kuendelea kuona sura ya baba huyo wa Kanisa Cardijn alivyo endelea na maisha yake kwa kuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki na maisha ya vijana....

Ni Sr Angela Rwezaula.

Vatican News.

 

13/01/2018 14:25