Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Sinodi ya Vijana 2018 ni kwa ajili ya kupyaisha uso wa Kanisa !

Pamoja na maandalizi ya Siku ya XXXIV ya Vijana huko Panama:inatanguliwa na mikutano muhimu ya maandalizi - RV

11/01/2018 14:00

Mwaka 2018 unawakilisha matukio muhimu na ya kina kwa upande wa utume kwa  vijana wa kizazi kipya: kwanza ni Sinodi ya Maaskofu kuhusu Vijana inayoongozwa na kauli mbiu  “Vijana, imani na mang’amuzi ya miito itakayofanyika mwezi wa Oktoba 2018 kuanzia tarehe 3 hadi 28, lakini ni  sinodi itakayofuatwa mara baada ya Mkutano wa Vijana wa Italia na Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 11 na 12 Agosti mjini Roma. Ni mkutano ambao utakuwa unahitimisha hija ya Vijana wote wa Italia katika maeneo muhimu ya kihistoria ya nchi hiyo.

Wakati huo huo kalenda inaonesha katika mantiki ya Sinodo ya Vijana kwamba kutakuwapo na mkutano wa vijana kabla ya Sinodi kuanzia tarehe 19 – 24 machi kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko, unaotarajia kuwaunganisha vijana karibia laki 300 ambao ni waamini wakristo  na wasio waamini kutoka pande zote za dunia. Na tarehe 25 Machi 2018 katika Sikukuu ya Matawi  katika viwanja vya Mtakatifu Petro itakuwa ni sikukuu Kimajimbo ya wanaadhimisha siku ya XXXIII ya Vijana. Katika matukio hayo yote pia yatakuwa katika maandalizi ya Siku ya XXXIV ya Vijana Duniani  itakayofanyika huko Panama, kuanzia tarehe 22-27 Januari 2019 barano Amerika ya Kusini.

Kwa kipindi chote hiki ni hatua ya kujikita katika kusikiliza na kuzungumza na vijana, lakini pia ni kama mwaliko kwa upande ulimwengu wa watu wazima, kutafakari kwa kina juu ya vijana wote wa leo na kizazi kijacho. Haya yamesemwa na muhusika wa huduma ya Kitaifa katika utume wa vijana kichungaji wa Baraza la Maaskofu nchini Italia Padre Michele Falabretti akielezea katika vyombo vya habari. Padre anaonesha bayana, bila hata kuficha makosa ambayo yanajitokeza, hasa akiomba ziachwe tabia za kutafakari vijana kama jambo ambalo halituhusu na  liko nje ya maisha yetu. Vijana ni kama chachu ndani ya maisha ya watu wazima na  tunapowatazama ni kama kioo katika maisha yetu! 

Hata Baba Mtakatifu wakati wa kutoa matashi mema ya Sikukuu ya Noeli alisema, kuwa makini kwa vijana haina maana ya kuwatazama wao peke yao bali hata kutazama ndani ya mioyo ya watu wazima zile cheche za moto katika madana maisha yak ila siku  kuwa na unyeti katika ya mahusiano na dharura. Hayo ni mahusiano ya kizazi endelevu, familia, katika maeneo ya kichungaji na maisha ya kijamii. Si kutazama vijana ili kuwasoma, badala yake ni kuwasililiza, kwasababu wao wanatufanya kutambua mambo mengi ya Kanisa ambayo watu wazima pamoja na kuwazaa vijana, wamejisahau. Mazungumzo kati ya kizazi yanasaidia watu wazima kutambua ulimwengu ambao watu watu wazima wanataka kutembea pamoja na vijana

Aidha Padre Falabretti akielezea juu ya lugha ambayo iweze kutumika labda kwa vijana, anathibitisha kuwa, si suala la lugha, katika  kuzungukia maneno, suala la msingi ni kwamba iwapo vijana leo hii wanaonekana kutafuta maana msingi ya maisha yao, lakini maana hiyo wanaitafuta katika sehemu nyingine, ni wazi kwamba hawana mfano wa kuiga na kuamininka kutoka kwa watu wazima amba wanawategemea,wala kuwa na nyenzo msingi za kuwasaidia, hivyo watu wazima hawawezi kuendelea kila mara kufikiria kuwa wanasababu, kwamba wanafuata ukweli na Injili. Maisha ya vijana leo hii yanaonesha wazi  na kueleza kuwa wanapotea njia kutokana na watu wazima kutojali au kukiuka misingi mikuu ya imani ambayo ingeweza kuwapa ujasiri wa dhati kukabiliana na maisha yao.

Ulimwengu wa watu wazima, anaongeza Padre Falabretti, kuwa unapaswa urudie kwa upya kuchota katika mzizi halisi wa imani, japokuwa inaoensha kuwa na hofu au woga wa kuoenekana kuwa hekima hiyo watu wazima hawana tena na wanapaswa kwa unyenyekevu kuitafuta.
Mizizi hiyo inajikiti katika hali ya uongofu wa kweli kwa njia ya moyo wa Injili. Huwezi kutoa kile ambacho hauna, na hivyo ili kuwa nacho kwa unyenyekevu , laizma utoke katika ushuhuda wa Injili na kuishi kwa matendo matendo ya dhati yanayoambatana na ishara za maneno na utashi wa kweli, hiyo ni inahitaji uthabiti wa watu wazima , kwa maana hatuwezi kusema dunia hii waliitaka wao , mana wameikuta hivyo.

Mabadiliko ya watu wazima, na uongofu ni jamabo msingi katika masuala ya man’amuzi ya vijana na maisha ya vijana. Kati ya dharura ya Injili na uzoefu wa maisha , kuna nafasi kubwa ambayo inaendelea kujikita katika mawazo ,na ambayo si rahisi kufanya kana kwamba hakuna kitu. Vijana wanhitaiji kuonesha udhati na uozoefu wa Injili, namana ya kuishini Injili kuanzia kwa watu wazima. Iwapo watu wazima hawajali, je inawezakanaje wao ndiyo nwafuate? 

Ni kwa njia hiyo ndiyo maana Baba Mtakatifu Francisko amerudia mara nyingi akisema,hakuna kipindi kama hawali cha Kanisa leo hii kutoka kujikita katika nafasi makini ya kusikiliza kizazi kipya. Hii ina maana kubwa na hasa katika maandalzi yote kuanzia mwezi wa tatu ambapo itakuwa fursa ya kusikiliza vijana , kama vile Sinodi itkavyo sikiliza mawaida kutoka kwao na ndiyo, anaongeza Pade… kuwa hii ni kuonesha mtindo wa kichungaji wa Kanisa zima la Ulimwenguni , kuwpa nafasi vijana! Kazi ya kawaida ya Sinodi, ni kutaka kuweka wazi na thabiti uhai wa Kanisa katika utume wa kichungaji wa Kanisa.

Padre amehitimisha kwa kusema kuwa, ikumbukwe kwamba tarehe 7 Desemba 1965 , mwisho wa Mkutano wa Mtakaguso wa Vatican II, waliandika ujumbe kwa Vijana wote duniani ili kusema kuwa Kanisa limefanya kazi kwa ajili ya kupyaisha uso wake. Kwa maana hiyo hatua ya mchakato wa  Sinodi ya Maaskofu wa kufikiria Vijana isaidie kupyaisha Kanisa  uso wake, kutoa chachu na nguvu  katika ndoto nyingi za vijana, kwa kutoa wito mkubwa utakao wahusisha na kuwagusa vijana kweli maisha yao.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 

11/01/2018 14:00