2018-01-11 14:36:00

Kard.Tagle:Tuwe chombo cha utetezi wa maisha,tumezaliwa na tutakufa bila uwezo!


Maisha hayajikiti juu ya kuwa na uwezo, kwani tumezaliwa bila kuwa na uwezo,hata tutakapokufa hatutachukua jambo lolote. Na kwa njia hiyo tujaribu kutafuta kuwa chombo cha utatezi wa maisha kwa ajili ya wengine. Ndiyo maelezo anayosisitiza Kardinali Luis Antonio G. Tagle Askofu Mkuu wa Jimbo la Manila na Mwenyekiti wa di Caritas Internationalis, wakati wa kuadhimisha misa ya usiku ,maadhimisho ya tukio la utamaduni kwa maandamano ya mti wa msalaba waKristo (Msalaba mweusi). Maandamano hayo yalifanyika usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 9 kwenye mitaa ya katikati ya mji Mkuu Manila  wa Ufilippini.

Wakati wa mahubiri yake, Kardinali Tagle ameshutumu vikali  tamaa na njaa ya kutaka uwezo au utawala wa dunia hii, akionya kwamba  kusahau umuhimu wa kutumikia Mungu, maana yake ni kuelekea katika njia potofu. Kila mwaka maandamano ya kupeleka njiani sanamu hii takatifu hufanyika kutoka katika Kanisa la Mtakatifu Nicola waTolentino kwenda katika Parokia ya Quiapo, ambapo madhimisho hayo huanza kwa novena tangu tarehe 31 Desemba ya kila mwaka na kumalizika tarehe 9 Januari. 

Mamilioni ya  waamini hukusanyika kusali kwa ajili ya kuomba neema au miujiza binafsi. Katika maadhinisho ya misa  ya Kardinali Tagle, idadi kubwa ya mapadre , maaskofu kutoka katika majimbo ya Kisiwa, walikuwapo; hata Balozi wa Vatican nchini Ufilippini Askofu Mkuu Gabriele Giornado Caccia.

Taarifa zinasema kuwa, hata mwaka huu, maandamano hayo ya Msalaba wa mti wa Kristo , umeweza kupitishwa katika njia za barabara za mji wa mkuu , ambao watu wengi, wakiwa wzalendo , hata watalii kujikita katika sala na maombi. Kati ya maadhimisho ya kidini ya aina hiyo maandamano ya Yesu mweusi wa Nazareth ni moja ya sherehe maarufu sana na ambayo watu wengi wa bara la Asia wanaudhuria.
 
Sanamu hiyo iliyochongwa ya msalaba wa Yesu inawakilisha Yesu aliyepinda chini ya msalaba mzito. Historia ya Msalaba huo, ilipelekwa katika mjini Manila na Padre mmoja wa Shirika la Mtakatifu Agostino kutoka nchini Uhispania mwaka 1607 ndani ya Meli iliyokuwa inatokea nchini Mexico.

Kwa mujibu wa maelezo, meli hiyo ilipatwa na moto na kuungua wakati wa safari, lakini uwakilishi wa msalaba wa Kristo ndani ya Meli hiyo kimiujiza haukuweza kuungua, japokuwa uliadili rangi na kuwa mweuzi kutokana na moshi.Maandamano hayo yanakumbusha kuhamishwa kwa sanamu hiyo tarehe 9 Januari 1767 na kwa njia hiyo mwaka huu ulikuwa na maana kubwa ya kuadhimisha miaka 250.

Wahusika wa usalama wa Kanisa la Quiapo wanaeleza kuwa idadi kubwa ya waamini ambao wameshiriki maandamano kwa mwaka huu 2018  ambao ni milioni 20 ni ongezeko la  asilimia 5% ya maandamano ya yaliyofanyika Januari 2017 yaliyodumu kwa masaa 21.Aidha Taarifa kutoka Asianews, kwa upand ew ausalama wanasema pamoja na wingi wa watu hao, ulinzi na usalama uliongezwa pamoja na kwa kwanza hawakupata habari zinazoashiria hatari, kwa njia hiyo maadhimisho yalikwenda vizuri. Vikosi vya ulinzi vilifanya kazi yeke barabara kwa maana polisi walikuwani 7,000, na wanajeshi 500.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.