2018-01-11 09:04:00

Dk.Tveit amesema nchi ya china itaongoza kwa wingi wa wakristo 2050!


Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, Dr. Olav Fykse Tveit,  amefanya maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza hilo  katika Kanisa la  Chongwemen nchini China, mahali ambapo amesema kuwa, kufikia mwaka 2050 nchi ya China inawezakana ikawa nchi yenye wakristo wengi zaidi katika ulimwengu. Dr. Olav Fykse Tveit aliyaeleza hayo  kwa maelfu ya waamini waliokusanyika siku ya Jumapili tarehe 7 Januari 2018  katika Kanisa la Chongwenmen mjini  Beijing, moja ya makanisa ya kiinjili maarufu la kihistoria na muhimu nchini China. Akiendelea na hotuba yake amesema,“uhai  na makuzi ya Kanisa nchini China umekuwa ni habari kuu muhimu kwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni kwa miaka kumi ya mwisho. Ushuhuda wenu wa kikristo ambao mnaupeleka mbele kwa uaminifu hata wakati mgumu sana, umeweza kutoa matumaini kwa walio wengi katika ulimwengu.”

Liturujia ya maadhimisho hayo tarehe 7 Januari 2018 mjini beijing ilikuwa ni tendo la kwanza  la kufungua ziara yake  rasmi ambayo kama  mwakilishi wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni anataendelea kufanya katika nchi hizo kwa siku zijazo; aidha ni ziara ya dhati inayokwenda sambamba na mwanzo wa maadhimisho ya miaka 70 tangu kuwanzishwa kwa chombo cha kiekuemeni chenye makao yake makuu Mjini Geneva. Kanisa hilo lilijengwa mwaka 1870 na Wamethodisti kutoka nchi ya Marekani,kwa njia hiyo Kanisa la Chongwenmen ni katika lenye kuwa na  historia ngumu ya ukristo katika nchi ya China. Kanisa hilo  lilichomwa na kuharibiwa wakati wa mapinduzi ya Boxer mwaka 1900 baadaye likapata ukarabati tena mwaka 1904; Lakini kama ilivyokuwa kama sehemu nyingine za kukatazwa madhimisho, Kanisa hilo lilifungwa tena wakati wa mapinduzi ya utamaduni kipindi cha pili cha miaka ya 60. 

Mwaka 1980 likafunguliwa kwa mara nyingine tena, ambapo  hadi  leo hii ni kituo hicho kinahesabiwa kuwa ni muhimu kwa jumuiya nzima makanisa ya kiinjili katika mji wa Beijing. Ni Jumuiya ambayo inaendelea kukua kwa haraka na muhimu katika nchi ya China kwa maana inasadikika kuwa ni milioni 23 ya waamini wa madhehebu matatu mama katika nchi ambayo yamezaa Kanisa la Kiinjili tangu mwaka 1991 na kuungana na Baraza la Kiekuemene la Makanisa ya China. 

Pamoja na hayo taarifa zaidi zinasema kuwa, ni waamini wengi zaidi wa kiinjili nchini China, hadi kukadiria kuwa ni  watu milioni 80 wanaojulikana na serikali na wasio julikana. Pamoja na kwamba bado yapo mateso makubwa ya waamini, lakinimateso hayo  hayazuii kabisa uuisho wa Roho Mtakatifu katika kazi ya ujilishaji wa ukristo katika nchi ya China. Na ndiyo maana uwepo wa mwakilishi mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kiekumene duniani katika mji huo na katika maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwake, ni kutaka kuhakikisaha hilo, na kama yeye mwenyewe alivyo thibitisha wazi kwa waamini wote waliokusanyika katika Kanisa  kwamba kufikia mwaka 2050 Kanisa la China linawezekana kuwa nchi ya kwanza ya kuongoza kuwa na wakristo wengi duniani.

 Na ndiyo maana kutokana na furaha na mateso ya ulimwengu, Mchungaji Tveit amewaalika wakristo wa China kuwa na mtazamo wa hali halisi wa wa upepo  unaovuma wa vita ambao umezunguka katika Peninsula za Korea hadi kufikia mateso ya Betlehemu na nchi zote za Mashariki kwa ujumla au kutazama pia umaskini ambao unazidi kuongezeka katika nchi nyingi. Akisisitiza hali masuala na changamoto za dunia anasema,leo hii katika ulimwengu siyo haki kusema kila kitu ni sawa au kusema ni dhambi, badala yake ni kutafuta namna ya kupokea wokovu wa dhambi na kujaribu kupambana zaidi dhidi ya mambo yaliyo hasi yatokanayo na makosa yetu binafsi. Mambo hayo anayataja kwamba yanaonekana katika mabadiliko ya hali ya hewa, katika migogoro, ukosefu wa haki, uchumi, uharibifu wa maisha na hata kwa kutumia jina la dini.

Hata hivyo kufuatia na ziara yake, taarifa zinasema kuwa, baada ya ziara yake mjini Beinjing, Katibu Mkuu  wa Kiekumeni wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, ataendelea na ziara yake huko Shanghai na Xi’ian , kabla ya kurudi Beijing kwa kwa ajili ya maadhimisho mengine ya kiliturujia katika Kanisa la kiinjili huko  Gangwashi, ambalo ni Kanisa la kizamani kabisa kati ya makanisa ya Kiinjili nchini humo China.Zaidi ya Makanisa mama matatu ya imani na Baraza la Makanisa nchini China, yanatarajia pia kufanya mkutano rasmi hata na wawakilishi wa utawala wa serikali kwa ajili ya masuala ya kidini.

Sr Amgela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.