2018-01-09 14:55:00

Watu wa El Salvador kuondolewa Kinga ya muda TPS nchini Marekani !


Marekani imetangaza kuondoa kinga kwa wahamiaji 200,000 kutoka El Salvador. Ni uthibitisho wa  Ikulu ya Marekani iliyotangaza hapo tarehe 8 Januari 2018, kwamba inaondoa kinga TPS ya muda kwa watu wapatao 200,000 kutoka El Salvador,na kutishia kuwafukuza maelfu ya familia nchini Marekani ikiwa bunge halitaweka sheria ya kuhalalisha kuwepo kwao. 

Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kirstjen Nielsen amezitaja sababu za kutoa kinga familia za watu walioihama El Salvador miaka ya mwanzoni ya 2000 kutokana na maafa ya tetemeko kubwa la mwaka 2001 kwamba hazipo tena. Kwa uamuzi huo wa Ikulu ya Marekani inasema, Wa El Salvador waliokuwa wakilindwa na kinga hiyo ya muda, maarufu kama TPS wamepewa muda  hadi tarehe 9 Septemba mwaka ujao wa 2019 kuwa wameondoka nchini Marekani.

Kituo kinachofuatilia masuala ya wahamiaji kimesema agizo hilo linaweza kuathiri familia 135,000 katika majimbo ya California na Texas. Kinga ya TPS vile vile imeondolewa kwa watu wengine 59,000 kutoka Haiti,pia 5,300 kutoka Nicaragua. Wabunge wa chama cha Democratic wamekosoa uamuzi wa kuwaondolea kinga hiyo watu wa El Salvador, wakisema nchi yao bado ni mahali penye hatari kwa maisha.

Hali kadhalika kufutia na maamuzi hayo,  maneno makali kutoka  Baraza la Maaskofu wa Marekani (USCCB) yametolewa na kuonesha  masikitiko yao ya kina ambapo pia khawakubalini na sera za siasa ya serikali ya sasa  na kwamba maamuzi ya kufunga kinga ya muda  (TPS) kwa watu Wa El Salvador ni ya kuumiza  ambayo itawaathiri pia  watoto zaidi ya 192,000 na familia zao. Familia nyingi watatengengana bila sababu msingi kutokana na maamuzi hayo. 

Katika taarifa liyotolewa na Fides, tarehe 8 Januari 2018 na kutiwa saini na Askofu msaidizi  Joe S, Vasquez wa Jimbo la Austin na Texas ambaye  pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Maaskofu wa Marekani kwa ajili ya Wahamiaji  inathibitisha wazi kuwa tarehe 8 Januari , Kitengo cha Ulinzi wa ndani (DHS) wametangaza kweli kufunga kwa kinga ya muda (TPS) kwa Wa el Salvador. Ambapo kwa miezi  18 iliyo baki hadi tarehe 9 Septemba waanze maandalizi ya kuondoka katika nchi ya Marekani.

Ujumbe wa Maaskofu wa Marekani uanaendelea kusema kuwa, pamoja na kutambua na kushukuru muda walio ongezwa wa kinga TPS; wao watakuwa bega kwa bega  kuendelea kuwalinda na   kujikita zaidi  katika  wasiwasi wa familia ya kibinadamu ya watu wa El Salvodor. Hivyo Ujumbe huo unatoa wito wa kufanya kazi kwa pamoja ili kutafuta suluhisho lao la kupata kinga TPS kwa muda mrefu na kwamba Kanisa liko tayari kusaidia juhudi hizo.

Ujumbe unaeleza kuwa walengwa wa kinga (TPS) ni sehemu ya pamoja ya jumuiya nzima, ya makanisa yote ya nchi na nchi kwa ujumla. Na hivyo wanasisitiza kuwa  bila Bunge la  Marekani kuingilia kati, maisha ya watu hawa itabadilishwa kabisa  na familia nyingi zitaharibika.

Aidha wanakumbusha kuwa kama ilivyotokea suala la “The Deferred Action for Childhood Arrivals (DACA) ambalo ni Sheria inayowatetea watoto na vijana wahamiaji ambao hawajuhi nchi nyingine zaidi ya Marekani waliozaliwa,iliyokuwa imetolewa na Rais mstaafu Barack Obama, na ambayo Rais Trump alitaka wapoteze haki zao ; maaskofu hao kwa upya, wanaiomba kwa nguvu zote Bunge na  wahusika wote wa Serikali kuunganika kwa pamoja ili kukabiliana na tatizo hilo mapema iwezekanavyo.  

Na kwa upande  wa wahusika wa suala hili la kinga (TPS) yaani Wa El salvador  Baraza la Maaskofu wanatoa ahadi ya kuendelea kuwa na mshikamano nao na kusali kwa ajili yao na  familia zao ambao wamerudikana au kulazimishwa kuacha nyumba zao. 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.