2018-01-09 14:34:00

Korea ya Kaskazini itatuma wawakilishi katika Olimpiki huko Korea ya Kusini!


Baada ya miaka miwili ya mivutano, mkutano wa kwanza wa wawakilishi kutoka Kaskazini na Kusini mwa Corea umefanyika tarehe 9 Januari 2018 asubuhi. Mapendekzo kutoka  Seoul  ni kuwa, wanariadha wa Kaskazini na Kusini waweze kuwa pamoja kufanya maadhimisho ya kufungua na kufunga michezo ya Olimpiki itakayoanza tarehe 9-25 Februari 2018! Na michezo hiyo inatarajiwa kufunguliwa huku Pyeongchang Kusini mwa Korea. 

Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mkutano wake na wanadiplomasia mjini  Vatican tarehe 8 Januari 2017, amesema, upo umuhimu wa kutafuta kila njia ya kuweza  kusaidia mazungumzo katika peninsula ya Korea ili mwisho wake wapate njia moja za kushinda mivutano ya sasa, kwa kukuza matumaini ya pamoja, na kuhakikisha wakati ujao wa amani ya watu wa Korea na ulimwengu mzima.

Aidha Kanisa  nchi ni Korea limasali sana kwa ajili ya mazunguzmo kati ya nchi mbili. Kabla ya mkutano  huo, Askofu wa Jimbo la Daejeon na mwenyekiti Taifa wa Haki na amani  ya Baraza la Maaskofu wa Korea alielezea shauku kubwa ya mkutano huo ambao umefanyika huko anmunjom kati ya wawakilishi wa Korea ya Kaskazini na kusini.

Askofu Lazzaro You Heung-sik wa jimbo la Daejeon akiliambia shirika la habari la Asianews, alisema furaha yake ni kubwa sana. Amesema kuwa wamefikia hatua hiyo shukrani za uvumilivu na msimamo wa Rais Moon Jae-in ambaye kamwe hakukosa kuacha milango wazi ili aweze kukutana na Korea ya Kaskazini, hata kipindi cha mivutano mikubwa ya miezi iliyopita. Askofu anasema kuwa Rais wakati wa hotuba yake ya mwisho wa mwaka alitumia lugha nzuri ambapo alikumbusha mara nyingi jinsi gani watu wa Korea mbili walivyo wamoja na wa rangi moja na kuonesha shauku hiyo ya makutano.

Amesisitiza kuwa, ushiriki wa Olimpiki kwa kipindi  cha baridi huko  Pyeongchang ni msingi. Na kwa njia hiyo ni matarajio yao kwamba wanariadha ya Kaskazini, hata washabiki kutoka huko, michezo na utamaduni wanaweza kuwafanya waungane zaidi pamoja. Lakini zaidi tendo la kukutana linaweza kuangusha zile hukumu na kudhihirisha kwamba silaha hazileti amani kamwe.

Tangu kuvunjika kwa mahusiano kati ya Korea hizo mbili mwaka 1953, familia nyingi ziligawanyika kati ya Kusini na Kaskazini, na si rahisi kutembeleana. Kwasababu wapo karibia watu 60,000 ambao wanazidi kuwa wazee, lakini ambao wanendelea kuimarishwa na matumani ya kuweza kuwaona siku moja ndugu na jamaa kabla kabla ya kifo chake. Kwa mara ya mwisho ya kukutana na familia hizo ulifanyika mwaka 2015.

Kwa upande wa suala la familia Askofu Yo amesema ni mada ya uchungu sana kwasababu inaonesha historia ya mateso ambayo yapo katika Korea ya Kaskazini na Kusini. Na kwa njia hiyo ni mategemeo yake, wanaweza kufungua mshikamano wa viwanda katika maeneo ya Kaesong na utalii katika mlima wa Kumgang kwa maana hapo ndipo kuna uwezekano wa fursa za kukutana na mazungumzo yanayosaidia ukuaji wa matumaini na mashikamano halisi kati ya Korea mbili.

Habari kutoka Asianews zinaelezea kwa kiefu juu ya mapendekezo  ya kukutania nchi mbili kwamba ni muhimu sana yaliyotolewa katika mkutano wa asubuhi ya tarehe 9 Januari 2018 kati ya wawakilishi wa kutoka sehemu zote mbili za Kaskazini na Kusini ambao wamekutana kwa mara ya kwanza tena mara baada ya miaka zaidi ya miwili katika mji wa Panmunjom, eneo lenye ulinzi mkali wa kijeshi. Aliyeongoza wawakilishi kutoka Seoul alikuwa ni Cho Myoung-gyon, waziri wa nchi ya Korea ya Kusini kwa ajili ya Muungano; na mwakilishi wa  Pyongyang  alikuwa ni Ri Son-gwon, mwenyekiti wa Kamati ya muungano wa amani katika taifa.

Zaidi ya mapendekezo kuhusu wanariadha kuwa pamoja; mkutano  wa asubuhi pia umetoa pendekezo la uwezekano wa  mkutano na chama cha Msalaba Mwekundu ili kujadiliana kuhusu kuwakusanya familia zote zilizotengana, lakini mkutano huo utaandaliwa wakati wa sikukuu ya mwaka mpya, inayotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi wa Februari 2018, ambapo ndiyo itakuwa kweli katikati ya michezo ya Olimpiki kwa kipindi cha  baridi kali. Pamoja na hayo kutoka Seuol, wamependekeza uwepo wa  mkutano  wa ngazi ya juu kati ya wanajeshi ili kuweza kuzuia uwezekano wa ajali katika mipaka.

Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Korea ya Kusini Bwana Chun Hae-Sung, akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Mkutano huo amesema kuwa, Korea ya Kusini wameshauri pia  ulazima wa kusitisha mara moja matendo ambayo yaweza kuongeza mivutano katika Kisiwa cha Korea na kuanza mazungumzo ili kuleta amani katika peninsula hiyo hasa zaidi uwezekano wa kusitisha silaha za kinyuklia.

Kwa upande wake pia amesema, Korea ya Kaskazini kwa sasa watajitahidi kuwatu wawakilishi wa michezo, hata wawakilishi wa  ngazi ya juu ya serikali, wanamichezo, vikundi vya mashabiki, wasanii, makundi ya mchezo wa taekwondo: (huo ni mchezo wa bondia ulioanzishwa kwenye miaka ya 40 na 50 ambao pia ni mchezo wa kitaifa katika nchi ya Korea ya Kusini, ambao msingi wake ni kama mchezo wa mpira japokuwa usanii wa mapambano ndiyo unaohesabiwa zaidi ) na waandishi wa habari.

Mkutano uliofanyika umetokana mara baada ya Kim Jong-un katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka akielezea juu ya uwezekano wa wanariadha wa Kakazini kushiriki michezo kipindi cha baridi kali, kwa kukubali mialiko uliyokuwa imetumwa siku zilizopita na Rais wa Korea ya Kusini Bwana Moon Jae-in. Kim alikubali mara baada Seoul na Washington kuamua mwezi wa Aprili kuondoa mazeozi ya wanajeshi.

Kwa upande wa Pyongyang mazoezi hayo ni sawa na mtindo wa  maandalizi katika vita. Kati wa wataalam wengi wa kisiasa wapo wanao muunga mkono Moon Jae-in kwa ajili ya umakini na msimamo wake wa kujaribu kuongeza mazungumzo ya kweli kati ya nchi ya Kaskazini, wakati huo huo ya kutaka kusimamisha tabia inayojionesha kupiga kwato na nchi ya Marekani.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.