Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa:Yesu anashiriki ubatizo wa kutakaswa kama binadamu katika mto!

Watu waliobatizwa na Yohane walikuwa na shauku ya utakaso wa dhambi zao - ANSA

07/01/2018 14:54

Leo hii ni sikukuu ya Ubatizo wa Bwana na kumalizika kipindi cha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ambapo tunaalikwa kutafakari Ubatizo. Bwana alitaka kupokea ubatizo uliokuwa umetangazwa na kufanywa na  Yohane Mbatizaji katika mto wa Jordani. Huo ulikuwa ni ubatizo wa kutubu: kwa maana wale wote waliojikita katika ubatizo huo, walikuwa wanajieleza shauku ya kutaka utakaso wa dhambi zao kwa msaada wa Mungu; hivyo walikuwa wakijibidisha kuanza maisha mapya.Ni mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Mama Kanisa akiwa anaadhimisha siku ya Ubatizo wa Bwana ambao unafunga siku kuu zote za kuzaliwa kwa Bwana tarehe 7 Januari 2018.

Baba Mtakatifu mesema kutokana na tukio hilo, tunaweza kutambua  unyenyekevu mkubwa wa Yesu, ambaye hakuwa na dhambi lakini anajipanga mstarini na wenye kutubu, anajichanganya nao ili aweze kubatizwa katika maji ya mto. Kwa kufanya hivyo yeye anajionesha kwa  kila ambacho tumeadhimisha katika sikukuu ya Noeli:  yaani uwezekano wa Yesu kujitosa katika mto wa binadamu ili kubeba  udhaifu na makosa ya binadamu; kushirikishana nao shauku ya kutaka ukombozi na kutoka kushinda kila aina ya kitu ambacho cha mfanya mwanadamu huyo kuwa  ambali na Mungu na ndugu. Kama vile Bethlehemu  hata njia ya kulekea mto Jordani, Mungu anaendelea kuonesha ahadi yake ya kuchukua mzigo wa mwanadamu; kwa njia hiyo Yesu ni ishara wazi na ya mwisho.

Baba Mtakatifu akifafanua kuhusu Injili ya siku ya Matakatifu Marko: “mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na roho  kama hua, akashuka juu yake”: (Mk 1,10) anassema, ni Roho aliyekuwapo wakati wa uumbaji, aliye mwongoza Musa na watu wake katika jangwa na sasa anashuka kwa ujazo juu ya Yesu na kumpa nguvu za kutimizia utume wake katika dunia. Ni aliye juu wa Ubatizo wa Bwana, hata kwa ubatizo wetu. Anayefungua macho ya moyo katika ukweli na ukweli wote. Anayesukuma maisha yetu kujikita katika njia ya upendo. Ni  zawadi ya Roho ambayo baba alimtendea kila mmoja, siku ile ya ubatizo. Ni roho ambaye anarithisha huruma na msamaha wa Mungu. 

Na zaidi ni roho Mtakatifu anayesikika katika Sauti ya Mungu akinena” wewe ndiye mwanangu mpendwa wangu. Na Sikukuu ya Ubatizo wa Yesu inatualika  hata kufanya kumbukumbu ya ubatizo wetu.  Baba Mtakatifu amesema kuwa, yeye hawezi kuwakumbusha siku yao ya ubatizo kwa maana, walio wengi walikuwa ni watoto, kama yeye wengi walibatizwa wakiwa watoto, lakini amewauliza swali iwapo wanajua tarehe waliyo batizwana kama wamesahau, wakirudi nyumbani waulize mama, baba, mjomba bibi, babu wasimamizi tarehe yao ya kuzaliwa.

Aidha anasisitiza: Na tarehe hiyo daima iwe katika kumbukumbu yao,kwasababu ni siku ya sikukuu; ni tarehe ya kuonesha mwanzo wa utakatifu,pia ni tarehe ambayo Baba ametuzawadia Roho Mtakatifu anayetusukuma katika mwendo wa imani; ni tarehe ya msamaha mkubwa na hivyo Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba, wasisashu tarehe ya ubatizo huo! Amemamlizia akisema, kwa maombezi na ulinzi wa Mama Maria Mtakatifu tumwombe ili wakristo wote waweze kutambua zaidi zawadi ya ubatizo na kuwajibika katika kuuishi kwa dhati, kushuhudia upendo wa Baba Mwana na Roho Mtakatifu!


BAADA YA MAHUBIRI YAKE NA SALA YA MALAIKA WA BWANA:

“Ndugu zangu kaka na dada ninawasalimia waamini wa Roma na mahujaji wa italia na wote  kutoka katika nchi tofauti. Niwasalimia kwa namna ya pekee watu kutoka nchi ya Korea ya kusini na wa Biella.“Hata waka huu sikukuu ya Ubatizo wa  Yesu, nimepata furaha ya kubatiza watoto 34 . Juu ya yao na juu ya watoto wote waliobatizwa siku za hivi karibuni, ninawaombea ulinzi wa Mama wa Mungu, ili kwa msaada na mfano wa wazazi wao na wasimamizi wao katika ubatizo, wakue kama mitume wa Yesu”.

Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari ya Neno la Mungu wakati wa sala ya malaika wa Bwana Jumapili 7 Januari 2018 katika viwanja vya Mtakatifu Petro. Na kwa wote amewatakia  matashi mema ya Jumapili  na safari njema ya mwaka ambao umeanza hivi karibuni ; “shukrani kwa mwanga ambao tumepewa na Yesu katika Noeli yake”. Aidha Wasisahau kazi yao aliyowakabidhi kufanya nyumbani yaani, kutafuta tarehe gani ya ubatizo wao!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

07/01/2018 14:54