Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa:Rithisheni watoto imani kwa njia ya lugha mama ya kuzaliwa!

Papa Francisko amebatiza watoto 34 katika Kanisa la Sistina Mjini Vatican , tarehe 7 Januari 2017, mama Kanisa akiadhimisha sikukuu ya Ubatizo wa Bwana - ANSA

07/01/2018 14:43

Katika  Siku kuu ya Ubatizo wa Bwana, Jumapili tarehe 7 Januari 2017, Baba Mtakatifu Francisko amebatiza watoto 34 katika Kanisa dogo la Sistina mjini Vatican. Baba Mtakatifu wakati wa mahubiri yake bila kuandika amesema wazazi wameleta watoto wao, katika ubatizo, kama hatua muhimu ya kwanza na shughuli waliyo nayo wazazi ya  kuweza kurithitisha na kuonesha imani hiyo, kwasababu peke yetu hatuwezi. Ili kuweza kuonesha imani hiyo Baba mtakatifu anabainisha kuwa ni  kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetoa uwezo huo wa kuirithisha na ndiyo maana wao wameweza kupeleka watoto wao ili waweze kupokea Roho Mtakatifu, kupokea Utatu Mkatatifu ambao ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu aweze kuishi katika mioyo yao.

Baba Mtakatifu pia maeongeza kusema: anataka kuwaeleza  jambo moja muhimu ambalo kama wazazi wanapaswa kufanya na jambo hili ni kwamba; ili kuweza kurithisha imani hiyo, inawezekana tu kutumia lugha ya familia, kwa maana ya lugha ya kuzaliwa ya  baba na mama, babu na bibi. Ndipo baadaye watafuata makatekista ili kuongezea mahali ambapo tayari watoto wamekweisha rithi  yaani kwa mawazo na maelezo zaidi, lakini jambo muhimu, Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba, wasisasahau hilo kuwa, imani inaridhishwa kwa njia ya  lugha ya kwanza ya kuzaliwa . Na lugha hiyo ikikosekana,hasa  iwapo wazazi hawaongei lugha ya upendo na kurithisha,  Baba Mtakatifu amebainisha kuwa, siyo rahisi na haiwezekani imani hiyo kukua.

Shughuli  msingi ya wazazi ni ile ya  kurithisha imani ambayo inaweza kufanyika kwa njiatu  ya  lugha ya upendo , lugha ya familia,kwa maana hata watoto wana lugha yao ya kwanza ambayo ni vizuri zaidi kuisikiliza,  amesema Baba Mtakatifu. Kwasasa wote wametulia tu, lakini yatosha mmoja aanze na tamasha zima litafuata!. Hiyo ndiyo lugha ya kwanza ya watoto! Baba Mtakatifu amethibitisha. Aidha ameendelea kusema kuwa, Yesu anashauri  kuwa kama wao na kuzungumza kama wao. Ni lazima kutosahau lugha ya watoto ambao wanaongea kadiri wawezavyo, lakini lugha hiyo ndiyo upendeleo mkuu wa Yesu;katika sala zao fupi na rahisi kama wao, wazazi wamwambie Yesu yote ambayo yamo ndani ya mioyo yao kama watoto wafanyavyo! Amewashauri Baba Mtakatifu Francisko!

Halikadhali amesisitiza kuwa, leo wao watazungumza kwa machozi lakini ndiyo lugha ya watoto. Ni lugha ya kuzaliwa ya wazazi ambayo ni upendo wa kurithisha imani na lugha  ya watoto ambao wamekubaliwa na wazazi wao na kuwafanya wakue katika imani. Na mwisho amesema, wakati wa kuanza ubatizo ndipo itasikika tamasha lao kwasababu ndiyo mtindo wao au wahisi  joto kali au wengine hawajisikii vizuri, wengine wana njaa, lakini kama wana njaa basi wazazi wasiwe na woga wawape chakula kwasababu hata hiyo ni lugha ya upendo! 

Ikumbukwe kwamba hata katika tweet ya Baba Mkatifu  Francisko, siku ya Jumapili tarehe 7 Desemba 2018 ikiwa Mama Kanisa  anaadhimisha sikukuu ya Ubatizo wa Bwaana; pia ikiwa ni sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu, katika nchi za Wakristo wa Mashariki yaani (Waorthodox), Baba Mtakatifu amesema, jina la Ubatizo pia ni mwanga ambao imani inaangaza moyo na kufanya tuone mambo mengine katika mwanga.  Lakini imani hiyo inawezakana kuirithisha tu kwa njia ya lugha  mama ya kuzaliwa.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

07/01/2018 14:43