Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa:Nia ya maombi ya Januari 2018 ni kwa ajili ya madhehebu madogo Asia!

Tusali kwa ajili ya nchi barani Asia, kwa ajili ya wakristo na madhebu yaliyo madogo, ili wote wapate kuishi na kujieleza imani yao katika uhuru - AP

06/01/2018 10:35

Kama ilivyo kwa kila mwezi, Baba Mtakatifu ametoa ujumbe kwa njia ya video, kwa ajili ya nia ya maombi ya kila mwezi. Kwa nia ya maombi ya mwezi Januari 2018, mawazo ya  maombi ya kitume yanawaelekea makundi madogo madogo ya kidini katika bara la Asia. Baba Mtakatifu anasema, katika kutofautisha dunia ya utamaduni barani Asia, Kanisa lazima kukabiliana na matatizo mengi hatarishi, ambapo kama  kazi ya utume, imeendelea kuwa ngumu kutokana na uchache wa makundi ya kidini.

Hatari hizo na changamoto zake, lazima kushirikishana na tamaduni nyingi za dini zilizo ndogo ambazo zinaunganisha shauku ya matumaini, ukweli na utakatifu. Halikadhalika Baba Mtakatifu amesema, tunapofikiria wengi wanaoteswa kwa ajili ya dini yao, ni lazima kutazama zaidi ya upeo wake na utofauti katika maadhimisho au imani. Ni lazima kuwa karibu na wanaume na wanawake wote, ili kupambana katika  kutangaza kila mmoja utambulisho wake.

Baba Mtakatifu anamalizia ujumbe wake kwa njia ya video kuwa,tusali kwa ajili ya nchi barani  Asia, ikiwa ni kwa ajili ya   wakristo  na madhebu  yaliyo madogo,  ili wote wapate  kuishi na kujieleza imani yao katika uhuru.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News 

 

06/01/2018 10:35