Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Papa:Dumisha utamaduni wa makutano,mshikamano kati ya shule na familia

Papa Francisko awataka waalimu kudumisha uhusiano mwema kati ya familia, shule na serikali ili kujenga kizazi cha jamii inayowajibika barabara. - ANSA

06/01/2018 10:51

Ninawakaribisheni nyote wawakililishi wa Vyama wa Walimu Katoliki Italia, katika tukio la Mkutano wenu wa kitaifa, shukrani kwa Mwenyekiti anayeng’atuka kutoka madarakani kwa  maneno yake.Ninapendea kuwapatia maneno matatu ya kutafakari na ambayo ni wajibu.Maneno hayo ni utamaduni wa makutano,mshikamano kati ya shule na familia, elimu ya ekolojia;vilevile la mwisho kuwatia moyo katika kutambua maana ya kuwa mwanachama. Hayo ni maneno ya hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 5 Januari 2018 aliyoanza nayo, wakati  alipokutana  mjini Vaitican na wawakilishi wa Vyama vya walimu Katoliki nchini Italia, ikiwa ni siku ya kuhitimisha  Mkutano wao wa XXI wa kitaifa.

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake, amewashukuru kwa machango wao wanaotoa katika shughuli ya Kanisa ya kuhamasisha utamaduni wa makutano. Anawatia moyo kuendelea kufanya hivyo ikiwa inawezakana kwa namna ya kuendeleza shughuli hii nyeti kwa kujikita zaidi kwa nguvu zote. Waalimu wa kikristo na kama wanafanya kazi katika shule katoliki au katika shule za serikali, wanaitwa kuhamasisha wanafunzi ili wawe wazi kwa wengine, kumtazama mtu kama ndugu na dada, kumtambua na kuheshimu historia yake, sifa zake, kasoro na udhaifu, utajiri na vikwazo.

Lakini ahadi ya kutenda,ni ile ya kushirikiana katika kuunda vijana walio wazi, wenye kupenda kujifungua katika hali halisi inayowazunguka; wenye uwezo wa kutunza; kuwa na ukarimu;kuwa huru kwa kupinga kuchukia mtu bila sababu, ambayo imesabambaratika kwa mujibu wa kutaka kuonekana au ulazima wa ushindani, ukatili, kuwa wagumu kwa wengine, hasa kwa wale ambao ni tofauti, wageni au kwa kila kitu kwa namna ambcho unonekana ni kikwazo.
Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, hiyo ndiyo hali halisi ambayo kwa bahati mbaya watoto wa siku hizi wanapumua ndani ya jamii n ana katika familia,  kwa njia hiyo ili kuzuia hali hii isiendelee ni lazima kufanya  kila njia kwamba hawapumui hewa hiyo ya utofauti, bali wavute hewa ya ubinadamu zaidi. Na ndiyo Lengo muhimu la kwanza la kuwa na mshikamano kati ya walimu na  wazazi.

Akifafanua neno la pili  yaani ya mshikamano wa elimu kati ya shule na familia, Baba Mtakatifu amesema, wote wanafahamu agano hilo, ambapo kwa kipindi kirefu  katika kipeo, kumekuwapo na kesi nyingi ambazo zinaonesha wazi kuvunjika kwa ushirikiano kati ya shule, familia na Serikali; agano hilo limevunjika anasisitiza,  na kwamba  ni lazima kuanza kwa upya ! Zamani kulikuwapo na juhudi za pamoja kati ya ushawishi kutoka kwa walimu na kwa wazazi;  Lakini leo hii hali hiyo imebadilika, japokuwa amebainisha kwamba, haiwezekani kamwe  kutokumbuka wakati uliopita. Ni lazima kuanza upya katika  matendo ambayo kwa ukimya  yanajikita kwa undani zaidi ikiwa ni familia na shule na  wajibu wa kujenga ushirikiano kwa ajili ya watoto na vijana.

Iwapo mkakati huo auonekani  kwa namna ya asili, basi ni lazima utafuta njia kwa mbadala ya kupanga hata kwa mahusiano ya watalaamu katika  kambi za elimu. Lakini kabla ya kufikia hapo, ni vizuri kujikita kwa kina katika  ugumu  huo kati ya walimu na wazazi. Hawali ya yote, Baba Mtakatifu anelekeza njia: ni lazima  kuacha kufikiria na kumwona mwengine kama mpizani na  kulahumiana  mmoja na mwingine. Badala yake ni kunyenyekea na  kujiweka katika nafsi ya mmoja na mwingine, ili kuweza kutambuw matatizo ya mmoja na mwingine ambayo leo hii yanajitokeza kwa ngazi ya mafundisho; hivyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema,inahitajika kuunda kwa nguvu zaidi mshikamano na ushirikiano!

Kipengele cha tatu ambacho Baba Mtakatifu amesisitiza ni kuhusu elimu ya Ekolojia, kutoka katika waraka wake kuhusu utunzaji wa mazingira wa Laudato Si. (Enc. Laudato Si’, 209-2015). Kwa ujumla si  jambo la kutoa baadhi ya ujuzi, lakini zaidi ni kuelekeza na kufundisha. Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, hii ni katika kufundisha mtindo wa maisha unaojikita katika tabia ya kutunza mazingira ambayo ni nyumba yetu ya pamoja na ambayo Mungu aliumba. Ni mtindo wa maisha ambao si ule wa kiulimwengu kama vile wa kutambua kutunza vema wanyama na kuacha kutunza wazee; au kutetea msitu wa Amazon wakati huo huo kuacha kutetea haki za wafanyakazi ambao wanapaswa kuwa na haki ya mshahara wao na mambo mengine.

Ekolojia ambayo ni lazima kuelimisha, pia lazima ishirikishwe anasema Baba Mtakatifu!  Na zaidi ya elimu, lazima ilenge maana ya wajibikaji:Akifafanua amesema, si kuwawekea kauli mbiu ambazo wengine lazima  wafanye, badala yake ni  kuchochea hali ya kufanya uzoefu wa maadili ya ekolojia, kuanzia  katika uchaguzi na matendo ya ishara za kila siku. Ni mtazamo wa tabia ambayo katika mantiki ya kikristo hupata maana na motisha katika uhusiano na Mungu aliyeumba na mkombozi, pamoja na Yesu Kristo, kiini cha historia ya  ulimwengu kwa njia ya  Roho Mtakatifu na kisima  cha umoja katika uelewano wa kazi ya uumbaji.

Mwisho Baba Mtakatifu amependelea kuongeza neno juu ya thamani ya kuwa na kufanya uanachama. Ni thamani na si mchezo, inabidi kuimarisha hasa kwa kipindi kama hicho cha mkutano kwamba kinasaidia kwa hilo. Baba Mtakatifu amewahimiza kurudia kwa upya kuwa na  utashi wa  kufanya uanachama katika kumbukumbu ya kanuni zenye kuchochea, kwa kusoma ishara za nyakati na kwa kuangalia wazi katika upeo wa kijamii na kiutamaduni. Wasiogope tofauti, pia  migogoro ambayo kwa kawaida ipo katika vyama vya kilei na kwamba  wasiifiche, lakini  wakabiliane kwa mtindo wa kiinjili katika kutafuta wema wa chama, kwa kupima katika misingi ya kanuni za kisheria . Kuwa na mwanachama  ni thamani na jukumu ambalo limekabidhiwa kwao sasa anathibitisha Baba Mtakatifu na kuongeza; Kwa msaada wa Mungu na wachungaji wa Kanisa, wanaitwa kutengeneza talanta hizi zilizowekwa katika mikononi mwao. Amemalizia kwa shukrani na kuwabariki wote, chama na kazi zao!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

06/01/2018 10:51