Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Baraza la Kipapa la Makleri wameunda Clerus App, je ni kitu gani?

Baraza la Kipapa la Makleri kwa ushirikiano na Sekretarieti ya mawasiliano wameunda Clerus App, inayohusu mahubiri ya kila Jumapili - AP

03/01/2018 16:00

Hakuna maonesho katika rejio, hata mahubiri marefu hadi kufikisha masaa mengi ambayo yanafanya waamini wakimbie makanisa. Ni moja wapo ya maelezo ya  Baba Mtakatifu Francisko ambaye aliweka bayana hali halisi katika maadhimsho ya misa hasa kwa upande wa mahubiri kuwa, lazima yawe mafupi ili kuepuka kufanana na mkutano au kipindi darasani,ni katika maneno yanayosomeka kwenye Waraka wake wa Evangelii Gaudium (Furaha ya Injili). Baba Mtakatifu Francisko anaongeza; inawezekana muhubiri kuwa hai kwa waamini kwa lisaa limoja, lakini neno hilo likiwa ni muhimu  katika maadhimisho ya imani. Kutokana na wito huo, Vatican imeamua kuunda “Clerus App”! Je ni kitu gani?

Hii ni nyezo msingi ya kuweza kuwa karibu na maparoko kusaidiana katika maandaliza ya tafakari yak ila Jumapili. Hayo ni maelezo ya Mosinyo Andrea Ripa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri  kwa ushirikiano na Sekretarieti ya Mawasiliano, ambao wameunda  hiyo  “Clerus App” inayohusu mahubiri na tafakari za kila Jumapili. Akifafanua Padre Ripa anasema hii haina maana ya kutaka kufundisha namna ya mapadre kuandaa mahubiri,hata kuwalekeza au kupangia mantiki zao. Lengo lao ni kutaka kuchangia mawazo kutokana na shughuli mbalimbali za utume walizo nazo ili kuweza kuandaa mahubiri yao.

Na kwanjia hiyo Padre Marko Ivan Rupnik Mjeusiti maarufu duniani katika kazi zake za kisanaa kama vile michoro ya  Kanisa Kuu la Fatima na huko Mtakatifu Yohane Rotondo , ambaye pia ni mtaalimungu na mwandishi wa vitabu vingi ataweza kuandaa mahubiri na tafakari hizo ambayo zitatolewa kwa mara ya kwanza katika lugha ya kitaliano.

Kusoma kile anachoandika Padre Rupnik, anaongeza Monsinyo Ripa, kwa hakika mawazo yake yanawakilisha mfano mwema. Lakini kila mmoja anaweza kuchukua kile ambacho anahitaji; kwa maana wapo ambao wana shida katika maandalizi na wengine wapo wenye uwezo. Lakini kuwa na nyenzo kama hiyo ni jambo muhimu amethibitishaMonsinyo Ripa. Pamoja na hayo pia amasema, hawawezi  kutotilia mkazo kuhusiana na  msisitizo wa Baba Mtakatifu Francisko juu ya mahubiri yanavyotakiwa kuwa mafupi. Na kwa njia hiyo wamefikiria kuunda jambo hilo kama kupanua huduma ambayo pamoja na kwamba ilikuwa tayari inatolewa katika mitando ya kijamii kuwasaidia watu kuwa karibu zaidi.

Taarifa inasema kuwa kila wiki wataweka mapendekezo kadhaa ya mahaubiri, ambayo yatawawezesha wote wanaotamani kutafakari kwa kina Neno la Mungu katika maandalizi ya Jumapili. App hiyo inawalenga zaidi hasa maparoko na makuhani wote lakini pia hata kwa wote wanaotaka kutafakari kwa kina la Neno la Mungu…..

Aidha katik kitabu cha mahubiri ya Mjesuiti Padre Marko Ivan Rupnik, upo uwezekano mwingine: mahali ambapo waweza kuchagua ukubwa wa maneno, kati ya rangi mbili za chini na kuratibu mwanga. App hiyo ni burepia ipo sauti au maandishi, upo uwezekano wa (download) kupakua au kuhifadhi mahubiri ili uyatumie baada ya kuondoka katika mtandao.

Tafakari hizo unaweza kushirikisha wengine katika mitandao ya kijamii. Kwa sasa unaweza kupakua kutoka (Play Store ) na siku zijazo itakuwa katika (App Store) kwa lugha ya kitaalino; wakati huo huo ikiwa katika machakato wa kutafsiri katika lugha mbalimbali, hivyo wanasisitiza kuwa, mahubiri hayo si kwa mapdre tu. bali hata kwa wote wenye mapenzi mema ya kutaka kutafakari kwa kina:  kila alhamisi Clerus App hitakuwa inasasishwa!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

03/01/2018 16:00