Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Papa:Tuinue macho na kutazama Mama Maria katika safari ndefu ya 2018!

Mama Maria ni mfuasi wa kwanza wa mwanae Yesu na Mama wa Kanisa - RV

02/01/2018 09:15

Katika sura ya kwanza ya kalenda ya mwaka mpya ambayo Bwana anatuzawadia, Kanisa linahimiza kutazama picha nzuri ya Sikukuu ya Liturujia ya Mama Maria, Mama wa Mungu. Na hivyo katika siku ya kwanza ya mwaka, tuinue macho yetu kwa kumtazama yeye, ili kuanza upya safari mdefu yenye njia nyingi za wakati hini ya ulinzi wa umama. Ni tafakari ya Baba Mtakatifu aliyo anza nayo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, katika viwanja vya Mtakatifu Petro, Mama Kanisa akiadhimisha Siku ya kwanza ya mwaka ambayo ni sikukuu ya Mama Maria Mama wa Mungu inayokwenda sambamba na siku ya amani duniani 2018.

Baba Mtakatifu anacambua Injili ya siku ya Mtakatifu Luka kwamba, inatupeleka moja kwa moja katika holi la ng’ombe huko Betlehemu. Wachungaji walifika kwa haraka na kumkuta Maria, Yosefu na kitoto kichanga, walipata kueleza yote waliyo ambiwa na Malaika na kwamba mtoto mchanga ni Mwokozi. ( Lk 2,16-21) Wote walishangaa, wakati huo huo Maria kwa upande wake aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake. (Lk, 2,19). Maria natufanya tutambue jinsi gani ya kupokea tukilo la Noeli. S kulipokea kijujuu tu, bali ndani ya moyo. Anatuonesha ukweli na namna ya kupokea zawadi ya Mungu, hata katika kuyaweka katika moyo na kutafakari. Baba Mtakatifu anahimiza kuwa, ni mwaliko wa kila mmoja kusali kwa kutafakari na kuonja zawadi hiyo ambayo ni Yesu mwenyewe.

Ni kutafakari Maria ambaye Mwana wa Mungu amechukuliwa mwili. Lakini umama wa Maria haupunguzi neema ya imani yake, yeye pia ni mfuasi wa kwanza wa Yesu. Na hiyo najipanua katika umama wake. Ni imani ya Maria ambayo itasababisha uwepo wa  ishara ya muujiza wa kwanza huko Kana, kwa maana ishara hiyo iliweza kuchangia na kuimarisha imani kuu ya wafuasi wa Yesu. Imani yake mwenyewe ya Mama Maria daima ipo na inaonekana hata  akiwa chini ya Msalaba na kumpokea Yohane mtume wa Yesu na mwisho baada ya Ufufuko, anakuwa Mama katikati ya maombi ya Kanisa ambalo Roho Mtakatifu alishuka juu yake siku ya Petenkoste.

Kama Mama, Maria anachukua nafasi maalumu ssana, yeye yupo kati ya Mwanae Yesu na watu katika hali zao halisi kama vile ukosefu wa mahitaji, umaskini na mateso. Ni mwombezi, na kwa kutambua kuwa yeye ni mama,  anapaswa kuwakilisha kwa Mwanao mahitaji ya watu, hasa walio dhaifu na wanye kuhitaji. Na katika hao watu, Baba Mtakatifu anaongeza kusema, ndiyo maana imetolewa mada ya Siku ya Amani duniani ambayo leo hii inaadhimishwa kwa kauli mbiu “Wahamiaji na wakimbizi: wanaume na wanawake katika kutafuta amani”. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesema kuwa, anataka kuwa sauti ya ndugu kaka na dada wanaotafuta wakati endelevu katika upeo wa amani. Katika amani hiyo ambayo ni haki kwa wote, hasa kwa walio wengi wambao wako tayari kuhatarisha maisha yao katika safari, ambayo sehemu kubwa ni ndefu na hatari, kukabiliana na ugumu na mateso (Taz ujumbe wa Siku ya Amani Duniani 2018,1)

Baba Mtakatifu amesisitiza kuseama kuwa, tusizime matumaini katika mioyo yao, tusikanyage matarajio yao ya amani! Ni muhimu kwa kila mmoja, taasisi za kiraia, elimu na Kanisa kuwajibika kwa kila hali na kila mmoja kuhakikisha kuwa wahamiaji na wakimbizi wanapata amani kwa siku zijazo. Bwana atujalie kufanya bidii katika mwaka huu, kwa ukarimu ili kuweza kukamilisha ulimwengu wa mshikamano na wa mapokezi.
Baba Mtakatifu anawaalika wote kusali kwa ajili hiyo, wakati huo huo kwapamoja amewakabidhi kwa Maria mama wa Mungu na Mama yetu katika mwaka 2018 ambao umeanza.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News.

02/01/2018 09:15