Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Mheshimiwa Padre Cristobal Romero ameteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Rabat

Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Cristobal Lopez Romero, S.D.B. kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Rabat, Morocco. - EPA

30/12/2017 09:36

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Vincent Landel wa Jimbo kuu la Rabat, Morocco. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa Padre Cristobal Lopez Romero, S.D.B. kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Rabat. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mkuu mteule Lopez Romero alikuwa ni Mkuu wa Kanda ya Wasalesiani wa Maria Auxialiadora, nchini Hispania. Alizaliwa tarehe 19 Mei 1952 huko Hispania.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kitawa, akaweka nadhiri zake za daima tarehe 2 Agosti 1974 na kupewa Daraja takatifu ya Upadre tarehe 19 Mei 1979. Tangu wakati huo, katika maisha na utume wake kama Padre amekuwa: mhudumu wa wakimbizi na wahamiaji; amejihusisha na utume kwa vijana; Paroko na Mkurugenzi mkuu wa Jalida la Wasalesiani huko Asunciòn. Padre Mkuu wa Kanda na Mkuu wa Jumuiya. Mara kadhaa amekuwa pia katika malezi na Jaalim kwenye vyuo vikuu kadhaa ndani na nje ya Morocco.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

30/12/2017 09:36